Rais Magufuli atangaza Baraza Jipya la Mawaziri - 10 Disemba 2015

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
588
1,698
Habari wakuu

Leo Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dr John Magufuli anatangaza baraza la mawaziri wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Tuwe pamoja kulifahamu baraza letu.

attachment.php

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.

Magufuli: Kumekuwa na speculation nyingi na watanzania wamekuwa na hamu kubwa ya kujua baraza la mawaziri, baada ya kusubira kwa muda mrefu, baada ya kuapa tulitakiwa angalau tarehe kumi tuwe tumetangaza baraza.

Tuliona angalau tujiridhishe kwanza, baraza lililopita lilikuwa na mawaziri na manaibu zaidi ya 59, tukaona tuwe na baraza dogo. Hatuwezi kukaa bila baraza, katika baraza hili, wizara nyingi tumeziunganisha na kutakuwa na wizara 18 na tutakuwa na mawaziri 19 tu, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri.

Lengo ni kutimiza ahadi yetu ya kuwa na baraza dogo kupunguza gharama na effective kwa kufanya kazi. Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina elezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure. Watafanya semina elekezi wenyewe ndani kwa ndani.

WIZARA
Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora: Mawaziri ni George Boniface Taguluvala Simbachawene na Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, Naibu waziri Selemani Saidi Jafo.

Ofisi ya makamu wa Rais, muungano na mazingira: Waziri ni January Yusuf Makamba, naibu Luhaga Mpina

Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu: Jenista Joakim Mhagama, Naibu nimemtua mbunge, Abdallah Possi. M ambae ni mhadhiri Dodoma

Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu: Waziri ni Jenista Muhagama, manaibu Anthony Mavunde, Possy Abdallah.

Kilimo, mifugo na uvuvi: Waziri ni Mwigulu Lameck Nchemba, naibu William Ole Nasha

Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano: Waziri bado sijamtafuta, naendelea kumfikiria, Naibu waziri mhandisi Edwin Ngonyani.

Fedha na mipango: Waziri bado tunamtafuta, naibu waziri ni Ashantu Kizachi

Nishati na madini: Waziri ni Professa Sospeter M. Muhongo, Naibu waziri ni Medadi Kalemani

Katiba na sheria: Waziri Harrison George Mwakyembe

Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa: Waziri ni Augustine Philip Mahiga ambae nimemteua kuwa mbunge na kisha waziri, Naibu ni Dr Suzan Kolimba.

Ulinzi na kujenga taifa: Waziri ni Dr. Hussein Ali Mwinyi

Mambo ya ndani: Charles Muhangwa Kitwanga

Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi: Waziri ni William Vangimembe Lukuvi, Naibu Angelina Mabula

Maliasili na Utalii: Waziri bado, naibu ni Ramo Makala

Viwanda, biashara na uwekezaji: Waziri Charles John Poul Mwijage

Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi: Waziri bado hajapatikana, Naibu ni Stella Manyanya

Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto: Waziri Ummy Ally Mwalimu, Naibu ni Hamisi Andrea Kigwangalla

Habari, utamaduni, wasanii na michezo: Waziri Nape Nnauye, naibu Anastazia Wambura

Wizara ya maji na umwagiliaji: Waziri Makame Mnyaa Mbarawa ambae nilimteua kuwa mbunge, Naibu ni Isack Kamwela
attachment.php


=====================

Swali: Kuna baadhi hukutaja, tatizo ni nini hasa kwa wizara ambazo hujateua? Wabunge wa chama chako hawana sifa? Usimamizi wa baraza unatarajia zitafanya kazi zake Dodoma ukiondoa TAMISEMI?

Magufuli: Nilitegemea ungeniuliza kwanini sikuteua siko niliyoteuliwa, subira yavuta heri, hawa wameanza na wengine watafata. Usiwe na haraka. Kuhusu Dodoma tutatekeleza yaliyoko kwenye ilani ya chama cha mapinduzi.

Swali: Umesema hakutakuwa na semina elekezi, utafanya nini waweze kwenda na kasi ya hapa kazi?

Magufuli: Niliyowachagua wote wana CCM na wengi wao ni wabunge, walinadi ya sera hapa kazi na ndio maana haja ya semina elekezi, spidi ni hiyo hiyo ndio maana hatutatumia semina elekezi ya bilioni mbili.

Manyerere Jackton(Jamhuri): Kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri na kwa kulinganisha na tulipotoka, serikali itakuwa imepunguza kiasi gani?

Magufuli: Wewe ndie utapiga hesabu, kwa vile ni mmiliki wa gazeti huwa unapiga hesabu huwa unapata kiasi gani. Utanisaidia katika kupunguza baraza tutakuwa tumesevu kiasi gani na zile tulizosevu za gharama elekezi, kuchelewa kutangaza baraza na wale ambao sijawataja na bahati nzuri nyie waandishi mnaweza kupiga hesabu vizuri. Zipo nchi zina mawaziri wengi mpaka kufikia hata 70, wizara 44, manaibu na mawaziri. Tutakapomaliza tutakuwa na baraza la watu 34 tu.

Wakienda kule mawaziri wakafanye kazi kweli ndio maana sisi tulipochaguliwa tulifanya kazie kweli na hatukwenda kwenye semina elekezi na tulijielekeza, wakajieleze kwenye maeneo yao.

Wasihangaike kufanya sherehe, wamepata kazi ngumu na kama wapo wanaopenda kufanya sherehe wajiandae kufanya sherehe siku wakifukuzwa, contract ni miaka mitano. Wakawafanyie kazi watanzania bila kuwabagua vyama, dini, ukanda au makabila yao. Baraza hili la wizara 15 tumejiridhisha linaweza kufanya kazi tunayowatarajia kuifanya effectivly bila kuwa kwenye masuala ya mchakato. Ngoja tukimaliza uteuzi wote tutajua tumesave kiasi gani ili ziweze kwenda kwa wananchi ya wananchi kama tulivyoahidi.

Raymond Nyamwigula(Uhai Production): Siku saba zimetimia, wafanyabiashara wamesharejesha zile hela?

Magufuli: Swali hilo kamuulize kamishna msaidizi wa TRA.

SWALI: Kuna wizara ina mawaziri wawili, huko kazi ngumu kuliko kwingine?

Magufuli: Kafanye utafiti hio wizara imeunganisha wizara ngapi, utapata majibu.

Swali: Katika baraza, kuna mawaziri wa baraza lililopita, ulizangatia nini wakati wa uteuzi?

Magufuli: Umekosea hata kupiga hesabu, Kafanye hesabu vizuri, waliorudi ni saba na sio kumi? Ukipiga utaelewa ni vigezo gani nilivyotumia.

Asanteni sana na ninawashukuru.



=====================

Kwa taarifa zaidi kuhusu baraza la mawaziri, tembelea => Magufuli atangaza Baraza la Mawaziri lenye Mawaziri 19 Wizara 18, Mawaziri wengi wapya
 

Attachments

  • jbb1.jpg
    jbb1.jpg
    29.6 KB · Views: 67,806
  • IMG-20151210-WA0020(1).jpg
    IMG-20151210-WA0020(1).jpg
    85.6 KB · Views: 49,910
Last edited by a moderator:
Zilitengwa Bilioni 2 kwa ajili ya semina Kwa mawaziri wateule Lakini Raisi Magufuli kafuta hiyo na Fedha kufanyia shughuli nyingi za kijamii
 
Asante JPM.
Pia kasema kuwa hakuna semina elekezi.
Hakuna sherehe ya kuteuliwa , ukifanya sherehe jiandae kufanya sherehe nyingine siku ukifukuzwa.
Pia hongera kwako Mh. angela Kairuki kwa kula shavu tena, piga kazi mama.

3.JPG
 
Last edited by a moderator:
wizara ya uchakuzi n mawasilianio bado hakuna waziri ila naibu yupo
 
Back
Top Bottom