Naona JF member Lizaboni unanipa majukumu nisiyostahili kutokana na taarifa niyotoa kuhusu UKAWA na Profesa Lipumba. Nikiwa Muasisi wa CHADEMA nafuatilia kwa karibu sana maendeleo ya chama. Pia nikiwa Raia anayefuatilia mchakato wa Katiba Mpya, naelewa jinsi Bunge Maalum la Katiba lilivyoundwa...
Lipumba siyo Mbunge. Wote walioteuliwa ni Wabunge wanaohudhuria Bunge la Bajeti. Bunge Maalum la Katiba ndiko Profesa alipo na huenda akawa ni 'Naibu' Kiongozi wa Upinzani wa hilo Bunge Maalum endapo UKAWA watujiunga nalo August 2014.
Nilisikiliza Mheshimiwa Tundu Lissu na nasikitika kwamba sikubaliani naye jinsi alivyoeleza shutma juu na dhidi ya Mwalimu Julius Nyerere, Baba na Muasisi wa Taifa letu. Inajulikana na umma wa Watanzania, kwamba mimi binafsi, kama Waziri wa Fedha, nilitofautiana na Mwalimu, nikajiuzulu Uwaziri...
Nilimsikiliza Mheshimiwa Tundu Lissu na nasikitika kwamba sikubaliani naye jinsi alivyoeleza shutma juu na dhidi ya Mwalimu Julius Nyerere, Baba na Muasisi wa Taifa letu.
Inajulikana na umma wa Watanzania, kwamba mimi binafsi, kama Waziri wa Fedha, nilitofautiana na Mwalimu, nikajiuzulu...
Hivi kuna Mwenyekiti au kiongozi yeyote anayeweza kuzuiya kundi lolote kukutana mahala popote na kukubaliana kujadili Katiba Mpya au jinsi ya kukusanya mawazo juu ya kutumia wakati wao wikiend hapo Dodoma? Mbona Mhe. Samuel Sitta anadhani amepewa majukumu ambayo hayatekelezeki? Kwani Ukawa ni...
Ronald Reagan na Winston Churchill walivuma sana nyakati zao wakiwa wamekomaa kama Mugabe. Wewe unataka wakina Clinton waliokuwa wanashughulikia wakinadada Lewinski tu?
Nimefungua computa yangu baada ya kupigiwa simu, nikaona yanayosemwa ktk hii thread na pia kwamba wananitaja kwamba CHADEMA ni chama cha ukoo wangu na ni SACOs ya Freeman Mbowe mkwe wangu. Kwa mantiki gani?
Singetaka kumaliza wakati juu ya ACT, ambacho ni chama kilichoanzishwa wiki mbili...
MwanaJF Chama,
Samahani sikuelewi. Ridhiwani kashinda kugombea jimbo alilowakilisha babake. Mimi nahusikanaje? Nakuhakikishia akiteuliwa na chama chake, atapambana na mteule wa CDM ambaye anajiandaa mpaka kieleweke!! Hakuna Kulala!!!
Nadhani wanaotumia nguvu zaidi kutetea umaarufu wao, ni viongozi wa mafisadi waliopiga picha za kumbaka na kumdhalilisha Hii ni aibu tupu kwa CCM!!!!!!!!
This is sad news indeed. Tanzanians will miss his constructive contributions to National issues.
May the Almighty God rest Sengondo Mvungi's soul in eternal peace!! AMEN.
ZeMarcopolo,
Kibogo,
Nimekwisha sema awali katika michango yangu humu jamvini, kwamba sifurahii kujibizana na wanaJF, hasa wale wanaotumia majina ya kificho (pseudonyms).
Lakini naona nj vema nimweleze Ndugu Kibogo kwamba mwaka 1979, Rais Nyerere hakunisimamisha kama Gavana wa BoT. U-Gavana...
Dada Mamndenyi,
Nashauri wasiliana na Profesa James Teri, Mkurugenzi wa TaCRI ambaye ataweza hata kupeleka wataalamu hapo shambani kwako wakatambua tatizo na kukushauri la kufanya. Simu yake ya kiganjani ni 0754 473895.
ZEMarcopolo,
Nimeeleza kwamba nikiwa Gavana BoT (1965-74), Freeman Mbowe na binti yangu Lillian walikuwa watoto wachanga, na singeweza kuwashirikisha katika miradi. Freeman alikuwa na miaka 4, na Lillian alikuwa na mwaka mmoja!!
Licha ya kwamba hizi zilikuwa enzi za Ujamaa, babake Freeman...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.