Hatua ya maswali ya dodoso (Cross Examination) kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, yanatarajiwa kutamatishwa leo Agosti 27, 2026 na kufungua mlango kwa shahidi mwingine wa Lissu kupanda kizimbani kwaajili ya kutoa utetezi wake.
Jana Agosti 26, 2026, Tundu Lissu alihitimisha kutoa ushahidi wake mbele ya jopo la majaji watatu, wakiongozwa na Jaji, Dunstan Ndunguru, ambapo ambapo baada ya hatua hiyo, upande wa Jamhuri (Washtaki) walipewa nafasi ya kuuliza maswali hayo kwa mshtakiwa...