Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Kwa mujibu wa kamusi ya kiswahili neno Mapooza ni watu ambao wanasifu Kila kitu hata kama Cha kipuuzi(chawa).Hivyo,alimaanisha chawa hawatakuja wapya zaidi ya Hawa wa sasa ambao watz wamewapuuza.
 
Umeangalia matokeo? GT anaangalia chanzo. Lakini Je, unao uthubutu wa kumsema dada katika imani? Huyo ndio tatizo kwa sababu Gwajima alishamvua nguo nje ndani, uwezo wake ulishamvua nguo mapewa, na hafai kweli. Ajabu dada yako kamteua.

Sasa hapo tatizo la akili ndogo ni nani? Makonda asingeweza kukataa uteuzi hata kama anajijua ni chenga
 
Kuna mijitu imezaliwa ili iwe michawa kwa wenzao,sijui hata wazazi wao wanajisikiaje kuwa na toto kama hilo!
 
Umeangalia matokeo? GT anaangalia chanzo. Lakini Je, unao uthubutu wa kumsema dada katika imani? Huyo ndio tatizo kwa sababu Gwajima alishamvua nguo nje ndani, na hafai kweli, ajabu dada yako kamteua.

Sasa hapo tatizo la akili ndogo ni nani? Makonda asingeweza kukataa uteuzi hata kama anajijua ni chenga
Hapo alifeli,amefeli,na akiendelea nae atazidi kufeli Hilo halina ubishi,Liko wazi,may be aliona ampe second chance but habebeki...
 
kazi kazi tu..
viva comrade Makonda viva 💪
Ndugu zangu Watanzania,

Kama kawaida ya Mwamba Mwenyewe Paul Christian Makonda ni mtu wa kuteka hadhira, ni mtu wa kuteka mijadala, ni mtu wa kuondoka na point tatu na magoli ya kutosha,ni mtu anayeijuwa siasa,ni mtu msema kweli, jasiri,imara, hodari, madhubuti, shupavu na mwenye misimamo yake na ya aina yake.

popote alipo ni lazima pafahamike na kuvuma kama upepo wa baharini, ni Mwamba kwelikweli, ni field Marshall ambaye akianza kuzungumza unaona hata sisiminzi wanatulia kusubiri amalize kuzungumza ndio waendelee na shughuli zao.kiukweli huyu Mwamba ni jasiri sijapata kuona. Ni jasiri mpaka shetani mwenyewe anamuogopa.

Leo katika kutoa kwake neno amemmwagia sifa kemkemu Askofu mkuu mstaafu wa jimbo kuu la Dar es salaam Kardinali Pengo kwa kusema kuwa amesimama naye wakati akiwa na cheo na wakati akiwa hana cheo.

Akaendelea kusema kuwa anafurahi tena kumuona akikanyaga katika ardhi aliyopewa na Mheshimiwa Rais kuiongoza na ni bahati ya kimungu , na kwamba ni mwisho kuzaliwa kwa mapooza na kwamba ardhi haitazaa tena mapooza.

Mnafikiri alimaanisha nini Mwamba kwa kauli hii ndugu zangu. Mnauonaje ujasiri wa Mwamba awapo jukwaani na Maiki Mdomoni pake.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

Pia, soma=> Rais Samia akiashiriki Misa Maalumu ya miaka 40 ya kumbukizi ya Kifo cha Hayati Sokoine
 
Friends and our Enemies...

Nahapa ninamnukuu Askofu Gwajima.

''Siyo kwamba Makonda/Bashite hafai kwenye kila kitu la hasha, Makonda au Bashite ana vitu vizuri, ana ule uthubutu au udiriki ambao ni jambo zuri.

Lakini hajawa mature enough kuweza kusimamia mambo ya utawala, kama Mkuu wa Mkoa, kwahiyo nakuomba Tena Kwa heshima Mh Rais, nakuomba Mh Rais huyu ndugu yetu muhamishie kwenye mahala pengine,siyo kwenye mambo ya utawala kama haya,kwenye nafasi hiyo.

Mambo ya utawala yanaweza kumfanya atuchafue na akuchafue wewe mbele ya macho ya wananchi,na ukiendelea kumuacha ipo siku atafanya jambo Bashite huyu,utatoka Moshi watu wote tutashindwa kufungua macho.

Sasa inawezekana tukawa tumeongea mambo mengi sana, Leo Mimi Nampa HUKUMU SASA


View: https://youtu.be/OleVb8LOJ14?si=_io5j1AmWJ4SbD3x

Hana mamlaka ya kumfuta mtu yoyote na Wala hawezi na Hana nguvu yoyote " Gwajiba hajawahi kufufua hata panya" nianeno yadogo wake ambaye ni wakili msomi
 
Back
Top Bottom