Vilio vya Wastaafu wa majeshi vitatuliwe haraka, kinachoendelea ipo siku kitatengeneza ‘matunda yasiyofaa’

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,340
5,565
Hivi karibuni kumekuwa na vilio kadhaa vya Wastaafu wa Majeshi yetu mbalimbali kuhusu viwango vya fedha ambavyo wanavipata.

Awali ilikuwa ni nadra kuona Mstaafu wa Jeshi lolote lile akilalamika hadharani, lakini kadiri siku zinavyosonga mbele ndivyo ambavyo vilio vimeendelea kusikika mdogomdogo na sasa imekuwa kawaida kuona malalamiko hayo hata kwenye vyombo vya habari.

Wazo la kuandika hoja hii nimekuwa nayo muda mrefu kutokana na ninayosoma yanayoendelea kuhusu Wastafu hao, lakini wazo limekuja baada ya kushuhusia Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka 2024/25 iliyowasilishwa leo Bungeni, Mei 20, 2024.

Hii siyo dalili nzuri, kuona Wastaafu wa Majeshi wakilalamika kuhusu stahiki zao, kwani kwa mujibu wa kanuni zao ni kuwa unapokuwa member wa Jeshi wewe siku zote ni mwanausalama tu hata kama amestaafu.

Inapotokea vita au dharura yoyote ya Nchi ambayo inahitaji msaada au nguvu ya Wastaafu, wanalazimika kurejea mzigoni na kulitetea Taifa.

Hivyo, wanapopitia hali kama hiyo ya masononeko sio jambo zuri kiusalama pia, tunawaona huku mtaani wanaishi maisha magumu, wengine wanakuwa ombaomba kisha haohao ndio tuwategemee kukitoke dharura, watakuwa na moyo kweli wa kulipigania Taifa?

Mfano soma haya maandiko kuhusu Wanajeshi wetu wanavyolia baada ya kustaafu au maoni kuhusu Wanausalama waliostaafu:

= Kikokotoo kilivyomtenda mstaafu Jeshi la Magereza
= Kasoro kubwa katika Ofisi ya Hazina (Kitengo cha Malipo ya Pensheni za Wastaafu)
= Rais Samia, Watumishi Wastaafu wa Jeshi tunaomba utusaidie kupata stahiki zetu, tunateseka

Tunatakiwa kujiuliza na kujua kuwa kwani hao Wastaa si ndio wengi wao wamewafundisha kazi hawa waliopo kazini sasa? Sio hapo tu kuna wengine ndo wazazi wao, walezi wao, ‘role model’ wao na mengine mengi.

Kuna Wastaafu ambao ndio waliowapa connection Watumishi waliopo Jeshini kwa sasa, hivyo wanapoona wakubwa wao wanafanyiwa haya wanayofanyiwa unadhani inakuja picha gani kichwani?

Kuna wale waliokuwa Watumishi wa vikosi mbalimbali vya Jeshi, niliona andiko lao wakilalamika, kuna yule mtumishi wa Magereza ambaye nimeona andiko lake akilia katika Gazeti la Mwananchi akidai wakati akitegemea kupata Shilingi milioni 55 ameambulia Shilingi Milioni 21.

Kuna wengine ambao wanawekwa katika Kundi moja la Wastaafu wanaostahili kupata haki yao wakiwemo waliostaafishwa kwa ugonjwa, waliofariki wakiwa kazini na waliostaafu kwa taratibu wote vilio vimekuwa vingi.

Wito wangu, Serikali iangalie jambo hili kwa jicho la kipekee, wasipoangalia wanaweza kutengeneza sumu mbaya ambayo miaka michache ijayo ikaathiri vyombo vyetu vya usalama.

Athari ambazo zinaweza kupatikana ni watu au kizazi kinchochipukia na kuona Wazee wao wakipta mateso, wao watakataa kujiunga na majeshi yetu au kufanya hujuma au kukosekana kwa uwajibikaji kam ambavyo majeshi yanasifika kwa sasa.
 
Je wastaafu wa kada zingine ndo wsteseke??
 
Kama kuteseka ndio sababu ya kuwa na maamuzi ya uhasi basi hawatakuwa na utimamu sababu huku nje raia kibao wastaafu wa kada mbali mbali wanapitia maisha magumu.
 
View: https://www.youtube.com/watch?v=UCTELHWkmZY

Tuko busy tunawatafutia fursa 😂 😂 😂 🤣 🤣 🤣 😀 😀 😀
 
CCM imeharibu sana mfumo wa utawala bora na uwajibikaji ndiyo maana hivi vikokotoo hakuna wa kuwasaidia wastaafu hadi labda mkuu wa nchi ajisikie kuwa imetosha sasa na wakiondoe...

Tanzania inahitaji kura yako ili iweze kubadilika kutoka kwenye kuporomoka kuelekea kwenye kukua
 
Kura siyo tatizo. Tatizo ni Tume ya Uchaguzi na Mfumo wote wa Uchaguzi. Kumbuka JPM aliwahi kusema akiwaambia Wakurugenzi wa Miji, Wilaya ambao ndiyo wanaosimamia Uchaguzi kwenye maeneo yao kuwa "nikuteue, nakulipa mshahara, nakupa usafiri, nakupa nyumba halafu umtangaze Mpinzani kuwa ni mshindi" Sasa hapo unategemea kura kweli!!!
 
Wao wamefundishwa kutii...wanatakiwa watii na kupokea hicho kiasi wanachopewa bila kuhoji wala kulalamika.
 
Wote tunajenga nchi moja, mwanajeshi au askari hapiti kwenye barabara ya jeshi tu, kula chakula cha jeshi pekee, kutibiwa na daktari wa jeshi pekee, kusomesha watoto wake kwenye shule za jeshi tu....na hao wote anaowalinda katika taifa pia wanamlinda yeye kwa kuhakikisha anapata kila anachohitaji ....na wote tunazeeka na kustaafu...hivyo hakuna anayetakiwa kuteseka na kunyimwa haki zake nikimaliza muda kwa mujibu wa sheria na kustaafu changu nipewe kwani ni jasho langu.
 
Back
Top Bottom