Mei Mosi: Dkt. Mpango asema Serikali imepokea hoja ya kuboresha kikokotoo kwakuwa wafanyakazi hawaridhishwi na kanuni zake

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,881
12,133
Fuatilia kinachojiri kwenye Maadhimisho ya siku ya Mei Mosi Kitaifa, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha, leo Mei 1, 2024


Maadhimisho haya yamehudhuriwa na Makamu wa Rais, Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Tulia Ackson, Mawaziri pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

KATIBU MKUU TUCTA, HERI MKUNDA
Akizungumza kwenye Sherehe hizo, Katibu Mkuu TUCTA Heri Mkunda amesema maboresho ya mishahara iliyofanyika bado haijakidhi mahitaji ya wafanyakazi, hivyo vinapaswa kuboresha kwani gharama za maisha zimepanda sana.
1000033827.jpg

Amesema wanatambua uwepo wa nyongeza ya 23.3% ya kima cha chini cha mshahara iliyofanyika, lakini inafaa ongezeko hili lizingatie pia wafanyakazi wengine.

Aidha, wafanyakazi wanaolipwa kwa mapato ya ndani ya halmashauri wanalalamika kutokulipwa maslahi yao kwa wakati kwani uwezo wa halmashauri unatofautiana. TUCTA inapendekeza wafanyakazi wote wa halmashauri kulipwa kutoka Serikali kuu ili kuondoa ubaguzi.

Kuhusu kikokotoo, wafanyakazi hawaridhishwi na namna kinavyofanyika na kimeleta malalamiko mingi. TUCTA inashauri kanuni za ukokotoaji mafao ziboreshwe ili kuleta manufaa kwa wafanyakazi.

Mambo mengine aliyozungumza ni kuongezewa likio ya miezi 3 kwa wanawake waliojifungua watoto njiti pamoja na kupitishwa kwa kitita kipya cha bima ya NHIF bila kushirikisha wafanyakazi kupitia vyama vyao hivyo kuzua taharuki. TUCTA inapendekeza wafanyakazi washirikishwe kwenye maboresho haya ya kitita.

DKT. PHILIP MPANGO, MAKAMU WA RAIS
Dkt. Mpango amewapongeza wafanyakazi kwa kazi kubwa wanayofanya.

Changamoto za kitita cha NHIF imezungumziwa pia. Dkt. Mpango amesema hatua za uboreshaji bado zinaendelea na vyama wahusika wote watashirikishwa.

Aidha, Serikali inasisistiza kuwa likizo ya uzazi ni haki ya mfanyakazi hivyo inapaswa kuwa siku 84 kwa mtoto mmoja, siku 100 zaidi ya mtoto mmoja na iwapo mfanyakazi atajifungua mtoto njiti, kipindi cha uangalizi hospitalini hakitahesabiwa kama likizo, na likizo rasmi itahesabika pindi madaktari watakapoona mtoto amemaliza kipindi cha uangalizi maalumu.

Serikali imepokea ushauri wa kuboresha kanuni za uboreshaji wa kikokotoo, hivyo imepokea hoja ya kuboresha kikokotoo kwakuwa wafanyakazi hawaridhishwi na kanuni hizo. Uamuzi wa kubadili ni lazima utazingatia ushauri wa watakwimu bima na vyama vya wafanyakazi kama TUCTA.

Kuhusu nyongeza ya mishahara, Serikali imesema ikiwa hali ya uchumi itaendelea kuimarika kama ilivyo sasa itatoa neno la faraja kwa wafanyakazi muda si mrefu.

====

Pia soma:

Kwanini Rais Samia kakwepa Hoja za Wafanyakazi na kamtuma Makamu wa Rais wakati Rais wa zanzibar yeye amevunja ziara kwa ajili ya Mei Mosi?

Rais Samia hajaonekana kwenye Sherehe za Mei Mosi, yuko wapi?

Tabiri yatakayotokea Mei Mosi 2024 Arusha

Paul Makonda awatengea barabara moja wajasiriamali maalumu kwa ajili ya kufanyia biashara zao siku ya Mei Mosi

Rais Samia mgeni rasmi Mei Mosi mkoani Arusha, maandalizi yafana

Rais Samia naomba ukemee ubaguzi kwenye sherehe za Mei Mosi

Mei Mosi: Upo uhusiano kati ya maslahi Bora na mfanyakazi kuwa na kitambi?

Mei Mosi: Wafanyakazi Zanzibar kuongezewa Tsh. 50,000 kama posho ya nauli
 
Mtoto wangu wa darasa la Saba nimemwambia usiende shuleni Leo,baadhi ya wilaya za Tanzania zimewaambia walimu waendelee kufundisha siku Yao ya wafanyakazi
 
KIKOKOTOO sheria haramu...tupewe fedha zetu zote TUKAFIE MBELE

Kama Dumuzi WAMEDUMULA Mungu anawaona
======

Update

Dakika zina yoyoma KIKOKOTOO Fc 4 sisi bila na hakuna dalili za kuchomoa

Mechi imeisha TUMEDUMULWA tena
 
Hii ni Mei Mosi (Sikukuu ya Wafanyakazi) au Birthday ya Samia - Machawa kumsifu Mtawala..., Kwa kinachoendelea unaweza kudhani ni the latter.....
 
Huyu MC anawatesa sana hawa wafanyakazi, kukimbizana ndo nini
 
Huyu MC anawakejelli wafanyakazi walio kwenye maandamano, anawazlazimisha wakimbie badala ya kutembea.

Namchukulia kama mpumbavu fulani

Screenshot_20240501_101344_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom