Hatimaye jana nimelipwa mshahara wa Machi na Aprili baada ya kufanyiwa ukatili na PEPMIS

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,911
36,754
Daaaaahh, so sad

Mtu unamnyima mshahara kwa miezi 2 ili afe njaa?

Ili afedheheke katika jamii?

Nakiri kuwa kwa upande wangu nilitimiza majukumu yangu ya kila siku na kutokumalizia kipengele kimoja cha mfumo wa PEPMIS ni uzembe wa mwajiri wangu.

Nimepokea pesa nimetumia laki tu zingine nimeweka reserve kama kawaida yangu.

Ingawa nimelipwa lakini siwezi kumshukuru mtu kwa kunilipa, ningekuwa na fedha nyingi ningeacha kazi na kuhama nchi.

Wanasiasa wakigonga madawati tu pale Dodoma wanalipwa millions of money bila kipingamizi.

Sijatetereka kiuchumi ila ratiba zangu zimeparaganika, nimetumia sehemu ya reserve yangu.

Serikali ikiwadharau watumishi wa umma wasidhani wananchi watapata maendeleo.

Mwafrika ni kama maji ukiyazuia huku yatapita kule, ndio maana bongo mtu anapokea mshahara wa laki 5 lakini anadrive Subaru haikati mafuta na service inafanywa kama kawaida, lakini mifumo ya njia za panya imeasisiwa na viongozi wetu.
 
Aiseeeeee pole kwanini wakufungie mshahara wakati ulishatimiza majukumu yako kama ulitimiza basi hukutimiza Kwa wakati mkuu wako wa taasisi ndiye ambaye wakutatua changamoto hata kabla ya kufika Kwa mwajiri kwakuwa mfumo umempa mamlaka pia
 
Hii nchi hao wakuu wa taasisi na vitengo wako busy kupiga madili tu
 
Daaaaahh, so sad !
Mtu unamnyima mshahara kwa miezi 2 ili afe njaa?
Ili afedheheke katika jamii?
Nakiri kuwa kwa upande wangu nilitimiza majukumu yangu ya kila siku na kutokumalizia kipengele kimoja cha mfumo wa PEPMIS ni uzembe wa mwajiri wangu.
Nimepokea pesa nimetumia laki tu zingine nimeweka reserve kama kawaida yangu.
Ingawa nimelipwa lakini siwezi kumshukuru mtu kwa kunilipa, ningekuwa na fedha nyingi ningeacha kazi na kuhama nchi.
Wanasiasa wakigonga madawati tu pale Dodoma wanalipwa millions of money bila kipingamizi.
Sijatetereka kiuchumi ila ratiba zangu zimeparaganika, nimetumia sehemu ya reserve yangu.
Serikali ikiwadharau watumishi wa umma wasidhani wananchi watapata maendeleo.
Mwafrika ni kama maji ukiyazuia huku yatapita kule, ndio maana bongo mtu anapokea mshahara wa laki 5 lakini anadrive Subaru haikati mafuta na service inafanywa kama kawaida, lakini mifumo ya njia za panya imeasisiwa na viongozi wetu.
Pole mkuu.
Iko siku atakuja mtu atasema KAMA HURIDHIKI NA MSHAHARA ACHA KAZI,kuna jamaa ananikonyeza hapa kwamba kati 2016-2021 hayo maneno yalishatamkwa.

Sasa waulize effectiveness ya hiyo pepsi ni kwa kiasi gani kama wanayo majibu.
 
Huo mfumo sio mbaya ila ulipaswa kuja na kufanyiwa kazi taratibu kwa awamu awamu kwamba hatua hii imekamilika kwa wote tunaenda awamu inayofuata mpaka pale kila kitu linakuwa Sawa.
Shida ya nchi yetu ni Kama tunapewa maagizo toka nje ya nchi kwamba Fanyeni hiki kwa siku 90 watumishi wote wa umma wawe wamefanya na kwakua nchi haina namna basi ni kukomaa utekelezaji bila kujali Kama inaumiza watu au lah.
Mtu anaekukatia mshahara yeye mwenyewe hawezi kuishi bila mshahara
 
Mtu anayezuia mshahara wako huyo ni muuaji
 
Back
Top Bottom