Akhsante Muinjilisti kwa mustakabali huu, nimesisimkwa na mwili kusoma haya uloyaandika kiasi cha kutamania aheri
ningekuwa switched at birth lakini naishi na wazazi wawili wanaonipenda na kunijali kuliko dhahma hii
niliyonayo.
kipimo cha DNA ni uthibitisho kwa wana ndugu kwamba mimi ni damu yao.
Muda wangu umeniishia hapa, ila najifikiria iwapo ungekuwa wewe kwenye umri huo unaambiwa lazima ufanye DNA
testing kuthibitisha uhalali wako kwa baba yako, kisha majibu yawe kinyume na unavyoyatarajia.
Nitakuja wasoma...
Hapana, niwie radhi unisomapo vibaya. Uchungu umenitawala ndo maana waona kama sitaki kupokea ushauri. Sawabho. Ninaloliongelea hapa ni post traumatic stress baada ya majibu ya DNA. Tayari najiona mdhaifu kuyapokea majibu yatayokuwa tofauti na ninavyoyategemea.
Mama keshanambia huyu ndiye baba'ngu, na baba keshanipokea kwa mikono miwili na mapenzi yote.
Shida ni ndugu wa baba ambao wao hawajajiridhisha mpaka pafanywe kipimo cha DNA.
Majibu yakija vizuri alhamdulillah. Uchungu wangu majibu yakirudi kinyume na matarajio yangu jamani.
Ndio maana natamani...
Hata mimi nashangaa, naomba dua tusifikie huko lakini mimi ni mtoto sina kauli ya kulisimamisha zoezi hilo.
Inaniuma sana. Natamani mjiweke kwenye nafsi yangu, mwenzenu najiona nisiye na thamani kiasi kwamba ati DNA tu ndiyo itayonikubalisha kwamba mie ni damu yao upande wa ubabani.
Wallahi bado sijalifikiria hilo na mwenyezi Mungu anistiri kwanza, ila wakati ukifika Inshaallah nitapata ujasiri huo iwapo
nitajiridhisha na matakwa ya kuyafanya hayo. Kila jambo linafanywa kwa utashi wa mtu.
Nasali nikiomba madua kutwa kucha, sina raha nikiombea basi hata hicho kipimo kisifanyike,
yaani wajiridhishe tu kwamba mimi ni damu yao, lakini yaonyesha hata baba'ngu
anakosa raha sasa. Ni shinikizo la nguguze.
Yarabi stara.
Nadhani yatokana na hisia za unwanted kid tangia mdogo, Kujiona baba'ngu kanitelekeza na yu wapi miaka yote hii.
Naogopa kuumizwa tena na hayo majibu baada ya kuonana na baba na ndoto zangu kutimizwa.
Hapana, nimekuwa natamani na mimi niwe na baba yangu. Nimevumilia mengi kuwaona wenzao na baba zao. Baada ya mwaka
na kufaidi raha na mapenzi ya baba niambiwe kumbe si baba'ngu kwakweli tayari ishaanza kuniuma kabla hata hatujapima. Natamani nikatae kupima Jamani. Sijui nimekosea nini Mwenyezi...
Loh! Hapo pananitia uchungu zaidi kwani kwa miaka yote hii amekuwa ananionyesha kwa picha baba'ngu ni huyu, halafu baada ya majibu negative, nianze kumhoji tena aniambie ukweli?
Picha ni taswira inayobakia kutokana na muonekano wa mtu kutokana na tukio na kipindi maalumu.
Kuzitupilia mbalini, au kuzihifadhi kutatokana na utashi wa mtu. Kwangu mie binafsi sioni hasara kuhifadhi
kumbukumbu ya matukio ya awali, kwani nishajikubalisha ya kale hayanuki.
Umri wangu ni miaka ishirini na mmoja. Wazazi wangu hawakuwahi kuoana wala kuishi pamoja kwani nilipokuwa conceived (wazazi) wangu walikuwa bado kwenye late teens, wakati huo wanafunzi. Katika mazingira hayo, umri wangu wote nimelelewa na familia ya mama yangu kisiwani zanzibar katika maadili ya...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.