Dkt. Mwakyembe mambo mazito: Ripoti ya ugonjwa wake yaivuruga Serikali

Mwakyembe keshajifia, kosa kubwa atakalofanya ni kutotoa ripoti hadharani kama alivyoficha baadhi ya mambo ya Richmond ambayo hata leo akiyatoa hakuna atakayeyaamini kwa asilimia mia. Aseme kitu gani kinamsumbua, anahusika, na kwanini kafanyiwa hivyo. La sivyo tutaishia kuwa na story za akina Balali tu.
Msije mkatusingizia watu wa monduli.
 
Oooohhh Tanzania yetu, Pole sana Dr Mwakyembe. Naombeni sana viongozi wetu wa CHADEMA muwe makini kila mnapoennda na kila sehemu mnazokula hawa maccm si watu kabisa
 
This is very sad, imagine mtu alikuwa na malengo yake kibao, ghafla maisha yake yanakatishwa ivi ivi!! kwakweli hii inchi inasikitisha sana hapa tulipofikia. I never expected to see this happening in my country.
 
Tanzania uongozi hamna,nchi za wenzetu swala kama hili mchawi anatafutwa haraka na kuwajibishwa.Hivi ni nchi gani

mnayoijua nyie ambapo rais wa nchi asingeingilia issue kama hii hata kama siyo kazi yake..yeye ni suprime leader na itamjengea

credibility kwa kuingilia,lakini hapa kwetu tuna bahati mbaya ya kutotambua watu wa kuweka madarakani.

KUHUSU Mwakyembe;huyu jamaa siyo shujaa kama watu wanavyoweza kuaminishwa kwa kupambana kwake na ufisadi,ni mtu

mwoga sana na hana ujasiri wowote, yeye alitaka umaarufu tuu hakujua kama watu aliokuwa akidili nao ni hatari ndiyo maana

hathubutu hata kusema kama aliwekewa sumu anajiamisha kuwa watakuja kummalizia wakati ameshakwisha.
 
Hakika hizi habari zinasikitisha,zinaudhi na zinaumiza mioyoya Watu wengi.

Mimi natoa ushauri kwa Dr. Mwakyembe kama ifuatavyo. Kamakweli wamempa sumu na Madaktari wa Appolo wamethibitisha hilo na taaarifazimetumwa Serikalini kupitia sijui Wizara ya Afya ,Mmabo ya Ndani etc. Yeye Dr.Mwakyembe personal AJITOKEZE HADHARANI AONGEE NA UMMA WA WATANZANIA kupitiavyombo vya habari ili aweke mambo hadharani. Hakuna haja ya kuficha hili jambokwani ni hatari sana kwa Watanzania wote bila kujali itikadi zao za vyama au dini.

Mwakyembe atoboe ukweli hata kama watasema amehatarishausalama wa Nchi. Tayari uslama wa Nchi umesha hatarishwa na hao WALIOMPA SUMUILI KUMUUA! Dr. Mwakyembe ajue kuwa tayari hawa jamaa walishakuwa na mpango wakumnyamazisha kwa sumu(poison killing).

Kama ni bahati yake kuwa madaktari wa Appolo wameweza kuokoa maisha yake ajue tu kuwa BADO WABAYA WAKE WANAMWINDA ILI WAMMALIZE UPESI KABLA HAJAWEKA MAMBO HADHARANI. Ni wakti wake wa kuwaweka WAZI HAWA WAUAJI KABLA HAWAJAMMALIZA KABISA ILI WATANZANIA WAJUE TUNA SERIKALI YA WATU WA AINA GANI.

Huu ni unyama ambao hauwezi kuruhusiwa uendelee kutamalakikwenye nchi hii iliyo asisiwa na wapenda AMANI kina Marehemu Baba wa Taifa Mwl.J.K.Nyerere. Hatutaki kuona mtu anaingia IKULU KWA KUMWAGA DAMU AU KUTOA UHAI WA MTU KWA KUTUMIA SUMU. Hatutaki,nasema hatutaaaaaaaaaaaaaaki!!!
 
Nyie Watanzania mbona mna kuwa wapelelezi kama Bibi Kiroboto??

Afya ya mtu mnaitakia nini?? Yeye anaumwa mnaona anaumwa. bado mwataka kujua anaumwa nini? Kama ni kila mgonjwa maradhi yake yawekwe bayana nashauri lianzishwe Gazeti la Kila siku liuzwe mitaani na jina liwe WATANZANIA NA MAGONJWA YAO.liwe linatoka daily. Na sheria ipitishwe pia..

Mwakiembe anaumwa.Full Stop..Maradhi gani ?? najua mkewe na aliyepokea result za maradhi yake..Alilishwa Sumu ok...Why na where???? God knows.

Tanzania ni njema atakaye na aje.
 
huyu bwana hawezi tena...hawezi kusema lolote juu ya hali yake na chanzo cha ugonjwa wake....hili gazeti linasema ataianika report hiyo hadhari kama serikali itaendelea kuificha....mi nasema hataweza na yeye anajua kuwa hawezi kuanika...labda mtu mwingine aiiibe ile kopy na kuipeleka kwenye vyombo vya habari ..lakini sio yeye

hali yake kwa sasa sio nzuri hata kidogo...kucha zinatoka, nyayo za miguuni zinapasuka pasuka, hana vinyweleo mwilin, hana nywele kichwan hata nyusi hana....ngozi ya uso wake inapauka sana na ni nyepesi sana japo inapakwa mafuta mengi yanayomfanya anang'ae lakini bado.....mikononi anavaa gloves ndefu na miguuni anavaa naweza kusema nazo ni gloves maana s viatu vile.....
japo uso wake una tabasamu na anaongea tena vizuri sana lakini bado anaumwa...ukiangalia cd ya namna alivyokuwa anapata tiba kule india...huwezi kujua kama ni yeye....anyway basi tu

hivi mnajua kwa nini amerudishwa nchini wakati hali yake bado?

Mkuu tujuze tu kulikoni karudishwa mapema?maana anaonekana dhahiri yu mgonjwa sana! kuhusu report angeisoma tu maana apparently hachomoki! na mtu hafi mara mbili
 
Hakika nawaambia ya kwamba hawa chichiem wana group inayotenda kazi hii kama walivyofanya kwa hawa,,,,,,,,,,,,,,,,lakini siku zitakuja ambao kamwe hawataweza kutenda lolote tena kamwe


Na Mi nafikiri hata wangekuwa na uwezo yani kuna baadhi ya maeneo huyu mukere wao asingeruhusu hata mwanga kuwepio na angetamani pawe giza siku zote atakazo yeye.

Hakika ya Dr Mwakyembe yatajulikana tu!!!!!!!!!!!!!!!!
 
mi sijui wanaogopa nini kusema wazi kuwa alilishwa sumu alhali kila m2 anajua hilo!?

Kila mtu anajua? Mbona mimi sijui? Ingekuwa ni kweli kwa jinsi ninavyomfaham asingekaa kimya, anaugua ugonjwa wa kawaida ila wanautumia for political motives!
 
Nyie Watanzania mbona mna kuwa wapelelezi kama Bibi Kiroboto??

Afya ya mtu mnaitakia nini?? Yeye anaumwa mnaona anaumwa. bado mwataka kujua anaumwa nini? Kama ni kila mgonjwa maradhi yake yawekwe bayana nashauri lianzishwe Gazeti la Kila siku liuzwe mitaani na jina liwe WATANZANIA NA MAGONJWA YAO.liwe linatoka daily. Na sheria ipitishwe pia..

Mwakiembe anaumwa.Full Stop..Maradhi gani ?? najua mkewe na aliyepokea result za maradhi yake..Alilishwa Sumu ok...Why na where???? God knows.




Tanzania ni njema atakaye na aje.

Hapo kwenye red,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,kakae na mukwere mpitishe

Mtumwa mkubwa wewe!
 
Siku pale haki itakapochukua mkondo wake.

Very true mkuu,imefika muda wa watanzania kila kitu kuchukulia kama ni ngonjera au maigizo tu kwamba yakipita basi,imefika wakati sasa wa issue serious na hatari kwa taifa letu tujue vyanzo vyake na mpaka hatima yake,sio kila kitu kuchukulia poa kama watu waliojikatia tamaha kabisa na kuwaacha wachache wafanye watakavyo kwa nchi hii
 
Jason bourne!!!!!!!!!!! Uko wapi Kamanda wetu???????????????????????
:focus::focus:
Mkuu!!! Hebu anguka kwa huku kidogo tu.
 
lisu huwa anamsemo wake unaoesema
"haki itashinda"
Naminasema amen. Yani naiwe kama ilivyotakiwa iwe.
 
Kimya kingi kina mshindo mkuu ingawa nadhani sasa it is too much!
 
Kuna mwanasayansi mmoja hapa JF aliichambua hali ya Dk. Mwakyembe aliyokuwa nayo kabla ya kwenda India.......nafikiri ule uchambuz haijawa disputed hadi leo...........

Wote kwa pamoja tukasome "Exfoliative dermatitis" kisha turejee hapa kwa discussion.mkumbuke kuangalia causative factors,symptoms na prognosis.
 
Kama kawaida hili sakata la sumu liliibuliwa humu na kupewa uzito na JB lakini kama kawaida ya magazeti yetu kwa makusudi wanasema eti Sitta ndio aliibua kwa mara ya kwanza! Wakati hata huyo Sitta alipeleka polisi ushahidi wa maelezo ya JB! Kwanini magazeti yanakataa kuipja credit JF? Au ndio lile bifu la magazeti kudoda maana wasoma magazeti wakubwa wameacha kununua sababu kila kitu kinapatikana hapa!

tofautisha kusema na kuandika. Sitta ni kiongozi, na anachosema kina athari kwa jamii. Sitta hakusoma jf ndio akaenda kusema bali alienda kwa mwakyembe na kuzungumza na familia yake na kuona hali halisi. Jason aliandika humu, na ujue habari za mtandao hata kama ni za kweli, sio rasmi
 
Back
Top Bottom