Pole mtoa mada kwa kudhani kila aliye ccm ni mwana ccm. Kuna ambao tumewabakiza huko kwa kazi maalum. Wao hufanya kazi ya ukawa ndani ya ccm, na kwa kweli wanaifanya kwa uadilifu mkubwa kiasi kwamba tunaweza kutembea kifua mbele kwamba come oct 25, ccm kwisha kabisa.
Hata mimi ntashangaa kura usipompa Lowassa, maana kwa maneno ya Sophia simba Lowassa ndio mwanaume wa shoka nchi hii. Sijaona mgombea mwingine kwa mwaka huu, wengine labda wajaribu miaka ijayo. Lowassa kaenea, anatosha.
Kuchafuka ndo dili mheshimiwa, si unaona waliochafuka na Richmond, escrow, nyumba za serikali, kupeleka wake shopping dubai kwa gharama za serikali, nk walivyo maarufu sasa. Wasio chafuka akina mahiga, Bilal, mpina, drs 7, nk unaona wana umaarufu wowote. Chafuka mkuu kadiri iwezekanavyo.
Ndugu yangu. Lowassa hatafika kwa wananchi kwa tkt ya ccm hata angekua na nguvu kama za Maywether, labda kwa wananchi atafika kwa tkt ya ACT. Kamuulize J. Malecela alichofanyiwa. Hao 'wanaomkubali' sio wananchi, ni vikundi vya wana ccm. Upinzani watapata urahisi sana wa kupiga kampeni dhidi ya...
Mtoa mada dont underestimate Magufuli. Huyu jamaa kama umemgundua si mtu wa porojo, ni vitendo tu. Amejizuia sana kutoa hotuba za mbwembwe. Lakini utendaji wake tangu alipoteuliwa kwa mara ya kwanza kwenye baraza la mawaziri hakuna mtanzania atakayeusahau. Sina hakika na January lakini kama...
Zamu kwani tuko kwenye foleni ya maji Hapa!!!!! Watanzania tujitahidi kuwa serious kwenye issues! Kwa mawazo madogo kama haya ni ndoto kupiga hatua ya maendeleo
Asipozuilika ndani ya chama, atazuilika nje ya chama. anaweza kuiweka NEC ya ccm mfukoni, lakini hawezi kuwaweka watanzania wote mfukoni. Kumpitisha lowasa ni kujaribu sumu kwa kuionja.....
Prof. Muhongo yuko vizuri sana, ila wakitumia na kigezo cha kujiuzulu kwa kashfa ya ESCROW, wanaweza kumweka kando. vinginevyo anaweza kuingia tatu bora badala ya Mwigulu.
Hajapitishwa Slaa, ila nadhani kwa UKAWA, yeye ndo anapewa nafasi kubwa zaidi akifuatiwa na Lipumba. Kwa kweli huyu jamaa (Dr. Slaa) ndo anayewanyima usingizi watu wa ccm
Mpaka kufikia jana jioni tar. 10/06/2015, takriban wanachama 29 wamechukua fomu au kutangaza nia ya kugombea urais wa nchi hii.
Hii ni idadi kubwa sana ya watu kutangaza kutaka urais wa nchi yetu, nadhani kiti cha rais sasa kimeonekana cha kawaida sana, kiasi kwamba kuna ambao wana elimu ya...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.