Elimu na kujitambua

Mkolosai2020

Member
Aug 11, 2022
22
31
Miaka ya hivi karibuni hususani miaka ya kuanzia 2010 mpaka sasa kumekuwa na utamaduni wa kusifia sana wakuu wa nchi badala ya kuleta hoja zitakazo ibua sifa au kuelezea utendaji kazi halisi wa hawa watawala ama viongozi.

Binafsi nikijaribu kuangalia historia ya nchi yetu (TANZANIA) naona kama miaka ya sasa wasomi ni wengi ukilinganisha na miaka ya 1960s - 1990s.

Kusifia viongozi kuwaabudu na kuwanyenyekea kupita kiasi kumeibuka kwa wingi kipindi ambacho wasomi ni wengi sana ambapo karibia kila familia ama ukoo yupo mmoja aliyesoma chuo kikuu.

Yaani hakuna hoja italetwa bila kuanza na kupongeza fulani. Hata maeneo ambako hawahusiki hususani misibani, makanisani na misikitini lakini wasomi wetu wanasiasa huanza kwa kusifia tu.

Najiuliza maswali haya
1. Wasomi wetu wamejaa ukasuku kwaajili ya kupata teuzi?
2. Elimu ya sasa na zamani kuna tofauti gani hapa katikati ingali vyuo ni vilevile?
3. Kwani kiongozi kutekeleza mradi fulani siyo wajibu wake inakuja kama bahati mpaka apongezwe ndio atapata motisha ya kutekeleza zaidi?
4. Viongozi hawaelewi wajibu wao?
 
Elimu yetu inafundisha watu kua wenye hofu, kuto kujitegemea, nidhamu ya uoga, uchawa, ufisadi pamoja na uongo.
Bila juhudi binafsi, hii elimu ninayo ijua mimi haijawekwa mahsusi kwaajili ya kumkomboa mtoto wa mkulima.
Hii elimu inamkaririsha mtoto kupata majibu ya kufaulu mtihani, wakati badala ingetakiwa imfundishe mtoto aelewe ili akajipime kwa kiwango alicho elewa wakati amefundishwa.
 
Miaka ya hivi karibuni hususani miaka ya kuanzia 2010 mpaka sasa kumekuwa na utamaduni wa kusifia sana wakuu wa nchi badala ya kuleta hoja zitakazo ibua sifa au kuelezea utendaji kazi halisi wa hawa watawala ama viongozi.

Binafsi nikijaribu kuangalia historia ya nchi yetu (TANZANIA) naona kama miaka ya sasa wasomi ni wengi ukilinganisha na miaka ya 1960s - 1990s.

Kusifia viongozi kuwaabudu na kuwanyenyekea kupita kiasi kumeibuka kwa wingi kipindi ambacho wasomi ni wengi sana ambapo karibia kila familia ama ukoo yupo mmoja aliyesoma chuo kikuu.

Yaani hakuna hoja italetwa bila kuanza na kupongeza fulani. Hata maeneo ambako hawahusiki hususani misibani, makanisani na misikitini lakini wasomi wetu wanasiasa huanza kwa kusifia tu.

Najiuliza maswali haya
1. Wasomi wetu wamejaa ukasuku kwaajili ya kupata teuzi?
2. Elimu ya sasa na zamani kuna tofauti gani hapa katikati ingali vyuo ni vilevile?
3. Kwani kiongozi kutekeleza mradi fulani siyo wajibu wake inakuja kama bahati mpaka apongezwe ndio atapata motisha ya kutekeleza zaidi?
4. Viongozi hawaelewi wajibu wao?
uoga wako ndio umaskini wako 🐒

elimu ni kipawa kila mtu amepewa na Mungu, ile elimu ya shuleni ni ya ziada tu 🐒

mwenye elimu kulaumu au kulalamikia wenye elimu wengine ni uvivu, utumwa na utegemezi....
 
Back
Top Bottom