KWELI Msongo wa mawazo husababisha uwaraza

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Hivi karibuni kumezuka sintofahamu kwamba msongo wa mawazo husababisha matatizo ya kupungukiwa na nywele (uwaraza), je ni kweli?

1716244606759.png
 
Tunachokijua
Msongo wa mawazo ni hali ya mtu kuzongwa na mawazo hasi ambayo mara nyingi hupelekea matokeo mabaya Kwa muhusika hasa pale asiposaidiwa au asipojisaidia kutoka kwenye changamoto hiyo.

Kupoteza nywele kunajulikana kama Alopecia. Kupoteza nywele kutoka kwa kichwa au mahali pengine kwenye mwili. Kupoteza nywele ni kawaida kwa wanaume na wanawake, na suala linaloweza kutibiwa. Upotezaji wa nywele hurejelea upotezaji au upotezaji wa nywele kichwani, nyusi, kope, au sehemu zingine za mwili. Inaweza kutokea hatua kwa hatua au ghafla na huathiri watu wa umri na asili zote. Aina ya kawaida ni ya kijeni, inayojulikana kama androgenetic alopecia au upara wa muundo.


Sababu zingine ni pamoja na hali kama vile alopecia areata au trichotillomania, pamoja na maswala ya kiafya kama vile anemia or ugonjwa wa tezi. Kupoteza nywele kunaweza kuathiri kujithamini, lakini matibabu kuanzia marekebisho ya mtindo wa maisha hadi dawa na upasuaji yanapatikana.

Kumekuwa na hoja inayozunguka katika Jamii ikidai kwamba msongo wa mawazo umekuwa ni miongoni mwa vichocheo/ sababu ya watu mbalimbali kupata upara. Hoja inayofanana na hiyo inadai kuwa watu wanaosoma sana wanakumbwa na changamoto ya upara sababu ya kutumia sana akili.

Upi ukweli wa hoja hii?
Katika kutafuta ukweli wa hoja hii JamiiCheck imepitia makala mbalimbali za Taasisi na Wataalamu wa Afya waliofafanua tatizo la upara kwa kina na visababishi vyake. Vyanzo vyote vilivyopitiwa na JamiiCheck vinakubaliana kuwa zaidi ya kuwepo sababu za kijenetiki na kiafya ya watu mbalimbali kupata upara, pia msongo wa mawazo umekuwa miongoni mwa kichocheo cha watu kupoteza nywele zao kichwani.

Mathalani, Hospitali ya Medicover inayochapisha makala mbalimbali za Afya mitandaoni inabainisha sababu saba za mtu kupata upara ambazo ni Urithi, Afya na Homoni, madawa, mionzi, mitindo ya nywele, Matibabu pamoja na msongo wa mawazo. Wakifafanua kwa undani kuhusu namna msongo wa mawazo unavyoweza kusababisha utokeaji wa upara wanasema:

Nyakati ngumu zinaweza kusababisha mtu kupata upara kutokana na kutokea kwa hali inayoitwa telogen effluvium (hali ya kudondoka kwa nywele nyingi sababu ya msongo wa mawazo).
Nao, Este Medical Group hawatofautiani na Hospitali ya Medicover wao pia wanaeleza kuwa Msongo wa mawazo unapelekea kuibuka kwa hali inayoitwa telogen effluvium inayochochea mizizi ya nywele kuathirika na nywele kuanguka. Wakieleza jambo hili wanasema:

Msongo wa mawazo unaweza kuathiri kupoteza nywele, hasa kupitia hali inayoitwa telogen effluvium. Aina hii ya kupoteza nywele hutokea kutokana na msongo wa mawazo kusukuma visukusuku vya nywele kuingia katika awamu ya kulala, na hivyo kusababisha kuanguka kwa nywele au kuathiri afya ya nywele.
Kwa upande wao Mayo Clinic wanaeleza kwa kina zaidi hali za msongo wa mawazo na namna zinavyoweza kusababisha mtu apoteze nywele na baadaye kupata kipara. wakifafanua zaidi hali hizi wanasema:

Kuna aina mbalimbali za upotevu wa nywele unaoweza kusababishwa na msongo wa mawazo, zikiwemo:​
Telogen Effluvium: Hii ni hali ambapo msongo wa mawazo wa kiwango cha juu unaweza kusababisha nywele nyingi zaidi kuingia katika awamu ya kupumzika (telogen phase). Baada ya muda (kawaida miezi michache), nywele hizi huanza kudondoka kwa wingi. Ingawa hali hii si mara zote husababisha kipara cha kudumu, inaweza kusababisha kupungua kwa nywele kwa muda fulani.​

1716329818667-png.2996387

Telogen Effluvium

Alopecia Areata: Hii ni hali ya kiafya ambapo mfumo wa kinga ya mwili hushambulia visukusuku vya nywele, na kusababisha vipara vidogo vidogo. Msongo wa mawazo unaweza kuwa moja ya vichochezi vya hali hii, ingawa si sababu pekee.​
1716330061383-png.2996391

Alopecia areata
Trichotillomania (kujinyofoa nywele): Hii ni shida ya kisaikolojia ambapo mtu anashindwa kujizuia kung'oa nywele zake mwenyewe kutokana na msongo wa mawazo au hisia za dhiki. Matokeo yake yanaweza kuwa vipara na uharibifu wa visukusuku vya nywele.​
1716330365020-png.2996392
Trichotillomania

Wataalamu wanafafanua kuwa ni muhimu kutambua kwamba ingawa msongo wa mawazo unaweza kuwa na athari kubwa kwenye ukuaji wa nywele, mara nyingi hali hizi zinaweza kudhibitiwa na kubadilishwa. Kupunguza msongo wa mawazo kupitia mbinu kama vile mazoezi, kupumzika, tiba ya kisaikolojia, na lishe bora inaweza kusaidia kuimarisha afya ya nywele na kupunguza hatari ya kupoteza nywele.
Mimi nadhani hizo ni genetics baba mwenye uwaraza mara nyingi kijana wake anakuja kuwa na uwaraza, na unautambua kuangalia nywele zilipoanzia hapo wenye makomwe wengi Wana hatari ya kupata uwaraza😂 all in all Kuna watu mashuhuri wenye Ankara na walikuwa na uwalaza
 
Mimi nadhani hizo ni genetics baba mwenye uwaraza mara nyingi kijana wake anakuja kuwa na uwaraza, na unautambua kuangalia nywele zilipoanzia hapo wenye makomwe wengi Wana hatari ya kupata uwaraza😂 all in all Kuna watu mashuhuri wenye Ankara na walikuwa na uwalaza
Hhhhh
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom