Paul Makonda kuongoza Mapokezi mazito ya Rais Samia siku ya Mei Mosi mkoani Arusha yatakakofanyika kitaifa

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,995
10,484
Ndugu zangu Watanzania,

Arusha imepata bahati na neema ya kipekee kabisa ya kuandaa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani kitaifa ambayo itafanyikia Mkoani hapo jiji na lango kuu la watalii hapa nchini.na katika maadhimisho hayo mgeni Rasmi atakuwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge.

Hii ni bahati kubwa sana kwa wana Arusha na kanda ya kaskazini nzima. Wana Arusha wanakwenda kuvuna pesa katika kila shughuli ya kiuchumi itakayofanywa na wana Arusha, kuanzia watu na vijana wa bodaboda, mama lishe, watu wa hoteli, daladala, bajaji, mabasi, ndege, utalii na biashara nyingine nyingi sana.

Lakini pia Mheshimiwa Mwamba Mwenyewe Makonda anakwenda kupata fursa na bahati ya kipekee tena ndani ya muda mfupi sana ya kuongoza mapokezi mazito sana ya kumpokea Mheshimiwa Rais wetu atakapotua katika ardhi ya Arusha. Hii ni bahati kubwa sana ndugu zangu.

Siyo jambo dogo. Mkuu wa nchi kuwa mkoani mwako kuna faida nyingi sana kwa kiongozi kama mkuu wa mkoa pamoja na mkoa wake, kwa kuwa unapata nafasi ya ana kwa ana ya kumueleza mambo ambayo ungependa aweke mkono wake au baraka pale panapoonekana kuwa kikwazo katika maendeleo ya mkoa.

Inatoa fursa ya kumuomba mambo mbalimbali pamoja na kupata majibu ya haraka na utekelezaji wa haraka.kwa sababu neno moja tu la Rais wa nchi linaweza kufungua mlango wowote ule uliofungwa au kutoa maagizo na yakatekelezwa ndani ya dakika moja kufumba na kufungua.

Lakini pia Dunia nzima pamoja na macho na masikio ya watanzania wote hapa nchini na nje ya nchi, yatakwenda kumsikia na kumtizama Mwamba Mwenyewe Makonda akiunguruma kama simba kutokea kaskazini. Hii ni baada ya kuunguruma siku ya kumbukumbu ya hayati Edward Moringe Sokoine na Kuitetemesha nchi, sasa anakwenda kuiteka nchi kwa mara nyingine tena tarehe hiyo.

Huyu Mwamba ni balaa kwelikweli, ni wa moto hasa, hapoi wala hatulii, ni matata na mtata kwelikweli. Kuna watu hawalali kwasababu ya kumuwaza na kumuogopa huyu Mwamba, kuna watu wanaweweseka kama wagonjwa wakimsikia au kulisikia jina tu. Huyu Mwamba acha kabisa. Sijawahi kuona kijana jasiri kama huyu Mwamba. Anatetemesha utafikiri anamiliki na kuongoza kikosi cha mizinga katika uwanja wa vita iliyokolea.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

IMG-20240206-WA0027.jpg
 
Ndugu zangu Watanzania,

Arusha imepata bahati na neema ya kipekee kabisa ya kuandaa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani kitaifa ambayo itafanyikia Mkoani hapo jiji na lango kuu la watalii hapa nchini.na katika maadhimisho hayo mgeni Rasmi
Aipoanza ilikua kiitikio ni mwanza mwanza versre ya imekwisha chrous ya pili Arusha Arusha kunaniiiiiii!
 
Arusha raha sana mama hakauki kabisa. Sio mbaya mali bila ukaguzi unaeza usuvune.

Arusha isipobadillka utawala huu mtaula wachuya.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Arusha imepata bahati na neema ya kipekee kabisa ya kuandaa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani kitaifa ambayo itafanyikia Mkoani hapo jiji na lango kuu la watalii hapa nchini.na katika maadhimisho hayo mgeni Rasmi atakuwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan mama
Asante sana Lucas kwa taarifa
 
Ndugu zangu Watanzania,

Arusha imepata bahati na neema ya kipekee kabisa ya kuandaa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani kitaifa ambayo itafanyikia Mkoani hapo jiji na lango kuu la watalii hapa nchini.na katika maadhimisho hayo mgeni Rasmi atakuwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge.

Hii ni bahati kubwa sana kwa wana Arusha na kanda ya kaskazini nzima. Wana Arusha wanakwenda kuvuna pesa katika kila shughuli ya kiuchumi itakayofanywa na wana Arusha, kuanzia watu na vijana wa bodaboda, mama lishe, watu wa hoteli, daladala, bajaji, mabasi, ndege, utalii na biashara nyingine nyingi sana.

Lakini pia Mheshimiwa Mwamba Mwenyewe Makonda anakwenda kupata fursa na bahati ya kipekee tena ndani ya muda mfupi sana ya kuongoza mapokezi mazito sana ya kumpokea Mheshimiwa Rais wetu atakapotua katika ardhi ya Arusha. Hii ni bahati kubwa sana hii ndugu zangu.

Siyo jambo dogo. Mkuu wa nchi kuwa mkoani mwako kuna faida nyingi sana kwa kiongozi kama mkuu wa mkoa, kwa kuwa unapata nafasi ya ana kwa ana ya kumueleza mambo ambayo ungependa aweke mkono wake au baraka pale panapoonekana kuwa kikwazo katika maendeleo ya mkoa.

Inatoa fursa ya kumuomba mambo mbalimbali pamoja na kupata majibu ya haraka na utekelezaji wa haraka.kwa sababu neno moja tu la Rais wa nchi linaweza kufungua mlango wowote ule uliofungwa au kutoa maagizo na yakatekelezwa ndani ya dakika moja kufumba na kufungua.

Lakini pia Dunia nzima pamoja na macho na masikio ya watanzania wote hapa nchini na nje ya nchi, yatakwenda kumsikia na kumtizama Mwamba Mwenyewe Makonda akiunguruma kama simba kutokea kaskazini. Hii ni baada ya kuunguruma siku ya kumbukumbu ya hayati Edward Moringe Sokoine na Kuitetemesha nchi, sasa anakwenda kuiteka nchi kwa mara nyingine tena tarehe hiyo.

Huyu Mwamba ni balaa kwelikweli, ni wa moto hasa, hapoi wala hatulii, ni matata kwelikweli. Kuna watu hawalali kwasababu ya kumuwaza na kumuogopa huyu Mwamba, kuna watu wanaweweseka kama wagonjwa wakimsikia au kulisikia jina tu. Huyu Mwamba acha kabisa. Sijawahi kuona kijana jasiri kama huyu Mwamba. Anatetemesha utafikiri anamiliki na kuongoza kikosi cha mizinga katika uwanja wa vita iliyokolea.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

Mapokezi ya majizi ya kura.
 
Ni mkakati mwingine wa kumpa fursa Makonda atukane Mawaziri wa Samia, inapangwa kimkakati sana, mara sijui kukumbuka kifo cha Sokoine, sasa inakuja na Mei Mosi
 
Back
Top Bottom