Search results

  1. K

    Mwanasiasa gani Tanzania mwenye mvuto namna hii?

    Uko sahihi kwa asilimia zaidi ya 100,itachukua muda mrefu kumpata mwanasiasa mkweli,mwenye mvuto na uchungu wa nchi yake wa aina ya Dr.Wilibroad Slaa.Kipindi chake cha ubunge wa karatu kimethibitisha hilo na haswa michango yake alipokuwa bungeni pia imedhihirisha ubora na umakini wake.Ni bahati...
  2. K

    Yuko Wapi Sakina Dattoo?

    Huyu mwanahabari yuko Uingereza anajiendeleza kielimu.Tunamuombea ahitimu masomo yake ili arudi kuiendeleza taaluma yake ktk kutatua changamoto zinazotukabili hivi sasa.Hakika amejaliwa kipawa cha kujieleza vizuri na kukubalika miongoni mwa jamii.
  3. K

    Selikali itupie jicho biashara za wachungaji hawa

    Hii mada in ukweli kwa asilimia 100,Dini imekuwa biashara inayowalipa wajanja wachache mijini kupitia mgongo wa maskini wengi waliokata tamaa na maisha.Wamefikia hatua ya kumghilibu Mungu kupitia mgongo wa makanisa yao yenye waumini Dar es Salaam pekee na wachache mikoani.Kuna mfano mzuri sana...
  4. K

    Marital "Walk-out"

    Kuna sababu kadhaa za msingi zinazosababisha Mahusiano/Ndoa za siku hizi kutokudumu.Mabadiliko yanayoletwa na "Utandawazi" na kubadili kabisa mfumo sahihi wa maisha umetupotosha kwa kiasi kikubwa sana ktk suala zima la mapenzi.Kinachotokoea ni kwamba ile falsafa ya kujitoa kwa hali yeyote kwa...
  5. K

    Ivory Coast Elections: Who is the Winner?

    Ni moja ya nchi zinazowakilisha mifano michache kati ya mingi inayohusu mapungufu ya Tume ya Uchaguzi pamoja na katiba ya nchi.Laurent Bagbo ktk kipindi cha utawala wake kuelekea uchaguzi ilimlazimu kuteua Tume ya Uchaguzi ya mpito kusimamia uchaguzi wa majuzi lakini hakufanya hvyo kwasababu...
  6. K

    Mwitikio wa Baraza, wale waliotemwa na Mengineyo

    kwa mtizamo awamu hii amelazimika kusikiliza maoni ya vigogo wa chama na wananchi baada dhoruba lililowakumba kwenye uchaguzi.kimsingi mtandao uliomwingiza madarakani ndio uliomwangusha kwa kiasi kikubwa na hivyo basi kwa wateule hawa wapya kuna matumaini ya kurudisha imani iliyopotea kama...
  7. K

    Chonde! Chonde! Mh.JK jibu hoja usifanye mzaha!

    Hotuba yake jana ilikuwa na mapungufu mengi sana haswa suala la udini ambalo wameliongea sana kipindi cha kampeni.Kimsingi sioni Udini unatokea wapi maana yeye mwenyewe juzi ameteua wabunge watatu wote waislamu,sijui tulitafsiri vipi?.Suala hili wamelifanya ajenda ili kumpunguza makali Dr.Slaa...
  8. K

    Chadema now has an upper hand and if they desire, they will shine!

    Nakubaliana na watangulizi wa hapo juu kuwa kitendo walichokifanya wabunge wa CHADEMA jioni hii ni cha kuungwa mkono na wapenda demokrasia wote.Nina imani hawakukurupuka kuchukua uamuzi huu maana wana wanasheria mahiri na makini na hivyo kufikisha ujumbe husika kwa jumuiya ya kimataifa.Naamini...
  9. K

    Mapendekezo ya muundo wa baraza la mawaziri - 2010-2015

    Awamu hii itamuwia vigumu sana kupanga baraza la mawaziri sababu ana watu wengi sana wa kuwalipa fadhila pamoja na kuanguka kwa baadhi ya waliokuwa mawaziri wake wa kutegemewa.Tatizo ni kuwa wengi wao ni wachumia tumbo wanaojivicha rangi ya kijana kwa misingi ya kupata vyeo na madaraka na mwisho...
  10. K

    Hongera cuf

    Ni kweli ametusaidia sana na hilo linaonekana wazi kwenye matokeo ya kura ambazo zimekuwa zikipigwa tangu uchaguzi wa spika na wengineo.Wasiwasi wangu ni kwamba kwa mwenendo wao wa mashirikiano na C.C.M wanajiweka kundi gani kwa huku bara.kimsingi wanacheza pata potea kwasababu itakapotokea...
  11. K

    TUJIKUMBUSHE - Kweli hata mimi kura yangu kwa JK na CCM - BIG NO!!

    Hata kama kuna mazuri aliyofanya kama yamezidiwa uzito na mabaya unatarajia yaongelewe yapi?.Ni wazi yatazungumzwa mabaya yanayoathiri maisha ya walio wengi kuliko mazuri yanayonufaisha wachache walio na ubinafsi wa kupitiliza.Tukubali tunahitaji mabadiliko na muda ni huu na si vinginevyo
  12. K

    Sabodo aichangia CHADEMA milioni mia moja

    Hakika amekuwa mfano wa pekee kwa wapenda demokrasia na mageuzi nchini maana wengi hawakuamini hapo jana walipoangalia kupitia luninga.Kwa waafidhina wa C.C.M ni pigo kwao maana kwa muda mrefu wamekuwa wakikejeli wapinzani kana kwamba ni maadui.Hivyo wajiandae kwa kampeni kabambe wakiwa tayari...
  13. K

    Hatuhitaji kirusi cha ccm hai

    Kweli kabisa miaka hii mitano jimbo limekosa mwakilishi makini,hivyo ni vema Freeman Mbowe akarudi kuliongoza ili kuwaletea maendeleo wananchi wa Hai waliopoteza matumaini.Mbunge wa sasa anajiaminisha kurudi lakini ukweli ni kwamba ana wakati mgumu na chama chake.Kila la kheri kwa Mwenyekiti wa...
  14. K

    Tabasam la Sitta kwa wananchi au wabunge wake?

    Spika nae amekuwa mtu wa maslahi zaidi pamoja na kuhubiri kasi na viwango ambavyo vimemshinda kutekeleza ndani ya chombi hicho.Sasa tunapokaribia uchaguzi na wanajua hawawezi kushinda bila kutumia hela ndipo inapowalazimu kumshurutisha Mkulo kuwapatia fedha hizo hivi sasa ili waweze kuandaa...
  15. K

    Corruption pervasive in Tanzania - report

    I concur with the think tank report on corruption in Tanzania,because in the past four years we have witnessed a significant change in life of the minority.These have accumulated a masive wealth thought to acquired through dubious ways the major one being grand corruption.That's why the gap...
  16. K

    Toa Maoni Yako Hali ya Kisiasa Tanzania

    Siasa za nchi hii kwa kiasi kikubwa zimetokea kutawaliwa na tamaa ya kujitajirisha kutokana na maslahi yatokanayo na kazi hiyo.Ndio maana basi mtu yeyote mwenye uwezo kifedha anatamani sana kuingia kwenye siasa akitumaini kuwa baada ya muda fulani atachuma zaidi ya alichowekeza.Kwa bahati mbaya...
  17. K

    Mrema wa TANROADS Kikaangoni

    Kinachotushangaza wengi ni kuwa na jeuri kushinda mamlaka zilizo juu yake kiutawala kufikia hatua ya kutokumsikiliza Waziri na Katibu Mkuu wake.Huyu bwana amekuwa Mungu mtu kwenye taasisi hiyo na ndio maaana miradi mingi ya barabara imekwama kwenye kipindi chake.Bado tunahoji mamlaka...
  18. K

    Ni kosa lipi alilofanya jk linalomgharimu hadi sasa?

    Kosa la kimsingi alilolifanya ambalo mtawala yeyote asiye makini litamsumbua na kuingiza wanamtandao kwenye baraza lake la mwanzo wengi wao wakiwa ni mizigo ya utawala uliopita.Matokeo yake baada ya Richmond wote walilazimika kuanguka na kuanza moja na watu wasio wake.Atalikumbuka sana kosa hilo...
  19. K

    Elections 2010 Wengi wa wanafunzi wa vyuo vikuu kutopiga kura 2010

    Hakuna lolote ni ghiliba za kisiasa kuwanyima wanafunzi fursa ya kufanya maamuzi wanayoyataka.Kwa jimbo kama la Ubungo lenye upinzani mkubwa sana kwa C.C.M inawalazimu kusogeza mbele tarehe ya kufungua maana wanafunzi wakiwepo ni dhahiri watashindwa tu.Hivyo hii yote ni mikakati ya kufanya hila...
  20. K

    Msaada wa mawazo ya Biashara/ Mradi

    Nafikiri na wewe unaweza kugundua kwa nini kimya,msaada unaoomba hapa si mahala pake kuupata maana hii ni sehemu ya kujadili siasa na si mengineyo.Hivyo ni vema ukaihamisha na kuipeleka sehemu ya biashara iliyo humu humu JF.Nafikiri nitakuwa nimekusaidia
Back
Top Bottom