Tofauti kati ya masalafi na wahabi

Asante sana mkuu. Je salaf aweza kuwa muumini wa dhehebu lolote (sunni, shia etc) ama salafiyyah ni dhehebu kamili linalojitenga na madhehebu mengine katika Uislamu?
Kama nilivyoeleza maana ya Salaf kiistilahi hapo nyuma, ataingia yoyote yule ambae atakae FANYIA KAZI mafundisho ya Dini kwa uwelewa wa wema waliotangulia (Salaf), yaani iwe IBADA, ITIKADI NA MIAMALAAT ni kama walivyoelewa Maswahaba kisha wanafunzi wao (Attaabiina)kisha wanafunzi wao (Atbau ttaabiina).

Ikiwa utafanyia kazi Dini kwa njia hii basi utakuwa umeifanyia kazi ile hadithi ya Mtume (swala na salamu ziwe juu yake) aliposema "... Umma wangu utagawanyika katika makundi 73, yote yataingia motoni isipokuwa kundi 1, Maswahaba wakamuuliza ni kundi gani hilo? Akasema ni lile litakalokuwa juu ya mwenendo wangu na maswahaba wangu" hii ni dalili kuwa ni LAZIMA kufuata uelewa wa Maswahaba.

Sasa kwa msingi huo aliouweka Mtume (swala na salamu ziwe juu yake) utaona watu wengi wanaanguka, wakiwemo mashia na jamaa zao masufi, maana wao utaona wanaenda kinyume na UWELEWA wa Salaf (Maswahaba) ktk Ibada, Itikadi na Miaamalaat.

Allahu a'lam
 
Wakuu amani kwenu,

With due respect naomba kujuzwa masalafi ni nani na wahabi ni nani? Ni nini tofauti zao kiimani na kiutamaduni? Je, Wanachangama vipi na Waislamu wengine wa madhehebu tofauti?

Karibuni tupeane elimu.
Unahisi huku utapata msaada unaoutaka mkuu kwa nn usiende sehemu husika
 
Wakuu amani kwenu,

With due respect naomba kujuzwa masalafi ni nani na wahabi ni nani? Ni nini tofauti zao kiimani na kiutamaduni? Je, Wanachangama vipi na Waislamu wengine wa madhehebu tofauti?

Karibuni tupeane elimu.
Salafi na Wahabi tofauti ni jina tu ila ni mtu yule yule.

Salafi kwa maana wema waliyotangulia. Aliyekuja na huu msimamo wa kuhuisha hii hali anaitwa Sheikh Muhammad Abdel Wahhab. Ya kwamba njia wanayoishika waislamu si sahihi wamepotea. Njia sahihi ni njia ya wema waliyotangulia yaani Salafi.

Kwa itikadi ya kwamba sunna zinapotezwa hazifuatwi kama zinavyotakiwa kinachotakiwa ni zihuishwe. Kwa maana wanazinusuru sunna. Kwa hilo wakasema wao ni Answar Sunna.

Huo ndiyo ulikuwa msimamo wa Sheikh Muhammad Abdel Wahhab. Wafuasi wake wakaitwa jina la huyo mwanzilishi yaani Wahhabi.

Hivyo tofauti ni jina tu! Salafi ndiyo Wahhab na ndiyo Answar Sunna.
 
Back
Top Bottom