Wanabodi habarini za majukumu. Mimi ni mjasiriamali ambaye nataka nijikite kwenye kuboresha na kupaki bidhaa za vinywaji vya asili kama mbege, togwa, na vileo vya mananasi n.k. changamoto ninayoipata ni kuwa, bidhaa hizi huaribika ndani ya Muda mfupi kama siku moja au mbili. Naomba mwenye...
Najiuliza RC na DC wanatakiwa kujua kusoma na kuandika, lkn wanasimamia wakurugenzi na wataalam wengine wanaotakiwa kutumia taaluma zao kuendesha mambo. Hii nchi itafika? Au ndo yale ya Waliofeli wanakuwa waganga wa kienyeji wanaokuja kuwaagua wasomi waliofaulu madarasani? Ni TZ tuu huu upuuzi...
Mbona nasikia serikali iko kwenye mchakato wa kukamilisha muswada wa sheria ya KUIFUTA TLS na badala yake kuanzisha BODI YA WANATAALUMA WA SHERIA ambayo wanataaluma wataomba uanachama na itakuwa chini ya waziri wa katiba na sheria?
Hata ubakaji una taratibu zake. Huu ni zaidi ya ubakaji. Ni vigumu kuamini kuwa huu uchuro unaweza kufanyika bila ya maelekezo ya kutoka serikalini. Na kama kuna maagizo kutoka JUU, niruhusuni niamini kuwa nchi ilikuwa imenyooka lakini sasa ndo inapindishwa. Tutaona mengi bado.
Nimepitia kurasa zote sita za michango ya wadau, hadi kichwa kimeuma.
Tukiacha siasa na mahaba ya itikadi pembeni, kama KOSA la DG ni mchakato wa upandishwaji wa bei, nakiri kuna shida ya kimaamuzi. Lkn kama behind the scene kuna jambo, siongei.
Lkn niseme jambo moja. Kinacholitesa taifa, ni...
Ukweli kuhusu Richmond utaendelea kubaki kuwa siri ya Baraza la Mawaziri la kipindi hicho cha Lowasa. Hakuna mkataba wowote unaoingiwa bila kujadiliwa kwenye Baraza la Mawaziri. Hivyo, sisi Raia wa kawaida (layman) tunaijadili RICHMOND kijuu juu tu, ukweli wanaujua mawaziri waliokuwepo.
Kuhusu...
Kenya hawezi kwenda. Kule ni kwa wajanja, si kwa wazembe wasiojali hata rasilimali zao kama ilivyo Tanzania. Ikitokea akienda kenya, ujue anakwenda kumsalimia nyanya yake tu, na si kuwapiga saundi kama atakavyofanya kwetu.
Tanzania si shamba la bibi Bwana?
Ndugu wana JF. Mimi binafsi nimemwelewa huyu Mwandishi wa Mtanzania. Nimeuelewa muktadha wa makala yake. Maadam yeye amejikita katika kuonesha mabaya ya CHADEMA, ingekuwa busara na ukomavu wa akili kama tutamkosoa kwa kuonesha pale alipokosea, na kumwelimisha kuhusu chanzo cha vurugu hizo...
Hao unaowafahamu waliosoma mpaka kuitwa Maprofesa wamelisaidia nini Taifa? si ndo hao hao wachakachuaji? Bora hata huyu aliyesomea Udj, amewasaidia watanzania kutambua haki zao, na ndo maana Watanzania wanamwamini. Pili, Katiba ya Nchi inasemaje kuhusu elimu ya Viongozi?. Inataka mtu awe anajua...
Siwadanganyi ndugu zangu wana JF. Mi mwenyewe sina imani na Jeshi la Polisi, Serikali, Usalama wa Taifa (Kama siyo Uhasama wa Taifa) na CCM. Dr. ana haki ya kutokuwa na imani na hawa watu maana ni matukio kibao ambayo amewapelekea lakini hawajafanyia kazi. Dr. Mwakyembe ambaye ni mwenzao...
Ndugu wana JF. Naungana na alichokisema Ndugu yangu Fred. Mzee Warioba alitulpiga changa la macho. Kama tutakuwa na kumbukumbu vizuri, Baba Ridhiwan alikataza watu kuujadili muungano. Baada ya kuona watu wamelalamika sana pamoja na kuonesha nia ya kutaka kususia mchakato wa utoaji maoni, Ndipo...
Kweli Umasikini wetu ndo kifo chetu. Marekani, Uingereza na utajiri wao wote, hawatagi vyama vingi kama ilivyo Tanzania. Hivi, Msajili wa Vyama vya Siasa kazi yake ndo hiyo ya kutia saini usajili wa vyama, au kuna kazi nyingine anaifanya?. Kazi kweli kweli.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.