Braza Kede
JF-Expert Member
- Nov 1, 2012
- 2,005
- 3,903
Haya ni maisha ya kawaida kwa mikoa iliyo mingi hapa Tanzania labda ukiiondoa Dar pekee.
Maisha ya mikoani ni full kufatiliana wajue unafanya nini au unapanga kufanya nini na lengo sio kusaidia bali ni udadisi, umbea na ukuda tu na ikiwezekana wakukwamishe tu.
Ikitokea umekwama basi kwao ni shangwe kubwa licha ya kwamba hawafaidiki kwa lolote!
Ufitini ni maisha ya kila siku. Hawataki unufaike lakini hiyo fursa hata ukiwaachia hawawezi kufaidika nayo.
Ikitokea umetoboa kimaisha basi utahusishwa na skendo zote mbofumbofu hapo mkoani. Mara Ooh huyu asingetoboa bila ulozi (uchawi) au utasikia jamaa lilikuwa lijambawazi hili au usalama wa taifa, mara ooh sijui aliiba tenda jeshini yani ujinga mtupu.
Unahitaji ngozi ngumu sana na pamba za kutosha za masikioni ili uweze kutoboa mikoani.