Referee Camera (RefCam)

DIDAS TUMAINI

JF-Expert Member
Nov 11, 2014
238
659
Mwamuzi wa ligi kuu ya nchini Uingereza, Jarred Gillett atakuwa mwamuzi wa kwanza wa Premier League kuvaa kamera ya video yenye kichwa wakati wa mchezo kati ya Crystal Palace na Manchester United usiku wa leo.

Pia, Gillett atavaa kifaa kilichowekwa kichwani ambacho kimeunganishwa kwenye mfumo wa kawaida wa mawasiliano ya waamuzi.

'RefCam' Itatumika kama reference kuhusu maamuzi yote yanafanywa, na jinsi maafisa wengine wa mechi wanavyowasiliana na wachezaji. Video hizo hazitarushwa live, lakini zitatumiwa baadaye kama sehemu ya kufanya maamuzi kulingana na taarifa ya mechi kamisaa.

Ligi kuu nchini ujerumani, Bundesliga ndio ligi ya kwanza kutumia kifaa hiki "RefCam" katika moja ya mechi zake msimu huu kati ya Eintracht Frankfurt na VfL Wolfsburg kwa dakika 26 tu za kipindi cha kwanza.
 

Attachments

  • Polish_20240506_155725500.jpg
    Polish_20240506_155725500.jpg
    615.6 KB · Views: 4
Back
Top Bottom