Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu
JF-Expert Member
- Mar 8, 2006
- 1,211
- 230
Nafikiri kilichomuudhi, Butiku, Mwinyi, Ulimwengu et al. ambao wamesimama upande wa dhati wa kumuenzi Mwl. JKN (RIP). Ni ile hali inayoendelea ya wanaoendesha serikali kama viongozi kuhubiri kumuenzi Mwl. Kinadharia lakini matendo yao yapo mbali sana na Mwl.Madilu, CCM watasema kuwa Butiku analalamikia kunyimwa ulaji, na yeye angekuwa kwenye mkao wa kula sijui kama angepiga kelele hivyo. Kuna baadhi ya watu wanadai kuwa yeye na Mkapa hawakuiva na Mkapa alimwonyesha mlango wa kutokea mapema Zaidi. Nasema CCM watasema hivyo kwa sababu wao huwa hawajibu hoja, wanawashambulia watoa hoja!