Ukilifahamu hili hautamdharau mtu yeyote kwa kazi au cheo alichonacho

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,911
36,754
Mungu alipomaliza kuiumba dunia na kisha kumuumba mwanadamu ambaye alipewa milki yote ya duniani ili aitunze na kuitawala aligawa majukumu kabla hatujauona uso wa Dunia. Sisi wanadamu tunahangahika kupata nafasi nzuri zenye kutukuka. Tunahangahika kupata vyeo vitamu vyenye kunguruma.

kumbe kila kitu kiko structured.
Kuna watu hata wenyewe hawajawahi kufikiri kupata nafasi walizo nazo ghafla tu ukawapata upepo wamekuwa mawaziri, Marais, makatibu wakuu n.k.

PHilip Mpango VP alikuwa busy kwenye utumishi wa ku calculate fedha mara anapata ubunge wa bure, mara waziri wa fedha mara Makamu wa Rais sasa.

Kuna vipanga nimesoma nao huko shule za vipaji mtu anaweza kusoma ukurasa mzima kisha anarudia kusoma au kuandika bila kuruka nukta wala mkato leo wako wanaendesha bodaboda.

Haiwezekani wote tuwe bodaboda, wote tuwe walimu, wote tuwe wajeda, wote tuwe wahasibu.
Hapo ulipo ndipo pako haswa , jivunie, mtu asikudharau. Usikubali mtu akuyumbishe.

Mimi ndoto zangu zilikuwa kufanya kazi Uhamiaji, tiss au pccb tu. Na ilifika muda kote kulitiki yaani milango ilikuwa wazi lakini sikupata huko. Niliumia kwa muda mrefu lakini baada ya kugundua Siri hii sasa nina amani.

Nikimwona afisa za hizo idara namwona kama watu wengine tu. Kama ninavyomwona mzoa taka ndivyo ninavyomwona Rubani. Ninavyomwona Engineer ndivyo ninavyomwona mshona viatu.

Ridhika hapo ulipo , kama una vituo vingi utapitishwa kote na Mungu bila wewe kutumia nguvu. Relax.
 
Usingebold maandishi hivyo yanaumiza macho kusoma bhana 🤒😎
20240424_005944.jpg
 
Back
Top Bottom