Kizaazaa Kibaha

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Ni kizaazaa.

Katika Barabara ya Morogoro sehemu ya Kongowe hadi Misugusugu. Kuna foleni ya ajabu sana. Inasababishwa na ukaguzi wa TRA kwa malosi eneo la Misugusugu.

Magari yanalazimika kupita barabara mbovu ya zamani. Basi la BM lililotoka Dar kwenda Moro saa 12 limekwama.

Nusura lipinduke kwa kuingia korongoni. Ni hatari.

Nipo hapahapa kuelekea nyumbani..
 
sio ukaguzi wa tra bali kuna mtu mmoja mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30-35 amegongwa na gari na kufariki papo hapo hali iliyopelekea wananch wa maeneo ya kongowe kuweka magogo kuzuia magari yasipite hadi mwili wa marehemu utakapoondolewa eneo la tukio.

Wanausalama walifanikiwa kuondoa maiti hiyo kilichofuatia ni kuondoa magogo.

Sijui kinachoendelea eneo la tukio kwani nimeshajimuvishisha eneo lingine.
 
Poleni kwa usumbufu huo wakuu. Sijui ajali zitaisha lini Tanzania au hata kupungua tu maana kumalizika si rahisi.
 
wanakagua zile sticker zao maana siku wakitumwa na wakubwa zao wakakusanye hela hawa tra,trafic police,tigo,fire utajuta barabarani kama gari yako mbovu
 
Poleni kwa usumbufu huo wakuu. Sijui ajali zitaisha lini Tanzania au hata kupungua tu maana kumalizika si rahisi.
Ajali zitaisha vipi wakati hakuna elimu ya Usalama Barabarani kwa watembea kwa miguu, waendesha baiskeli, mikokoteni, pikipiki, bajaj na madereva vimeo kibao! Watu wanafanya biashara ndogo barabarani.

Barabara zenyewe ni finyu, hakuna anayejali unatarajia nini? Serikali badala ya kuchukua hatua sitahiki inazidi kujaza matuta ktk barabara kuu,na kuondoa hata maana ya kujengwa barabara za lami.
 
Namshukuru Mungu nilifika salama. Kwa muda niliofika,sikuweza hata kuingia tena JF. Nilifikia kulala...
 
Back
Top Bottom