Season 2: Akili ya binadamu

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
3,711
9,385
Habari wakuu,

Baada ya kuijadili kwa kina thread yetu pendwa Akili ya binadamu katika huo uzi mimi nilikuwa mchangiaji mkuu, niliichambua na kuielezea akili ya binadamu ktk angle ya kibaiolojia, nikiri tu kwa kusema kuwa akili ya binadamu ni complex sana huwezi kuichambua ktk angle moja peke yake ukaimaliza.

Niliahidi ntarudi kuichambua tena, ktk uzi huu tutaichambua ktk angle ya kisaikolojia (human psychology) na itakua ktk mtindo wa episodes, nafanya hivi kwa sababu ni thread pana sana pia itatumika ktk thread zijazo kama reference.

EPISODE 1
Mwanasaikolojia nguri Freud Sigmund anaichambua akili ya binadamu kwa kuigawa katika vipande vitatu ambavyo ni id, ego na superego
model-theory-freud-s-psychoanalytic-unconsciousness-people-minds-psychological-analysis-iceber...jpg


Id

Ni mkusanyiko wa matamanio, tamaa, hamu, uchu au kiu ya kitu fulani (all desires and needs) haya mambo yote huanzia ktk akili yako na jina lake la jumla ni "id" segment ya akili, mfano tamaa ya pesa, tamaa ya ngono, tamaa ya mali, uchu wa madaraka, kiu ya pombe, kiu ya maji, njaa, hamu ya kula chipsi, kutamani mwwanamke mwenye makalio makubwa n.k kila binadamu anapozaliwa huzaliwa na hii akili ya awali.

ego
Hii ni sehemu ya akili inayohusika na kucontrol matamanio yote (id) na kuyatimizia kwa kuzingatia njia sahihi zinazofaa ktk jamii mfano tumeona hapo juu akili imetamani mwanamke mwenye makalio makubwa, ego itaprocess hiyo information na kuja na analysis kuwa wewe umeoa una mke na watoto hivyo basi kuchepuka ni kukaribisha magonjwa na kuhatarisha ndoa yako unakuja na conclusion kuwa ukaushe tu usimtongoze huyo mrembo mwenye makario makubwa, mfano mwingine ni unakiu kali ya maji umeagiza maji lakini uliyemtuma kachelewa sana halafu hapo pembeni yako kuna dogo anachupa ya uhai anakunywa maji akili yako inakutuma umpokonye unywe wewe ila unakausha unafikiria na kuona kuwa sio ubinadamu unaamua kukausha usubirie tu huyo ulomtuma mpaka atakapokuletea maji yako. Kinachofanya kazi hapo ni ego.

Superego
Hii ni sehemu ya akili inayohusika na haki, majuto pamoja na uchanganuzi kuwa jambo fulani ni haki na jambo fulani sio haki, hii sehemu ya akili hu control ""id" na "ego' kwa mpigo. Mfano umepewa jukumu la kukusanya michango kwa watu ili ukalipie bili ya matibsbu ya mtoto yatima aliyelazwa anasubiri hizo pesa afanyiwe upasuaji wewe unaingiwa na tamaa unaamua kwenda bar kulewa then yule mtoto unakuja kusikia amefariki unajikuta ni mtu mwenye majuto sana na unajilaumu sana kwa upumbavu wako kuwa hukutenda haki na unajiona ni mtu mwenye hatia.

Ktk hizo sehemu tatu zote za akili zinatakiwa kubalance, na ndio zitakazo ongoza mienendo yako na tabia yako, kimoja wapo kisipo balance utakuwa mtu fulani wa ajabu ajabu ktk jamii.

INAENDELEA
 
EPISODE 2
kuna mdau mmoja aliwahi kuanzisha uzi uliokuwa na title ikisomeka hivi "kuna muda shetani huwa anapiga story na Mungu" View attachment 2974037picha inaonyesha mfano wa akili jinsi ilivyogawanyika ktk sehemu tatu ndani ya mwili mmoja


yule jamaa hakukosea, ipo hivi id ni shetani ego ni wewe na superego ni jeshi la malaika mfano kuna wazo limekujia ghafla ktk akili yako wazo lenyewe ni la kumtamani mke wa mudu (wazo la shetani) ego(wewe) itafanya analysis itakupa faida na hasara lakini superego(malaika) watakuambia kuwa kufanya hivyo sio sawa na sio haki kataa zinaa, yaani kuna kuwa na mvutano wa mawazo ya pande mbili kwenye akili yako, na ni lazima upande mmoja ushinde
8psMY7eNkdw1cUp1686596499547.jpg


dkoac8-4acb3461-1144-4942-a9f3-21435cf1248e.jpg

Id ikishinda vita ni shetani kashinda, superego ikishinda ni malaika kashinda. Mzani lazima ubalance
id-ego-superego.jpg
 
EPISODE 2
kuna mdau mmoja aliwahi kuanzisha uzi uliokuwa na title ikisomeka hivi "kuna muda shetani huwa anapiga story na Mungu" View attachment 2974037picha inaonyesha mfano wa akili jinsi ilivyogawanyika ktk sehemu tatu ndani ya mwili mmoja


yule jamaa hakukosea, ipo hivi id ni shetani ego ni wewe na superego ni jeshi la malaika mfano kuna wazo limekujia ghafla ktk akili yako wazo lenyewe ni la kumtamani mke wa mudu (wazo la shetani) ego(wewe) itafanya analysis itakupa faida na hasara lakini superego(malaika) watakuambia kuwa kufanya hivyo sio sawa na sio haki kataa zinaa, yaani kuna kuwa na mvutano wa mawazo ya pande mbili kwenye akili yako, na ni lazima upande mmoja ushinde
View attachment 2974039

View attachment 2974040
Id ikishinda vita ni shetani kashinda, superego ikishinda ni malaika kashinda. Mzani lazima ubalanceView attachment 2974045
Hiyo 👆🤣 uliyo weka tayari mods wamepita nayo
 
Umezunguka sana, kwa kiswahili rais ndo ile tunasemaga "Ngoja kwanza Halmashauri yangu ya kichwa ifanye kazi"
 
Back
Top Bottom