Dkt. Mwakyembe mambo mazito: Ripoti ya ugonjwa wake yaivuruga Serikali

Mkuu tujuze tu kulikoni karudishwa mapema?maana anaonekana dhahiri yu mgonjwa sana! kuhusu report angeisoma tu maana apparently hachomoki! na mtu hafi mara mbili


Mwakyembe kapewa sumu ..tena sumu kali...kurudishwa kwake huku ni kwamba hakuna uwezekano wa kupona na hivyo hakuna haja ya kuendelea na madibabu ghali huko..amepewa dawa za kutuliza maumivu tu lakini visigino na sehemu za kucha zinamuuma sana maana kunapasuka .....na hili limechezwa vizuri sana na wahusika wakuu wa mpango huu ili arudi.......
 
Si utuambie basi chanzo cha ugonjwa wake kama kinajulikana??


chanzo cha ugonjwa ni sumu aliyopewa mwaka jana.....na kwa mujibu wa wahusika wakuu waliofanya ufedhuli huo wanadai file la huyu mwakyembe lilifungwa rasmi mwaka jana mwezi august likifuatiwa na sherehe fupi ya kupongezana...walichokuwa wanataka wamekifanikisha na huyu dk hawezi kurudi katika hali yake ya kawaida....
 
Nipo nafuatilia kila post, ila niseme tu kuwa ripoti yangu ile itasimama daima!

mkuu hivi umepta nafasi ya kumuona sasa hivi alivyo??...anatia huruma sana...japo anatabasamu lakini ni mgonjwa sana...rafiki yake sasa (6) hata maji ya ofcn mwake hanywi, wala knywaji chochote.....na hatumi mtu ...anaenda dukani na kununua mwenyewe.....maisha gani haya!!!! full wasi wasi
 
Kama kawaida hili sakata la sumu liliibuliwa humu na kupewa uzito na JB lakini kama kawaida ya magazeti yetu kwa makusudi wanasema eti Sitta ndio aliibua kwa mara ya kwanza! Wakati hata huyo Sitta alipeleka polisi ushahidi wa maelezo ya JB! Kwanini magazeti yanakataa kuipja credit JF? Au ndio lile bifu la magazeti kudoda maana wasoma magazeti wakubwa wameacha kununua sababu kila kitu kinapatikana hapa!

Ndo maana yake.
 
Mwakyembe kapewa sumu ..tena sumu kali...kurudishwa kwake huku ni kwamba hakuna uwezekano wa kupona na hivyo hakuna haja ya kuendelea na madibabu ghali huko..amepewa dawa za kutuliza maumivu tu lakini visigino na sehemu za kucha zinamuuma sana maana kunapasuka .....na hili limechezwa vizuri sana na wahusika wakuu wa mpango huu ili arudi.......

Roho yangu inaniuma sanamoyo wangu unamlilia Dr Mwakyembe eeh mola mpe ujasiri atuambie watanzania kwa kinywa chake kabla hajafa
 
chanzo cha ugonjwa ni sumu aliyopewa mwaka jana.....na kwa mujibu wa wahusika wakuu waliofanya ufedhuli huo wanadai file la huyu mwakyembe lilifungwa rasmi mwaka jana mwezi august likifuatiwa na sherehe fupi ya kupongezana...walichokuwa wanataka wamekifanikisha na huyu dk hawezi kurudi katika hali yake ya kawaida....

Sidhani kama watakuja kuepuka mkono wa Mungu ,ndio wamepongezana lakini yatakuja kuwarudi Mungu si wa kuchezea
 
RIPOTI ya ugonjwa unaomsumbua Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, imeendelea kuivuruga serikali, safari hii Wizara ya Mambo ya Ndani ikisisitiza kuwa Wizara ya Afya ndiyo inayopaswa kuzungumzia suala hilo.

Kauli hii mpya toka Wizara ya Mambo ya Ndani imekuja ikiwa ni takriban wiki moja tangu gazeti hili lilipomuuliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni, kuhusiana na ripoti hiyo na kusema kuwa suala hilo haliwahusu. Uamuzi wa Tanzania Daima Jumatano kutaka kupata kauli toka Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo kimantiki inashughulikia madai ya jinai ulikuja baada ya kile kinachodaiwa kuwa ripoti ya ugonjwa wa waziri huyo kutoka kwa madaktari bingwa wa hospitali maarufu ya Apollo nchini India ambayo hadi sasa imebaki kuwa siri, inadaiwa kueleza chanzo cha ugonjwa wa Dk. Mwakyembe kuwa umetokana na sumu kali aliyowekewa hapa nchini.

Gazeti hili jana lilimtafuta Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, kutaka kupata kauli yake juu ya ripoti hiyo na tuhuma zinazotajwa ambapo alisema mwenye uwezo wa kuzungumzia juu ya ripoti hiyo ni Mkemia Mkuu wa Serikali toka Wizara ya Afya. Alipoulizwa na gazeti hili anazungumziaje juu ya kile kinachodaiwa Dk. Mwakyembe kuwekewa sumu hapa nchini, Waziri Nahodha alijibu kwa sauti kali kidogo: “Aa..ah, sikiliza; wenye uwezo huo nimekwambia ni Wizara ya Afya, mimi kama Waziri wa Mambo ya Ndani kuzungumzia suala hilo ni mpaka niletewe taarifa kama mtu anatuhumiwa kwa sababu wizara yangu inashughulika na kesi za jinai.

“Sasa sijaletewa taarifa, mimi ripoti siijui, ripoti za afya za watu ziko Wizara ya Afya... hao si ndiyo wanawapeleka watu India?...Sijaletewa ripoti sijaiona na sidhani kama nitalewa,” alisema. Alipoulizwa kwa nini anasema hadhani kama ataletewa ripoti hiyo je hakuna taarifa zinazodai kuwa ugonjwa unaomsumbua Dk. Mwakyembe unatokana na sumu? Bado aliendelea kusisitiza kuwa hajapokea taarifa zozote za mtu kutuhumiwa kumuwekea sumu Dk. Mwakyembe na kusisitiza kuwa kama gazeti hili linamfahamu mtuhumiwa huyo basi limtajie. Hata hivyo ingawa taarifa rasmi ya serikali haijatolewa, ripoti ya ugonjwa wa waziri huyo kutoka kwa madaktari bingwa wa hospitali maarufu ya Apollo nchini India ambayo hadi sasa imebaki kuwa siri inadaiwa kupelekwa serikalini kupitia Wizara ya Afya.

Taarifa za Dk. Mwakyembe kuwekewa sumu, mara ya kwanza ziliibuliwa rasmi nchini na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye ni rafiki mkubwa na mshirika wa karibu wa Dk. Mwakyembe katika mapambano dhidi ya ufisadi nchini katika mahojiano na kituo cha televisheni cha ITV katika kipindi chake cha dakika 45 kilichorushwa mwaka jana. Sitta alisikika akisema kuwa wasiwasi huo wa Dk. Mwakyembe kuwekewa sumu unatokana na mabadiliko ya ngozi na nywele alivyoondoka navyo nchini kwenda India.

Kwa Mujibu wa Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), alisema alipokwenda kumwona Dk. Mwakyembe nyumbani kwake, alipata mshtuko mkubwa kwani ilikuwa ni mara yake ya kwanza katika umri alionao kushuhudia ngozi ya mtu ikitoa unga. Sitta alikaririwa akisema, “Kuna kitu kama mba kwenye nywele na kwenye ngozi ya Dk. Mwakyembe. Akishika hivi, baadhi ya nywele zinadondoka. Mkono umevimba, sehemu mbalimbali. Mke wake alichukua video. Alikuwa anatuonyesha kwenye laptop (kompyuta ndogo). Kwa kweli inatisha.” Hata hivyo, Sitta alihojiwa na polisi kuhusiana na taarifa hiyo kwa madai kuwa ingeweza kuhatarisha amani, lakini alipotakiwa kutoa ushahidi anadaiwa kutoa ushahidi wa habari za kwenye mitandao ya kijamii.

Kabla ya Dk. Mwakyembe kwenda India kutibiwa, kulikuwa na uvumi kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa kiongozi huyo kulishwa sumu, ingawa yeye binafsi hajakanusha wala kuthibitisha habari hizo. Katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu aliporejea nchini, Dk. Mwakyembe alisema ripoti ya ugonjwa wake iko serikalini. Hata hivyo, serikali hadi sasa imekataa kuitoa hadharani ripoti hiyo ya madaktari bingwa wa Hospitali ya Apollo, India, waliomtibu Dk. Mwakyembe. Habari zaidi zinasema kuwa mwanasiasa huyo amepania kuianika ripoti hiyo hadharani kama serikali itaendelea kuifanya kuwa siri.

Dk. Mwakyembe alipelekwa India Oktoba 9 mwaka jana na kurejea nchini Desemba 11 mwaka jana hata hivyo licha ya kupata matibabu nchini India na kuendelea na tiba hiyo hapa nchini, hali yake bado siyo ya kuridhisha kwani amenyonyoka nywele, kope, nyuzi na hata vinyweleo vyote mwilini.


Source: Tanzania Daima 11/01/2012

KITENDO CHA MAAFISA WA SERIKALI KUPISHANA KAULI KINAZIDI KUONGEZEKA KASI SIKU BAADA YA SIKU. WAPEMBUZI WA MAMBO YA KIJAMII WANAJUA MAANA HALISI YA WATU KUPISHANA KAULI NA SABABU YA HIZO SINTOFAHAMU. KAMA ASILI YA UGONJWA WA DK NI SUMU??NINI KIFANYIKE ILI KUBAINI MAHARAMIA WALIOMDHURU DK MWAKYEMBE??JE NI WATETEZI WANGAPI WA RASILIMALI YA TAIFA HILI WATADHURIKA KWA UTARATIBU HUU??WAPO WAPI WALE WANAINTELLEJENSIA WETU MAHIRI WA KUZUIA MAANDAMANO YA CHADEMA, WAPO WAPI WALE MAJEMEDARI WA KUSAFIRISHA KWA NDEGE ZA KIVITA VIONGOZI WA CHADEMA KUWAPELEKA MAHAKAMANI KUHUDHURIA KESI???MBONA HATUWAONI KAZINI, MMEGOMA KUFANYA KAZI AU BADO MNASUBIRI MAELEKEZO KAMA KAWAIDA YENU?? HIVI NI KWELI MPO KWA AJILI YA USALAMA WA RAIA WEMA AU MNATUMIA HUO KAMA MSEMO KUJUSTIFY MALIPO YA MISHAHARA YENU KUPITIA KODI ZA WANANCHI MASIKINI????INAUMA SAAAANA. I STRONGLY BELIEVE KWAMBA IPO SIKU MATESO HAYA YATAKUWA HISTORIA!!!!SUALA LA SIKU HIYO NI LINI NAOMBA NAWAACHIE WANANCHI WAAMUE WAO SIKU WATAYOONA INAFAA KUACHANA NA HAYA MATESO YA KUJITAKIA! HIVI KWELI TANZANIA IMAFIKA MAHALI HAPA???NINI CHANZO!!!

Mungu akupe nguvu Dk. Mwakyembe, wananchi wengi sana wapo nyuma yako wakikuombea upone maradhi yanayokusumbua. Kwa kuwa repoti ya tatizo lililokupata ni haki yako, wananchi wengi sana wangeshukuru kama ungewajulisha kilichojiri ili tuweze kuchukua tahadhari stahiki.

Tumo hatarini iwapo tutakuwa tunaendeshwa na shutuma badala ya ushahjidi. Si gazeti ,si Mwakyembe mwenyewe, si Sitta wala mtowa mada alikuja na ushahidi. Kazi kwelkweliiiiiii!
 
mwenye haki akitawala watu hufurahi , bali mwovu atawalapo mioyo ya watu hutaabika. Mwakyembe hakuchaguliwa kuwa waziri kwa nia nzuri ya mtu wa kuwatumikia wananchi hapana! alipewa nafasi ile kwa nia ya kupumbazwa ili ajisahau nakuangukia katika mtego wa maadui zake ambao ndio waliopendekeza apewe uwaziri. nae bila kujihadhari kama mwenzake Sitta, masikini amenasa katika wavu waliomtega waovu. kwa sasa sidhani kama kuna tunaloweza kufanya zaidi ya kumwomba Mungu mwenye kuitizama haki akulipizie kisasi dhidi ya hawa waovu wanaoidhulumu haki yako ya kuishi.
 
mkuu hivi umepta nafasi ya kumuona sasa hivi alivyo??...anatia huruma sana...japo anatabasamu lakini ni mgonjwa sana...rafiki yake sasa (6) hata maji ya ofcn mwake hanywi, wala knywaji chochote.....na hatumi mtu ...anaenda dukani na kununua mwenyewe.....maisha gani haya!!!! full wasi wasi
kaka pole sana kwani wewe umepata fursa ya kumwona hivyo unayo haki ya kuuzunika,lakini angalia usije ukawa umeona kwenye

picha kama sisi pia, alafu ukaamua kua ndiyo ushamuona..,nikuambie kitu mkuu wangu huyu mwakyembe siyo shujaa au jasiri kama

kama watu wengi wanavyoamini,kwanini nasema hivi.?.hapo alipo kweli inawezekana kabisa asipone kwa habari tunazozipata kupitia vyombo vya habari.,sasa kama kweli anajitambua kwamba watu wake wanamjali na kutaka kujua hali yake na ukweli wa swala zima

basi angeonyesha ujasiriwa kuzungumzia hili jambo hata kwa maandishi ili kuondoa wasiwasi kwa wapendwa wake,lakini hadhubutu ni mwoga ,anaogopa hawa jamaa watakuja kumalizia bila kufahamu kwamba amekwisha teyari...mashujaa hawakai kimya eti kusubiri
kufuata taratibu,yeye anazidi kudhoofika kila siku sasa ni taratibu gani anasubiri ndiyo atueleze..???????.
 
Ozzie!
Nakubaliana na wewe kwa asilimia 80%. Dr. Mwakyembe ameponzwa na unafiki. Kuna msahafu unasema dhambi huzaa mauti. Kama angesema yote ya kweli kuhusu Richmond ingebidi Serikali ijiuuzulu na ufisadi wa awamu hii ya nne na King pin wake Rostam Aziz ungekoma. Ufisadi una tabia ya kinyonga kubadili rangi tu Kama CCM walivyotaka kufanya. Una sifa ya utandawazi na hujirudia kila baada ya miongo kwa staili mpya. Ripoti original ya Richmond RA anayo na hawatakuwa salama watakufa wajumbe wote ndiyo security code ya mafia. Dr. Mwakyembe has no option but to go for glory aimwage hadharani afe Kama shujaa. Kwa uhakika ile sumu naifahamu inaua taratibu.Akiamua kutokusema basi hata huko aendako ataadhibiwa. Asiogope Serikali ya CCM na wana CCM watapita lakini na sisi wote pia ila Tanzania is here to stay.Msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Mungu ibariki Tanzania bila viongozi wake!:A S 465:
 
Nisomapo taarifa ya afya ya dr. Mwakyembe au nisikiapo ikisimuliwa mtaani naumia sana. Nampenda sana achilia mbali mapungufu yake. Sidhani kama anatambua kwamba kuna watu tunaumia roho kwa sababu yake, hata kama hatujui. Kama nikweli alilishwa sumu akisema itasaidia sana katika kulinda usalama wa wapigania haki tanzania.
 
Ozzie!
Nakubaliana na wewe kwa asilimia 80%. Dr. Mwakyembe ameponzwa na unafiki. Kuna msahafu unasema dhambi huzaa mauti. Kama angesema yote ya kweli kuhusu Richmond ingebidi Serikali ijiuuzulu na ufisadi wa awamu hii ya nne na King pin wake Rostam Aziz ungekoma. Ufisadi una tabia ya kinyonga kubadili rangi tu Kama CCM walivyotaka kufanya. Una sifa ya utandawazi na hujirudia kila baada ya miongo kwa staili mpya. Ripoti original ya Richmond RA anayo na hawatakuwa salama watakufa wajumbe wote ndiyo security code ya mafia. Dr. Mwakyembe has no option but to go for glory aimwage hadharani afe Kama shujaa. Kwa uhakika ile sumu naifahamu inaua taratibu.Akiamua kutokusema basi hata huko aendako ataadhibiwa. Asiogope Serikali ya CCM na wana CCM watapita lakini na sisi wote pia ila Tanzania is here to stay.Msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Mungu ibariki Tanzania bila viongozi wake!:A S 465:
Asante kiongozi MOKEREMA.,What you've just wrote here is fact of what every one needs to know n no more bla bla.
 
Nisomapo taarifa ya afya ya dr. Mwakyembe au nisikiapo ikisimuliwa mtaani naumia sana. Nampenda sana achilia mbali mapungufu yake. Sidhani kama anatambua kwamba kuna watu tunaumia roho kwa sababu yake, hata kama hatujui. Kama nikweli alilishwa sumu akisema itasaidia sana katika kulinda usalama wa wapigania haki tanzania.
we Didia wala usisononeke hata kidogo huyo unayemuona kama mtetezi wa nchi yetu mr.mwakyembe hakujali wewee hata kidogo

kila kitu alichokuwa akifanya ni kwa manufaa yaje binafsi,sasa mchezo mchafu yeye kataka kuucheza kwa usafi na anazidi

kuharibu eti anasubiri serikali ambayo aliwahi kuiambia kuwa watu wanataka kumuuwa na haikufanya chochote badala yake wanamuua sasa na anaiamini..
anategemea wamuonee huruma gani sijui,wakati sumu ashalishwa...,shujaa wa ukweli hutoa wosia muhimu zaidi wakati anakata roho
likini wababaishaji hawawezi kwani mambo ambayo wamekuwa wakifanya hayakuwa na nia njema kama ilvyokuwa machoni pawengi.
 
ripoti ya ugonjwa unaomsumbua naibu waziri wa ujenzi, dk. Harrison mwakyembe, imeendelea kuivuruga serikali, safari hii wizara ya mambo ya ndani ikisisitiza kuwa wizara ya afya ndiyo inayopaswa kuzungumzia suala hilo.

Kauli hii mpya toka wizara ya mambo ya ndani imekuja ikiwa ni takriban wiki moja tangu gazeti hili lilipomuuliza katibu mkuu wa wizara ya afya na ustawi wa jamii, blandina nyoni, kuhusiana na ripoti hiyo na kusema kuwa suala hilo haliwahusu. Uamuzi wa tanzania daima jumatano kutaka kupata kauli toka wizara ya mambo ya ndani ambayo kimantiki inashughulikia madai ya jinai ulikuja baada ya kile kinachodaiwa kuwa ripoti ya ugonjwa wa waziri huyo kutoka kwa madaktari bingwa wa hospitali maarufu ya apollo nchini india ambayo hadi sasa imebaki kuwa siri, inadaiwa kueleza chanzo cha ugonjwa wa dk. Mwakyembe kuwa umetokana na sumu kali aliyowekewa hapa nchini.

Gazeti hili jana lilimtafuta waziri wa mambo ya ndani, shamsi vuai nahodha, kutaka kupata kauli yake juu ya ripoti hiyo na tuhuma zinazotajwa ambapo alisema mwenye uwezo wa kuzungumzia juu ya ripoti hiyo ni mkemia mkuu wa serikali toka wizara ya afya. Alipoulizwa na gazeti hili anazungumziaje juu ya kile kinachodaiwa dk. Mwakyembe kuwekewa sumu hapa nchini, waziri nahodha alijibu kwa sauti kali kidogo: “aa..ah, sikiliza; wenye uwezo huo nimekwambia ni wizara ya afya, mimi kama waziri wa mambo ya ndani kuzungumzia suala hilo ni mpaka niletewe taarifa kama mtu anatuhumiwa kwa sababu wizara yangu inashughulika na kesi za jinai.

“sasa sijaletewa taarifa, mimi ripoti siijui, ripoti za afya za watu ziko wizara ya afya... Hao si ndiyo wanawapeleka watu india?...sijaletewa ripoti sijaiona na sidhani kama nitalewa,” alisema. Alipoulizwa kwa nini anasema hadhani kama ataletewa ripoti hiyo je hakuna taarifa zinazodai kuwa ugonjwa unaomsumbua dk. Mwakyembe unatokana na sumu? Bado aliendelea kusisitiza kuwa hajapokea taarifa zozote za mtu kutuhumiwa kumuwekea sumu dk. Mwakyembe na kusisitiza kuwa kama gazeti hili linamfahamu mtuhumiwa huyo basi limtajie. Hata hivyo ingawa taarifa rasmi ya serikali haijatolewa, ripoti ya ugonjwa wa waziri huyo kutoka kwa madaktari bingwa wa hospitali maarufu ya apollo nchini india ambayo hadi sasa imebaki kuwa siri inadaiwa kupelekwa serikalini kupitia wizara ya afya.

Taarifa za dk. Mwakyembe kuwekewa sumu, mara ya kwanza ziliibuliwa rasmi nchini na waziri wa ushirikiano wa afrika mashariki, samuel sitta, ambaye ni rafiki mkubwa na mshirika wa karibu wa dk. Mwakyembe katika mapambano dhidi ya ufisadi nchini katika mahojiano na kituo cha televisheni cha itv katika kipindi chake cha dakika 45 kilichorushwa mwaka jana. Sitta alisikika akisema kuwa wasiwasi huo wa dk. Mwakyembe kuwekewa sumu unatokana na mabadiliko ya ngozi na nywele alivyoondoka navyo nchini kwenda india.

Kwa mujibu wa sitta ambaye ni mbunge wa urambo mashariki (ccm), alisema alipokwenda kumwona dk. Mwakyembe nyumbani kwake, alipata mshtuko mkubwa kwani ilikuwa ni mara yake ya kwanza katika umri alionao kushuhudia ngozi ya mtu ikitoa unga. Sitta alikaririwa akisema, “kuna kitu kama mba kwenye nywele na kwenye ngozi ya dk. Mwakyembe. Akishika hivi, baadhi ya nywele zinadondoka. Mkono umevimba, sehemu mbalimbali. Mke wake alichukua video. Alikuwa anatuonyesha kwenye laptop (kompyuta ndogo). Kwa kweli inatisha.” hata hivyo, sitta alihojiwa na polisi kuhusiana na taarifa hiyo kwa madai kuwa ingeweza kuhatarisha amani, lakini alipotakiwa kutoa ushahidi anadaiwa kutoa ushahidi wa habari za kwenye mitandao ya kijamii.

Kabla ya dk. Mwakyembe kwenda india kutibiwa, kulikuwa na uvumi kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa kiongozi huyo kulishwa sumu, ingawa yeye binafsi hajakanusha wala kuthibitisha habari hizo. Katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu aliporejea nchini, dk. Mwakyembe alisema ripoti ya ugonjwa wake iko serikalini. Hata hivyo, serikali hadi sasa imekataa kuitoa hadharani ripoti hiyo ya madaktari bingwa wa hospitali ya apollo, india, waliomtibu dk. Mwakyembe. Habari zaidi zinasema kuwa mwanasiasa huyo amepania kuianika ripoti hiyo hadharani kama serikali itaendelea kuifanya kuwa siri.

Dk. Mwakyembe alipelekwa india oktoba 9 mwaka jana na kurejea nchini desemba 11 mwaka jana hata hivyo licha ya kupata matibabu nchini india na kuendelea na tiba hiyo hapa nchini, hali yake bado siyo ya kuridhisha kwani amenyonyoka nywele, kope, nyuzi na hata vinyweleo vyote mwilini.


source: Tanzania daima 11/01/2012

kitendo cha maafisa wa serikali kupishana kauli kinazidi kuongezeka kasi siku baada ya siku. Wapembuzi wa mambo ya kijamii wanajua maana halisi ya watu kupishana kauli na sababu ya hizo sintofahamu. Kama asili ya ugonjwa wa dk ni sumu??nini kifanyike ili kubaini maharamia waliomdhuru dk mwakyembe??je ni watetezi wangapi wa rasilimali ya taifa hili watadhurika kwa utaratibu huu??wapo wapi wale wanaintellejensia wetu mahiri wa kuzuia maandamano ya chadema, wapo wapi wale majemedari wa kusafirisha kwa ndege za kivita viongozi wa chadema kuwapeleka mahakamani kuhudhuria kesi???mbona hatuwaoni kazini, mmegoma kufanya kazi au bado mnasubiri maelekezo kama kawaida yenu?? Hivi ni kweli mpo kwa ajili ya usalama wa raia wema au mnatumia huo kama msemo kujustify malipo ya mishahara yenu kupitia kodi za wananchi masikini????inauma saaaana. I strongly believe kwamba ipo siku mateso haya yatakuwa historia!!!!suala la siku hiyo ni lini naomba nawaachie wananchi waamue wao siku watayoona inafaa kuachana na haya mateso ya kujitakia! Hivi kweli tanzania imafika mahali hapa???nini chanzo!!!

mungu akupe nguvu dk. Mwakyembe, wananchi wengi sana wapo nyuma yako wakikuombea upone maradhi yanayokusumbua. Kwa kuwa repoti ya tatizo lililokupata ni haki yako, wananchi wengi sana wangeshukuru kama ungewajulisha kilichojiri ili tuweze kuchukua tahadhari stahiki.

si aseme mwenyewe basi...suala litageuka worship, we dont need this blabla
 
Yapata mwezi toka arejee kwenye matibabu nchini India, wakati akiwa India yeye pamoja na viongozi wengine waliokua wakitibiwa tuliweza kupata taarifa za maendeleo ya afya zao lakini toka dr mwakyembe arejee kimya kimekua kingi sio wizara ya afya ambao wameweza kuzungumzia afya ya kiongozi huyu na hata pia ofic ya bunge na yenyewe haijazungumza kitu chochote, tunasikia hali yake sio nzuri ila wana jf hii hali ya ukimya wa serikali kuhusu afya ya kiongozi ambae ni sehemu ya serikali inaashiria nini au ndio rumours kwamba kuna watu wanausika na masaibu ya kiongozi huyu aliesimama kidete kwenye scandal ya richmond, tafakari!
 
Mhhh hali anayoendelea nayo DR Mwakyembe kwa sasa yeye mwenyewe ana sehemu ya kulaumiwa juu ya hili. Kwa nini nasema hivyo??? Toka alivyoanza kuugua hadi ikapelekea kwenda India and finaly akarejeshwa, bado kila anapoulizwa chanzo cha hali hiyo amekuwa mgumu kueleza umma nini hasa kilichomsibu. Mi nafikiri kama ni woga wa "SYSTEM" Kumshughulikia pamoja na kukataa kwake kuueleaza umma nini kilichotokea, bado hali ni hiyo. Mi nafikiri huu ni wakati muafaka saana kwa yeye kuja mbele ya jamii na kutueleza hasa nini anachosumbuliwa, vinginevyo Binafsi yangu naanza kuhisi kuwa chanzo cha maradhi yake mwenyewe anakijua!!
 
Hii Habari imenifanya nimuamini sana JB,Buriani Mwakyembe Kama kweli unapenda wanachi wenzio na nchi yako kwa kinywa chako tuambie hao wabaya wako utaokoa wengi waliokwenye listi ya kuteswa na kisha kuuliwa kama wewe tunkuombea amani tele katika njia ya kutangulia ambako sote tutakufuata au tutakutangulia kwenda

Re: Dk. Mwakyembe mambo mazito: Ripoti ya ugonjwa wake yaivuruga Serikali
Haya irudieni na muone waliohusika na njama chafu hizo!

RIPOTI YA UCHUNGUZI BINAFSI JUU YA UGONJWA WA DR HARISON MWAKYEMBE 12/10/ 2011


JASON BOURNE
TEL:*********
ID************

Hatua ya kwanza:
Niliamua kujua kama ni kweli kalishwa sumu. Na watu nilio wahusisha katika kujua huko ni TISS.

Katika uchunguzi niliweza kuzungumza na LTK wapatao kumi na tano.

Maboharia wawili

Wapanga mikakati wawili

Mkuu wa LTK

Vijana wa kazi kumi

Wote maelezo yao yalifanana kwa maana ya (walishiriki kupanga na kutekeleza kumlisha sumu Dr Harison Mwakyembe)

Hatua walizopitia:

Kwa mujibu wa maelezo ya LTK/D00/B1 mkuu wa kitengo hicho ambae kwa kweli niliongea nae kama rafiki yangu wa karibu ndie aliyenipa mwangaza wakufanikisha kazi yangu.

Katika misheni hii watu wengi wanatakiwa KUFA, nitawataja wale muhimu tu:
1. Wilblod Slaa
2. Samweli Sitta
3. Harison Mwakyembe
4. Said Kubenea
5. Mark Mwandosya

Mnamo ijumaa ya tarehe 01/10/2010 saa 4:25, kikao kikuu cha mikakati kilikalika Moven Pick kikihudhuriwa na watu sita,


TISS/A001

TISS/B1

TISSB32

TISS/B5

TISS/A6

TISS/F5


Baada ya mjadala wa saa moja uliogusa magumu inayokumbana serikali na watu walio waona wao ni vikwazo na waliosababisha magumu hayo, ndipo wakaibuka na listi ya wanaotakiwa kusalimisha uhai wao:

Bada ya hapo kesho yake TISS/B1 alikutana na LTK/D00/B1 na kumpa amri ya misheni hiyo na orodha kamili ya watuhumiwa bila kuwa ambia sababu za mauaji hayo, zaidi alisema nahitaji ripoti ya utekelezaji.



Baada ya amri kuwa chini ya LTK, mikakati ya aina ya kifo kwa kila mtuhumiwa ilipangwa ambapo walipamgwa katika makundi matatu,

1 Samweli Sitta
2 Harison Mwakyembe
3 Mark Mwandosya
Hawa wamepangiwa vifo vya aina mbili kwanza ajali na ikishindikana watalishwa sumu.

1 Said Kubenea

Kumwagiwa tindikali, baada ya kufeli ile ya kwanza imeagizwa nyingine toka Bulgaria yenye kuua baada ya masaa kumi na mbili tu!

1.Wilblod Slaa

Huyu anatakiwa kufa kwa shabaha ya risasi (snipers) ndio wanao andaliwa tu kwa sasa.

Waliopewa kipaumbele kufa ni Samweli Sita, Mark Mwandosya na Harison Mwakyembe ambapo LTK/D00/B10, LTK/D00/B14, LTK/D00/B17 na LTK/D00/B21 walipewa kazi hiyo.

Kikwazo kikuu walichokumbana nacho vijana wa kazi, ni kuwa, Sita, Mwandosya na Mwakyembe wote ni majasusi na kwapamoja walifanikiwa kufumbua njama hizo chafu za mauaji kwa siri.

Mitego ya ajari 16 kwa Mwakyembe yote imemkosa, 12 kwa Sita nayo ikamkosa,7 kwa Mwandosya nae kakoswa.

Walipoona mbinu zote za vifo vya ajali zimefeli wakahamia kwenye aina ya pili ya vifo vya kulishwa sumu:


Katika aina hii ya mauaji kwa muujibu wa vijana wa kazi wanashangaa uimara wa Samweli Sita na Mwakyembe kwani wameshalishwa aina nyingi za sumu lakini bado wanadunda tu, kwanza sumu ya kwanza kuwalisha ni katika kikao cha kwanza cha bunge mwa 2011, hawakupata madhara yoyote.


Wakabadilishiwa aina ya sumu, hakika hii ilimpata zaidi Mwandosya kwani ilipandikizwa katka simu yake ya mkononi bila yeye kujua saa 4:40 asubuhi ofisini kwake tarehe 7/3/2011.

Aina hii ya sumu (jina sikupata kujua lakini hapa huitwa LTK/XXX) nayo ilishindwa kuzaa matunda kwa Mwakyembe na Sita licha ya kupewa katika mazingira tofauti,hii ilitokana na kuwa kidogo.



Zoezi hili zito na la hatari baada ya kuwa gumu kupita kiwango kwakuwa hata Mwandosya hakudhurika sana, ilibidi uhitajike msaada toka nje ya nchi na ndipo jasusi mashuhuri wa kitanzania Exaveri H.Limo akaenda Urusi kutafuta aina nyingine ya sumu kali.

Tarehe 11/7/2011 akafanikiwa kukutana na Zudrav Ghev mmoja wa wakemia wa KGB katka kituo cha Moscow akapata Polonium 236, kutokana na unyeti na hatari ya sumu hiyo ilimlazimu bwana Zudrav Ghev kuchukua ndege ya watu wa tano na kuruka mpaka tz .

Baada ya kufika tz bwana Zudrav alitoa mafunzo ya wiki moja jinzi ya kuhifadhi na kutumia kisha akatokomea kurudi kwao na vijana wake wanne.


Baada ya Mrusi kuondoka misheni zikaendelea na mnamo tarehe 24 /7/ 2011 wakati afya ya Mwandosya ikiendelea kuzorota mmoja wa LTK/D00/B10 wa kike alifanikiwa kumuwekea Polonium 236 katika chai nyumbani kwake akiwa ni miongoni mwa watu waliokwenda kumjulia hali,

Na Mwakyembe alikuja kuwekewa ktk maji ya kunywa na kwenye kitambaa cha kufutia uso LTK/D00/B17 siku ya uzinduzi wa kikao cha Makandarasi,Wahandisi na Wakadiriaji majenzi pale Mlimani City kilichohudhuriwa na rais.

Kuonyesha kuwa Mwakyembe ni jasusi aliye kubuhu siku hiyo maji hakuyanywa wala kugusa kabisa lakini mungu si athumani kitambaa akakitumia, jambo la kushangaza nikuwa baada ya kama dakika 20 kukitumia kile kitambaa alikitupa wakati anatoka eneo la Mlimani City.

Hivi sasa LTK wameshamaliza kazi yao kwa watu wawili na anayefuata ni Samweli Sita
Na uwezekano wa kupona kwa India ni mdogo ila wanaweza kupunguza makali na kusogeza mbele mauti yao hiyo ni kwa mujibu wa mkuu wa LTK.

Slaa maandalizi yake yanaangalia zaidi uchaguzi ujao ingawa kumeingia aina ya mabishano makali juu ya kumuua hasa wakihofia kutokea kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe kwakuwa jamii ya kitanzania na kimatafa inamtambua.


Said Kubenea amekabidhiwa LTK/D00/B21 ambae anasubiri kitendea kazi toka Bulgaria ambapo jasusi Yugrov Dittzov ndie atakae ileta.


Huu ndio uchunguzi wangu binafsi baada ya kupata taarifa juu ya hali ya Dr Harison Mwakyembe kuwa ni tete.

Nasema kuwa serikali ya Tanzania inafanya mauaji ya rai wake hasa viongozi wenye mtazamo tofauti na serikali.

Naiomba serikali ya Mh rais isikilize kilio cha watanzania isisikilize kilio cha mafisadi.

Nina waomba watanzania tuungane pamoja bila kujali dini zetu,makabila yetu wala rangi zetu kulikataa kundi hili la wahalifu lililo jichimbia ikulu huku likitengeneza mazingira ya kuweka watu wao likimaliza mda wao wa uongozi kwa maslahi binafsi


Huu ni uchunguzi wangu, unahaki ya kusubiri uchungu wa madaktari wa India

ASANTENI SANA:
JASON BOURNE
 
Back
Top Bottom