DOKEZO ERB na Surveyors Registration Board fuatilieni personnel walioko kwenye miradi ya umma. Wengi hawana sifa na vyeti vya kughushi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kwa muda wa miaka 10 niliokuwa kwenye sekta ya ujenzi, nimegundua kuwa kuna watu wengi hawana sifa za kitaaluma wana vyeti vya kufoji vya ndani na nje ya nchi.

Kwa kuwa bodi za kitaaluma (ERB na nyinginezo) hazifanyi due diligence, watu hao wamekuwa wakitekeleza majukumu kwa nafasi kubwa wakati uwezo wao ni mdogo na hawazingatii Code of Conducts.

Wengine hata form 4 walifeli ila leo wanafanya kazi km maTechnicians, wengine Surveyors kwenye miradi ya ujenzi ya barabara na reli. Na hao ndo wana watrain junior engineers ambapo wao hakuna wanachokijua ni ujanja ujanja tu.

Nawaomba ERB na the like wawe wanatembelea miradi na kukagua vyeti vya watu hao ili kujiridhisha baadala ya kusajiri na kupata ada.
 
Mkuu unaweza kutoa case study? Mtaje huyo mwenye vyeti feki. Hatta PM karibu
 
Back
Top Bottom