Baa nyingi kufa baada ya Magufuli kufuta maadhimisho ya sherehe za kiserikali

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,908
51,904
Kuna baa zinazomilikiwa na wafanyakazi wa serikali na mashirika ya umma zilikuwa zikiishi kwa wizi.Kukiwa na maadhimisho ya kitaifa wanasingizia wamenunua kreti labda elfu kumi wakati wamenunua mia kutoka breweries kreti zinazozidi wanapeleka kwenye maduka yao ya jumla ya kuuza bia na baa zao.

Hongera Magufuli kuliona na kupiga marufuku sherehe
 
Na zife tu.

Kwanza nyingi zimejengwa kwenye maeneo ambayo yalipaswa kuwa ya wazi.

Kama hilo halitoshi, nyingi zimo katikati ya makazi ya watu ha hivyo kuwa kero na viota vya ukahaba.

Zife tu.
 
baa zikifa maana yake pombe hazitauzika na pombe isipouzika hii nchi haiwezi kusonga ukizingatia makampuni ya pome ndio yanalipa kodi kubwa kuliko migodi na makampuni ya utalii
 
baa zikifa maana yake pombe hazitauzika na pombe isipouzika hii nchi haiwezi kusonga ukizingatia makampuni ya pome ndio yanalipa kodi kubwa kuliko migodi na makampuni ya utalii

Bandari itachukua nafasi usijali Magufuli keshaanza Kudhibiti mianya.Nchi haiwezi endeshwa kwa kutegemea akina Chapombe ambao hawawezi dumu hatamuda mrefu kwakuugua magonjwa yatokanayo na ulevi na ambao hata kulala na wake zao hawawezi kama ilivyo kule Rombo
 
Ha wapi haziwezi kufa na kama ni kufa basi katika 100 ni 0.02 ndio zitakufa.kwasabab walevi wengi ni wajasiriamali na watu ambao hawapo katika mfumo
 
kwa mwendo huu wa mweshimiwa rais lazima heshima itarudi mitaani maana tulikuwa tunadharauliwa sana. MUNGU AMTETEE RAIS WETU MAISHA MAREFU NA ASIPATE WA KUMRUDISHA NYUMA.
 
baa zikifa maana yake pombe hazitauzika na pombe isipouzika hii nchi haiwezi kusonga ukizingatia makampuni ya pome ndio yanalipa kodi kubwa kuliko migodi na makampuni ya utalii

Acha mawazo mgando wewe,hujasikia kuhusu contena 300 zinazopotea bandari?
 
Na zife tu.

Kwanza nyingi zimejengwa kwenye maeneo ambayo yalipaswa kuwa ya wazi.

Kama hilo halitoshi, nyingi zimo katikati ya makazi ya watu ha hivyo kuwa kero na viota vya ukahaba.

Zife tu.
kama shimoni karibu na goig, bamboo karibu massana, China town karibu na intachiki na Nguruko pale engen. Nadhan umenipata vizuri bro
 
Hazifi bwana ila watapunguza tu kuuza bia zisizo rasmi kwenye mitaji yao
 
Back
Top Bottom