Mapadre waanza rasmi kumpigia Magufuli kampeni

kelao

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
8,132
5,785
Katika kile kinachoonyesha viongozi wa dini kuingilia mambo ya siasa, padre Mbano akihubiri ktk Ibada ya leo j2 kwenye Kanisa kuu Katoliki Songea Mjini amesema ujio wa Magufuli ndio jembe haswa lililokuwa linasubiriwa.

Akaendelea kusema kuwa anawaomba radhi wapinzani safari hii waachane na urais wamwachie Magufuli aweke mambo sawa. kaendelea kusema, 'wapinzani tutawapa ubunge, lkn urais Magufuli anatosha' hapa kulikuwa na minong'ono kanisani. Najiuliza ni mapadre hawa hawa na maaskofu mwaka 2005 walisema JK ni chaguo la Mungu lkn sote ni mashahidi wa kilichotokea. Kwa nini wasiwaachie wananchi waamue wenyewe?

Kwa ushawishi walio nao mapadre kwa waumini wao wapinzani wasipokemea haya basi wasahau urais 2015. Pia hawa mapadre wana elimu kubwa sana lkn wanashindwa kutambua kuwa wale waumini wanaowahubiria kuwa ni wafuasi wa vyama mbali mbali..
 
Sio ajabu kwani ccm imetenga fungi la pesa kws mapadre binafsi na wachungaji km walivyofanya huko nyuma. Ila sasa mapadre wachukue tu pesa lkn wasituambie cha kufanya. Tutaanza nào mapadri kwa kwa hili hawana mawasiliano na Mungu
 
Mimi ni mkatoliki lakini mapadre kama hawa hawafai ni mawakala wa shetani!
 
Inasemekana rais mkristo atatoka katoliki tu. Na rais muislamu atatoka ------------tu hivyo basi huyu ajaye ni rais wa katoliki ingawa katoliki ilimtaka Pinda sasa inabidi wamsapoti huyu. EL dhehebu pia limemponza tz ni katoliki na shia. Mi mkatoliki wa kufa na kuzikana ila huyu padri anapaswa kuvuliwa joho mambo ya udini sifagiliii issue inaishia kwenye ukawa vs ccm
 
Mkuki kwa nguruwe! Mmesahau 2010 mapadri walivyompigia debe dk slaa? Hii nchi inaongozwa na kanisa na Kama kanisa limeamua magufuri awe rais hakuna wa kupinga nyie mnasikiliza viongozi wenu wanasema nini na kufata tu, kipindi cha nyuma mliwalaumu waislam kwa kuchanganya dini na siasa ila hata nyie mlikuwa mnachanganya tatizo waislam hawakua wanafiki walisema waziwazi Kama mnavyofanya nyie leo
 
Back
Top Bottom