Jinsi ya kupika chapati laini na zenye ladha nzuri

Asante.sasa hizo chapati za nazi zinakuwaje?una maanisha unakandia nazi badala ya maji?
Ndiyo maana yake, hakikisha unapata tuwi zito ndo ukandae unga wa chapati, ili kupata tui zito baada ya kukuna nazi yako ibrendi na maji kidogo katika brenda kwa muda mrefu, kisha kanda unga na chumvi, usikawie papo hapo sukuma chapati na uchome.

Kumbuka chapati iive vizuri mpaka ndani lakini kamwe isiunguwe wala kuonyesha arama yeyote nyeusi. kama utahitaji kula baadaye kidogo zihifadhi katika hotpot.
 
Ndiyo maana yake, hakikisha unapata tuwi zito ndo ukandae unga wa chapati, ili kupata tui zito baada ya kukuna nazi yako ibrendi na maji kidogo katika brenda kwa muda mrefu, kisha kanda unga na chumvi, usikawie papo hapo sukuma chapati na uchome. Kumbuka chapati iive vizuri mpaka ndani lakini kamwe isiunguwe wala kuonyesha arama yeyote nyeusi. kama utahitaji kula baadaye kidogo zihifadhi katika hotpot.
Nitafanya practical soon.Ubarikiwe
 
Chef mkuu, mimi huweka mafuta ya moto sana kwenye unga wenye chumvi. Lakini nahakikisha nimechekecha unga (to add in air) kabla ya kuutumia. Then nachanganya unga na mafuta kwa kutumia vidole tu (inaitwa rub in, to add more air). Nakanda na maji ya uvuguvugu kiasi.

Nikishasukuma mara ya kwanza na kupaka mafuta kidogo, navuta kwa vidole gently kila upande napata mdabwada wenye unene mdogo sana, kisha nakamata kona moja na kukunja kamba (hapa napata layers nyiingi nyembamba kwenye chapati zangu).

Naziacha kama muda wa nusu saa hivi, kisha nasukuma miduara.
ili zisinyonye mafuta mengi, nakausha pande zote kikaangioni, then naweka mafuta kidogo ( nusu ya tea spoon) juu then naipindua. Inakuwa na rangi nzuri sana, laini na inasasambuka haswaa!
 
Chef mkuu, mimi huweka mafuta ya moto sana kwenye unga wenye chumvi. Lakini nahakikisha nimechekecha unga (to add in air) kabla ya kuutumia. Then nachanganya unga na mafuta kwa kutumia vidole tu (inaitwa rub in, to add more air). Nakanda na maji ya uvuguvugu kiasi. Nikishasukuma mara ya kwanza na kupaka mafuta kidogo, navuta kwa vidole gently kila upande napata mdabwada wenye unene mdogo sana, kisha nakamata kona moja na kukunja kamba (hapa napata layers nyiingi nyembamba kwenye chapati zangu). Naziacha kama muda wa nusu saa hivi, kisha nasukuma miduara.
ili zisinyonye mafuta mengi, nakausha pande zote kikaangioni, then naweka mafuta kidogo ( nusu ya tea spoon) juu then naipindua. Inakuwa na rangi nzuri sana, laini na inasasambuka haswaa!
Nimependa upishi wako na inaelekea chapati zako huwa zinakuwa laini na tamu.Sasa niambie hapo kwenye air naona ni pageni kwangu.Faida za air kwenye chapati ni nini na kisayansi inakuwaje???
 
X-PASTER asante sana for this recipe
nilikuwa sijawahi pika chapati
nimetumia maelekezo yako na chapati zangu za kwanza watu wamezipenda kweli.

once again thanks
 
Last edited by a moderator:
Chef mkuu, mimi huweka mafuta ya moto sana kwenye unga wenye chumvi. Lakini nahakikisha nimechekecha unga (to add in air) kabla ya kuutumia. Then nachanganya unga na mafuta kwa kutumia vidole tu (inaitwa rub in, to add more air). Nakanda na maji ya uvuguvugu kiasi. Nikishasukuma mara ya kwanza na kupaka mafuta kidogo, navuta kwa vidole gently kila upande napata mdabwada wenye unene mdogo sana, kisha nakamata kona moja na kukunja kamba (hapa napata layers nyiingi nyembamba kwenye chapati zangu). Naziacha kama muda wa nusu saa hivi, kisha nasukuma miduara.
ili zisinyonye mafuta mengi, nakausha pande zote kikaangioni, then naweka mafuta kidogo ( nusu ya tea spoon) juu then naipindua. Inakuwa na rangi nzuri sana, laini na inasasambuka haswaa!

Wifi kuna namna nyingine nilijifunza kupaka mafuta na kusokota kama ukiona kazi sana kufanya moja moja. Unakata donge kubwa kama la chapati 5-10 alafu unalisukuma mpaka liwe lembamba. Ukishapata wembamba unaotaka unapaka mafuta, unasokota kama kawaida alafu unakata vipingili pingili kwa kisu. Sinakua kama umesokota moja moja, kinachobaki kusukuma tu wakati wa kukaanga.

Natamani ningeweka picha ili na wengine wafaidi (haswa wale wasiojua/wanaokwepa kusokota kisa uvivu) sema hichi kimeo changu kinaleta pozz.
 
Nimependa upishi wako na inaelekea chapati zako huwa zinakuwa laini na tamu.Sasa niambie hapo kwenye air naona ni pageni kwangu.Faida za air kwenye chapati ni nini na kisayansi inakuwaje???

Kumbuka chapati haiwekwi hamira kama maandazi. Hewa ndio inayoumua na kufanya ngano isigandamane. Na haswa nia ya kusukuma mara mbili ni introduction ya hewa zaidi. Vitu vitatu muhimu vinaongeza hewa: kuchekecha unga, kukanda, na ile kusukuma mara mbili.
 
Aaah, wifi nimekuaminia. This weekend lazma nifanye hii yako. Ila sasa ukishapaka mafuta, kata mistari, then please vuta mdabwada ndo ukunje uone layers zitakavyotoka nyembamba.
Asante kwa kunijuza, faida kweli kuoa vichwa hehehe!
Wifi kuna namna nyingine nilijifunza kupaka mafuta na kusokota kama ukiona kazi sana kufanya moja moja. Unakata donge kubwa kama la chapati 5-10 alafu unalisukuma mpaka liwe lembamba. Ukishapata wembamba unaotaka unapaka mafuta, unasokota kama kawaida alafu unakata vipingili pingili kwa kisu. Sinakua kama umesokota moja moja, kinachobaki kusukuma tu wakati wa kukaanga.

Natamani ningeweka picha ili na wengine wafaidi (haswa wale wasiojua/wanaokwepa kusokota kisa uvivu) sema hichi kimeo changu kinaleta pozz.
 
Uchaga tu unakusumbua,lol!

Tatizo ni ukandaji kama alivyosema snowhite. Unatakiwa ukishachanganya maji na unga kiasi uanze kukanda from the edges towards the centre. Yaani unakamata donge pembeni unaleta kati, ukizungusha donge ili ukande pande zote.
Pili zingatia joto la maji. Inabidi yawe makali zaidi kidogo kuliko chakula cha mtoto. Namaanisha ukidondoshea nyuma ya kiwiko ustuke kidogo. Chapati za kumimina maji yanatakiwa ya baridi kabisa (mimi hutumia ya kwenye friji)
thanks kwa somo..
kitu gani kinafanya chapati kuwa ngumu?
 
Last edited by a moderator:
Aaah, wifi nimekuaminia. This weekend lazma nifanye hii yako. Ila sasa ukishapaka mafuta, kata mistari, then please vuta mdabwada ndo ukunje uone layers zitakavyotoka nyembamba.
Asante kwa kunijuza, faida kweli kuoa vichwa hehehe!

Naomba nikutembelee week end uwe mwl.wangu
 
Nazipenda kweli chapati...Nafurahi pia kujua kuzitengeneza, wiki haipiti bila kuzipika!! huh
 
Habari jf chefs,ninatatzo moja kila nikipika chapati za kusukuma zinakua ngumu nawakati mwingne znakatikakatika nataman nipike chapati yani ukiiweka mdomoni ufurah mwenyewe.plz nsaidieni nimsuprize huyu shemej yenu weekend hii afu namwekea na rost la maini

=================================================

CHAPATI ZA VIAZI NA MAYAI

View attachment 333663

Kwanza, unahitaji viazi, mayai na vitunguu maji.
View attachment 333643
Pili, weka maji madogo katika bakuli moja kubwa, ondoa ngazi ya viaz na kuzikata ziwe chips, halafu unatakiwa kuviweka katika bakuli lenye maji.
View attachment 333644
Tatu, tia chumvi, unga wa bizari na unga wa pilipili, korogakoroga
View attachment 333645
Nne, tia mayai, korogakoroga
View attachment 333647
Tano, tia unga kwa kijiko tano(ukipenda unaweza tia unga nyingi zaidi, inategemea)
View attachment 333648
Sita, tia vitunguu maji, korogkoroga mpaka iwe kama uji(vitunguu maji ziwe vipende vidogovidogo)
View attachment 333651
Tia mafuta madogomadogo katika sufuria, moto iwe ndogo, weka uji kadhaa, baada ya dakika 2, geuza upande endelea kupika baada ya dakika 1, chakula kiko tayari.
View attachment 333652 View attachment 333653 View attachment 333654

Kuna njia tofauti za kukanda chapati zako zikawa laini, lakini siri kubwa ya kupata chapati nzuri ni kuukanda huo unga vizuri na ulainike.

Mahitaji basic:

1. Unga wa ngano
2. Chumvi
3. Sukari kidogo sana kwa ajili ya seasoning
4. Mafuta kidogo ya kukandia kulingana na unga wako, usijaze mafuta kibao
5. Maji - hapa inategemea na ukandanji wako mimi natumia maji ya baridi sana ikiwezekana nayaweka kwenye freeza kidogo yazidi kuwa baridii.

Mhitaji extraa:

Hapa ni kulingana na ufundi na uzoefu wako unaweza kuweka vitu vifuatavyo ukipenda lakini sio vyote waweza chagua kimoja

1. Tui la nazi (waweza kutumia kukandia unga badala ya maji
2. Maziwa - ukitaka kuongeza virutubisho kwenye mlo wako
3. Mayai - Na chapati inakuwa laini kama sufi, kwa sababu mayai hayafanyi chapati iwe ngumu kama ni hivyo basi hata keki zingekuwa ngumu kama jiwe.
4. Vitunguu maji - kwa ajili ya kuongeza ladha
5. Nyama ya kusaga au mboga mboga yoyote ile -kwa ajili ya kubadilisha aina za chapati sio kila siku ni chapati design ile ile tu.

Kwa basic Chapati -Stage 1:

1. Tia unga wako kwenye chombo au mashine yako ya kukandia.
2. Weka chumvi, na sukari kidogo kwa ajili ya seasoning
3. Tia mafuta kwenye unga (kwa mfano kwa unga kilo moja weka mafuta 1/4 kikombe)

4. Changanya vizuri mchanganyiko wako
5. Weka maji yako kwenye unga kidogo kidogo mpaka unga uchanganyike.
6. Unga ukishanyanganyika ukande mpaka ulainike.
7. Ukisha lainika weka kwenye friji kama nusu saa hivi, kama huna friji ufunike mahali pasipo na joto.

Stage 2:

1. Changanya unga wako vizuri kisha ukate madonge madogo madogo kiasi.
2. Chukua donge moja usukume kwenye kibao au juu ya meza iliyo safi.
3. Paka mafuta kidogo juu ya chapati yako uliyoisukuma, waweza kutumia samli au mafuta mazito kama samli.
4 Kunja chapati yako irudi katika umbo la donge tena. Hapa ndio key unaweza kufanya chapati yako ikawa ngumu au ikawa laini yenye layers.
5. Sukama tena donge lako ulilolikunja, anza na lile la kwanza.
6. Weka chapati yako kwenye chuma kikavu (frying pan) kilichopata moto, kisiwe cha baridi wala cha moto sana.
7. Ikiiva upande mmoja igeuze upande wa pili.
8. Ikishaiva pande zote weka mafuta kijiko kimoja tu kikubwa cha chakula kwenye chapati yako upande wa chini.
9. Ikunje hiyo chapati na uigeuze pande zote ipate mafuta, au waweza kuisuguasugua na kijiko chako kukahikisha upande zote zinapata mafuta na kuiva vizuri (inakuwa na rangi ya brownish)

10. Ondoa chapati yako kwenye chuma iko tayari kwa kuliwa.

Waweza kula peke yake, na chai, mchuzi wa aina yoyote ile au hata na maharagwe.

NB:
Waweza kukanda unga kwa kutumia mashine kama bread maker unachagua dough, kisha unaumonitor unga ukishakandika tu ndani ya 30 minutes unautoa ndani ya mashine na kuuweka kwenye friji kwa nusu saa. Au unaweza kukanda unga kwa kutumia mixer zile kubwa na unatoa dough maker.
Hii ni kwa wale wenye hizo mashine kama mimi. Kama huna mashine basi utaukanda unga wako kwa mikono hadi ulainike vizuri. Kulainika hapa sio kujaza maji, bali kutumia viganja vyako kuulainisha mpaka unga ukiupiga unavutika. Kisha unauacha uendelee kulainika kwa kuuweka kwenye friji.

ILANI: Mkishajaribu msinisifie mie maana hata mi nimeipata kwa KIJARUBA!

Vipimo.

Unga vikombe 4 vikubwa.
Maziwa vikombe 2 kasorobo.
Chumvi kiasi.
Baking powder 1 tea spoon
Hamira 1 tea spoon
Yai 1
Ufuta kiasi
Samli
Siagi vijiko 2 vya kulia

Namna ya kutaarisha

1)Changanya pamoja unga,maziwa,chumvi,siagi,hamira na baking powder..
2)fanya madonge kama 8 kwa kipimo hicho cha unga
3)sukuma kila donge na upake samli na ukunje kama chapati.
4)ukimaliza kukunja zote 8 then sukuma duara kiasi na uweke kwenye trey ya kuchomea kwenye oven...
5)subiria mpaka iumuke then pakaa yai kwa kutumia brush then nyunyuzia ufuta
6)washa oven moto kiasi hadi iwive
7)pakaa mafuta juu na tayar kwa kuliwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom