Hali ya Uchumi Tanzania: Kutumia utalii ili kuleta manufaa makubwa zaidi

Hali ya Uchumi Tanzania: Kutumia utalii ili kuleta manufaa makubwa zaidi

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,247
Reaction score
5,731
Wadau wa JamiiForums,

Benki ya dunia kwa mara nyingine imetoa ripoti ya 'Tanzania Economic Update' ikilenga utalii kwa namna ipi inaweza kuleta mafanikio kwa Tanzania na Watanzania. Ripoti hiyo imeanisha mengi kuhusiana na Sekta ya Utalii. Baadhi machache ni;

  • Tanzania imeajiri karibu watu laki tano katika sekta ya utalii
  • Watanzania karibu millioni mbili maisha yao yanategemea sekta ya Utalii
  • Ripoti inaibua swali endapo kuna uhusiano kati ya ukuaji wa Uchumi katika kuongeza kazi kwa vijana
  • Wananchi wana matumaini (as per conducted survey) kuwa itafika wakati Uchumi wa Tanzania utaimarika Tanzania
  • Sekta ya utalii inalenga kuzidisha mara nane mapato yake ifikapo mwaka 2025
  • Utalii tayari huleta manufaa makubwa kwa uchumi wa Tanzania na ungeweza kuleta manufaa makubwa zaidi katika siku zijazo iwapo utasimamiwa ipasavyo.
  • Wadau wengi wa Maendeleo wamechelewesha kutoa fedha kwa ajili ya kusaidia bajeti kwa sababu wanasubiri ufafanuzi kuhusu kadhia yenye utata ya IPTL
======================

Ujumbe Muhimu toka kwenye ripoti "Unloacking the Potential of the Tourism Industry for Tanzanians"


Kwa wapenzi wengi wa Ligi ya Mpira wa Miguu ya Uingereza, vivutio vya kitalii vya Tanzania vyenye hadhi ya kimataifa vinafahamika vyema. Mlima Kilimanjaro, nyumbu wanaohama kwa makundi kutoka Serengeti kwenda Masai Mara na kurudi, fukwe mwanana za Zanzibar, vyote hivi vimetangazwa wakati wa michezo zaidi ya 100 kwenye viwanja mbalimbali vya Uingereza.

Tanzania ilivutia zaidi ya watalii milioni moja mwaka 2013. Aina ya watalii wenye uwezo wa kifedha ambao sasa hivi Tanzania huwavutia wako tayari kulipa kiasi kikubwa cha fedha ili kutembelea vivutio vyake vya kipekee, hivyo kulipa fedha za kigeni katika nchi ambayo takribani theluthi moja ya watu wake bado wanaishi chini ya mstari wa taifa wa umasikini. Ijapokuwa sekta ya utalii nchini Tanzania imekua kwa haraka katika muongo mmoja uliopita, ingeweza kutumika kuleta manufaa makubwa zaidi kwa idadi kubwa ya Watanzania.

Kama ilivyo kwa matoleo yaliyopita, toleo hili la sita la hali ya uchumi lina sehemu mbili. Sehemu ya kwanza inatoa tathmini ya hali ya sasa ya uchumi wa Tanzania pamoja na matarajio yake ya muda mfupi na wa kati, wakati sehemu ya pili inajikita katika jinsi watunga sera wanavyoweza kupata manufaa makubwa zaidi kutokana na utalii.

Hali ya Uchumi wa Tanzania
Mtazamo wa kawaida wa uchumi wa Tanzania umekosolewa baada ya kufanyika kwa tathmini mpya hivi karibuni ya mahesabu ya taifa na matokeo ya utafiti wa bajeti ya kaya kwa mwaka 2012. Kwa misingi ya tathmini mpya, Tanzania inaonekana kukaribia kufikia hadhi ya nchi ya kipato cha kati, ambapo wastani wa kipato cha mtu ni takribani Dola za Marekani 1000. Pia inaonyesha wazi kwamba ukuaji wa uchumi umewafika hadi kwa watu masikini, wakiwemo walio masikini sana. Hii ni habari njema kwa uchumi wa Tanzania na matarajio yake kwa ukuaji unaozingatia usawa.

Hata hivyo, maendeleo haya yanahitaji maelezo ya ziada. Takribani asilimia 40 ya Watanzania watu wazima wana kipato cha chini ya Dola za Marekani 1.25 kwa siku, wakati Watanzania 9 kati ya 10 wana kipato cha chini ya Dola za Marekani 3 kwa siku.

Uchambuzi wa hivi karibuni wa ukuaji uchumi wa Tanzania haujaathirika kwa kiwango kikubwa na takwimu hizi mpya zilizoboreshwa. Kiwango cha ukuaji uchumi kimekuwa hakiendi mbali na asilimia saba, ijapokuwa kasi ya ukuaji imekuwa ikibadilika mara kwa mara kuliko ilivyokokotolewa hapo mwanzoni. Kiwango cha mfumuko wa bei kwa mwaka uko kati ya asilimia 5 na 6, wakati urari wa malipo kwa ujumla haujabadilika.

Udhaifu wa usimamizi wa uchumi mkuu wa Tanzania unabaki kuwa sera yake ya fedha. Wakati nakisi ya fedha kwa ujumla imepungua kwa kiasi kikubwa katika mwaka 2013/14, kutoka asilimia 5 (kwa tathmini mpya) ya Pato Ghafi la Taifa (GDP) hadi asilimia 3.4, kupungua huko kulifikiwa kwa gharama kubwa. Hii iliwezekana tu kupitia malimbikizo makubwa ya madeni ya makandarasi na mifuko ya pensheni.

Thamani ya madeni haya kwa sasa yamefikia viwango vya kutisha. Kupungua huko pia kulipatikana kwa kupunguza matumizi ya umma katika sekta za kipaumbele, matokeo yake ni kwamba ile programu iliyotangazwa sana ya ‘Matokeo Makubwa Sasa" ilipata rasilimali chache kuliko ilivyokuwa mwaka 2012/13. Vivyo hivyo, matumizi ya maendeleo yalipungua kwa asilimia 1.2 ya GDP. Thamani ya jumla ya fedha iliyotumwa kwa serikali za mitaa pia ilipungua, na kuhatarisha utoaji wa huduma za elimu na afya. Mwenendo huu hasi katika bajeti unadhoofisha mipango mikubwa ya Serikali ya kutoa huduma nzuri za miundombinu na za kijamii kwa idadi ya watu inayokua kwa kasi.

Marekebisho makubwa katika viwango na maudhui ya matumizi katika kipindi cha mwaka 2013/14 kwa sehemu kubwa yalitokana na kiwango cha chini cha makusanyo ya ndani. Sio tu kwamba malengo ya mapato hayakufikiwa kwa kiwango kikubwa, lakini pia utendaji, kwa maana ya ukusanyaji wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) umekuwa mbaya sana, mapato hayo yakilingana na thamani ya asilimia 3 tu ya Pato Ghafi la Taifa (GDP) katika mwaka 2013/14. Uwiano huu ni moja ya viwango vya chini zaidi duniani, mbaya kuliko Madagascar na mbaya zaidi ya kiwango kilichofikiwa na Burkina Faso na Msumbiji, nchi ambazo pia ni masikini na zenye chumi zinazotegemea zaidi kilimo.

Shinikizo la fedha limeendelea kuongezeka kuanzia mwanzoni mwa mwaka wa fedha 2014/15. Mwaka huu tena malengo ya mapato hayakufikiwa, kwa asilimia 10 katika robo ya kwanza, wakati thamani ya madeni kwenye mifuko ya pensheni imeendelea kuongezeka, na kusababisha mmoja kati mifuko mikubwa kukaribia kufilisika. Aidha, Wadau wengi wa Maendeleo wamechelewesha kutoa fedha kwa ajili ya kusaidia bajeti kwa sababu wanasubiri ufafanuzi kuhusu kadhia yenye utata ya IPTL, ambayo inaweza kuwahusisha baadhi ya viongozi wa juu wa serikali kufanya makosa.

Mwitikio wa Serikali kwa matukio haya hasi ni kwa kudhibiti baadhi ya matumizi yake na kuongeza kiwango cha kukopa kutoka soko la ndani. Serikali pia imeanza kupanga mipango ya kulipa madeni yake kwa mifuko ya pensheni na makandarasi wakati matokeo ya uchunguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali katika sakata la IPTL na mapendekezo ya Bunge pia yanafanyiwa kazi. Serikali pia itoe kipaumbele kwa utekelezaji wa haraka wa Sheria mpya ya VAT. Kwa kifupi, inaonekana mamlaka imetambua haja ya kudhibiti hali ya kifedha wakati gurudumu la kisiasa linaongeza kasi. Kura ya maoni imepangwa kufanyika Aprili mwaka huu, wakati uchaguzi mkuu utafanyika mwezi Oktoba.

Matarajio ya muda mfupi na wa kati yanabakia chanya kwa uchumi wa Tanzania. Ukuaji wa Pato Ghafi la Taifa (GDP) unatabiriwa kubakia asilimia saba, wakati kiwango cha mfumuko wa bei na urari wa malipo utabakia katika viwango vyake vya sasa. Hata hivyo, mfumuko wa bei na akaunti za nje huathirika kwa urahisi na kuyumba kwa bei za bidhaa za kimataifa, hususani bei za chakula, dhahabu na nishati.

Utabiri huu chanya unachukulia kwamba hali ya kifedha itabaki ikiwa imedhibitiwa, nakisi ya fedha ya jumla ikiendelea kuwa sawa na takribani asilimia tatu ya GDP katika miaka michache ijayo. Hii itahitaji juhudi kubwa ili kuboresha makusanyo ya mapato, hususani iwapo mamlaka zitataka kutekeleza programu zao za uwekezaji wa umma, ambalo ni jambo linalofanyika kwa nia ya kuleta maendeleo na ni muhimu. Mamlaka pia zitahitaji kupanua wigo wa fedha wa kutosha ili kulipa na kuzuia madeni mapya, na kuzuia kujikopesha katika masoko ya ndani na ya kimataifa.

Kuna uwezekano wa faida kwa utabiri huu kwa maana kwamba nchi inaweza kutumia kwa kiwango cha juu fursa ilizo nazo. Tanzania imejaaliwa kuwa na maliasili za kila aina, rasilimali hizo zinajumuisha gesi asilia, madini, udongo wenye rutuba na wanyama pori wengi. Kwa kutumia rasilimali hizi, Tanzania iko katika nafasi nzuri ya kuweza kupenya katika masoko ya kanda na kimataifa.

Aidha, Tanzania ina fursa nzuri katika utalii, ambao unaweza kutumika kuongeza nguvu ili kuharakisha ukuaji uchumi, kuongeza mapato ya fedha na mapato ya ziada ya fedha za kigeni. Hii ni sekta ambayo sio tu inakua kwa haraka duniani, lakini pia inahitaji nguvu kazi nyingi hivyo kuwa na uwezo wa kutengeneza idadi kubwa ya ajira. Matokeo yake ni kwamba maendeleo ya sekta ya utalii yako juu katika ajenda ya Rais pia na Baraza la Taifa la Biashara.

Kutumia utalii ili kuleta manufaa makubwa zaidi

Utalii tayari huleta manufaa makubwa kwa uchumi wa Tanzania na ungeweza kuleta manufaa makubwa zaidi katika siku zijazo iwapo utasimamiwa ipasavyo. Sekta hii imepanuka kwa haraka katika miaka ya hivi karibuni, ikivutia idadi inayoongezeka ya wageni kila mwaka. Kwa sasa inaajiri takribani watu nusu milioni na ni chanzo muhimu sana cha fedha za kigeni.

Licha ya faida ambazo tayari zinatokana na sekta hii, Watanzania walio wengi bado hawajafaidika kadri iwezekanavyo. Kwanza, wakati watalii wengi wako tayari kutumia kiasi kikubwa cha fedha kutembelea Tanzania, sehemu ya matumizi haya yanabakia huko huko ng'ambo. Hili ni jambo la kutarajiwa, na Tanzania haina tofauti na nchi nyingine, kwani watalii wengi ni watu wa mataifa ya nje na huandaa safari zao kupitia taratibu zilizotayarishwa kabla.

Pili, karibu shughuli zote za kitalii zimejikita katika maeneo mawili - kanda ya kaskazini kuzunguka Arusha na kisiwa cha Zanzibar – ambayo inaelezea kwa nini sehemu nyingine za nchi hazijaunganishwa.

Tatu, hata katika maeneo ambayo yanatembelewa sana, umasikini umekithiri, hususani karibu ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, ikiashiria kwamba bado mahusiano na wana jamii wa maeneo hayo hayajanzishwa.

Nne, wakati sekta ya utalii ikipanuka kwa kasi, bado haijatengeneza kazi zenye tija za kutosha kwa wananchi katika miaka ya karibuni, iwe ni za moja kwa moja au kupitia njia nyingine. Mwisho, mfumo wa kodi usiotabirika na usioeleweka umekatisha tamaa wawekezaji, wakati taratibu zisizo wazi za mgawo wa mapato umefanya kuwa vigumu kufuatilia matumizi ya mapato yanayokusanywa kutoka kwenye sekta ya utalii.

Masuala yote haya yanaelezea kwa nini kutayarisha mkakati mpya wa utalii kwa Tanzania ili kuleta manufaa makubwa zaidi katika sekta ambayo tayari ina mchango mkubwa katika uchumi ni muhimu. Hili ni jambo ambalo kwa sehemu kubwa limekubalika, na majadiliano ya kina baina ya wadau tayari yanafanyika. Wadau wanaonekana kukubaliana kwamba ni muhimu kufanikisha malengo makuu mawili: (i) ongezeko la idadi ya watalii wanaotembelea nchi; na (ii) juhudi za makusudi kuelekeza shughuli za utalii kusini mwa nchi. Ijapokuwa malengo haya kimsingi ni mazuri, mafanikio yake yanahitaji kusimamiwa kwa uangalifu iwapo yatatakiwa kuleta matokeo chanya badala ya hasi.

Sekta ya utalii inalenga kuzidisha mara nane mapato yake ifikapo mwaka 2025. Lengo hili lina maana kwamba Tanzania itapokea idadi sawa ya watalii ambao sasa hivi Moroko na Afrika Kusini wanapokea. Ili kufanikisha lengo hili, itakuwa ni lazima kufikia kiwango cha ongezeko la takribani asilimia 20 kila mwaka, karibu mara mbili ya kiwango cha sasa cha kukua. Ijapokuwa kinafikika, kufanikisha lengo hili kunahitaji uwekezaji wa kutosha katika miundombinu, kutolewa kwa msaada kwa sekta binafsi, na kuendeleza rasilimali watu katika maeneo mbalimbali ya kijiografia.

Kwa sababu rasilimali za umma ni finyu na zitaendelea kuwa hivyo, Serikali lazima ifikirie njia bora zaidi ya kuvutia uwekezaji binafsi na kuchukua hatua za kutengeneza mazingira yanayofaa zaidi ya kufanya biashara. Njia bora zaidi ya kufikia hapa ni kwa kuanzisha ubia wa kimkakati na kupitia kuanzishwa kwa miradi inayojitegemea yenyewe, kama nchi nyingine zilivyofanya.

Iwapo litafanikiwa, lengo la kuvutia idadi kubwa zaidi ya watalii kuja Tanzania, ijapokuwa ni jambo jema lakini hii itasababisha kuwepo kwa athari ambazo lazima tukubaliane nazo na itatulazimu kuzisimamia vyema. Ongezeko kubwa la wageni litasababisha onegezeko la shinikizo katika maliasili zetu ambazo ndizo zinazobeba utalii wa nchi. Tayari, ujangili usiodhibitiwa umesababisha kupungua kwa idadi ya tembo na faru katika maeneo mengi. Kama asemavyo mfanya biashara mmoja wa utalii, kwa kifupi na kwa masikitiko: "Hakuna tembo, hakuna utalii." Pia kutakuwa na ushindani mkubwa kwa rasilimali maji, na uwezekano wa kutokea migogoro ya maslahi baina ya wakulima, shughuli za kuzalisha umeme na mifumo ya ekolojia asilia.

Kupanua kanda za utalii kuelekea Kusini kutahusisha kuendeleza bidhaa mpya za utalii katika maeneo kama vile Pori Tengefu la Selous, Hifadhi ya Taifa ya Ruaha au fukwe katika pwani ya kusini. Hata hivyo, wakati haja ya kupanuka kuelekea maeneo mengine imetambuliwa na kujadiliwa kwa muda mrefu, ni kama hakuna kitu kilichonyika. Bado kuna wageni takribani 20,000 kwa mwaka wanaoenda Ruaha, asilimia kumi tu ya idadi ya wanaotembelea Hifadhi ya Serengeti. Sababu za kutokuwepo maendeleo ni pamoja na kukosekana kwa miundombinu, vikwazo vikubwa kwa uwekezaji binafsi, uhaba wa rasilimali watu inayohitajika, na kukosekana kwa mkakati wa kutangaza vivutio vya utalii zaidi ya kupanda Mlima Kilimanjarpo, kuangalia nyumbu wanaohama na kurudi katika Serengeti, au kufurahia fukwe za Zanzibar.

Wakati kuongeza mapato yatokanayo na utalii na kupanua wigo wa vivutio vinavyotolewa kwa watalii ni kiini cha mkakati wowote wa kuendeleza utalii nchini Tanzania, kuna haja ya watunga sera na watendaji wa sekta kufikiria nje ya mfumo tuliouzoea na kufanya mambo kwa ubunifu. Hii itahitaji watunga sera kuridhia hatua chini ya nguzo tatu tofauti.

Nguzo ya kwanza inahusu upanuzi kuingia maeneo mapya. Hata hivyo, upanuzi huu usiwe wa upande mmoja. Lazima ihusishe sio tu upanuzi kwa misingi ya kijiografia; pia itahusisha kukidhi mahitaji ya sehemu tofauti za soko la utalii kwa kuanzisha shughuli mpya ambazo zinakidhi mahitaji ya wigo mpana wa watalii. Hadi sasa, msisitizo umekuwa katika kukidhi mahitaji ya watalii wenye uwezo wa kifedhai ambao wanaweza kulipa Dola za Marekani elfu kadhaa kwa ajili ya kuona wanyama wakati wanakaa katika hoteli za kifahari. Aina nyingine za utalii ziendelezwe, ikijumuisha shughuli za ufukweni ili kukidhi mahitaji ya watalii wenye bajeti za chini na kati. Miundo ya aina hizi za utalii ambayo inakidhi masoko haya tayari imeanza kuibuka kisiwani Zanzibar, ambayo hutoa malazi rahisi na ndege za kukodi, hivyo kufanya maeneo ya vivutio kufikika kwa urahisi kwa wigo mpana wa watalii, ikijumuisha wageni kutoka ndani ya nchi na katika kanda, na kukuza mahusiano na biashara za wenyeji na wafanyakazi.

Aina nyingine za utalii ambazo zinaweza kupanuliwa ni pamoja na utalii wa kibiashara katiika majiji ya Dar es Salaam na Arusha, utalii wa kitamaduni katika maeneo kama vile magofu ya Kilwa, na kutembea katika milima ya Usambara na Udzungwa. Mchanganyiko wa aina zote hizi za utalii pia unawezekana kupitia taratibu maalum ambazo zinawawezesha watalii kukaa kwa muda mrefu zaidi na kutawanya faida za kiuchumi.

Nguzo ya pili inahusu muunganisho wa shughuli za utalii katika maeneo yaliyopo. Ni jambo lililo wazi kwamba sekta ya utalii hadi sasa haijaweza kutengeneza ajira za kutosha za thamani kubwa na zenye tija kwa wananchi, pia haijawezesha maendeleo ya mahusiano ya pande zote na wadau wa nchini kwa kadri inavyowezekana. Kwa mfano, mfanyakazi wa kawaida mwenyeji wa Tanzania kwa wastani anaingiza kipato ambacho ni theluthi moja ya mwenzake nchini Kenya. Hoteli nyingi zinategemea vifaa, zana na chakula vinavyoagizwa kutoka nje.

Hivyo sera shirikishi zinahitajika ili kushughulikia maeneo haya mawili. Misaada mingine ya ziada inahitajika kwa jamii za wenyeji kwa kuwahusisha wananchi wa jamii hizi katika usimamizi wa hifadhi, na kwa kutumia mapato yanayotokana na shughuli za utalii kujenga miundombinu ya eneo husika; kwa kusaidia miradi ya biashara ya wenyeji na kwa kutoa fedha moja kwa moja kwenye uhawilishaji wa fedha.

Nguzo ya tatu inahusu hatua za kuboresha utawala bora. Hususani hii itahusisha utekelezaji wa mfumo unaotoa haki kwa wote na ulio rafiki kibiashara, na utayarishaji wa taratibu za wazi za kugawana mapato. Juhudi zinahitajika sana kutayarisha vipengele hivi vya mfumo wa utawala kwani sekta ya utalii kwa sasa inakwazwa na utozaji wa kodi na ada nyingi ambazo hukatisha tamaa wawekezaji, hasa wawekezaji wadogo, na kuongeza fursa kwa kampuni zinazonyonya nchi bila ya kunufaisha jamii pamoja na rushwa. Ushuru mwingi ambao hauna tija unaweza kuondolewa au kurasimishwa na hivyo kuongeza ushindani wa sekta.

Ni vigumu kuamini, kwamba licha ya kodi zote hizo, kiwango cha ukwepaji kodi kinaonekana ni kikubwa katika mchango wa jumla wa sekta ya utalii kwa mapato ya ndani, ukiwa ni theluthi ya ule wa sekta ya madini, licha ya kwamba utalii huchangia sehemu kubwa zaidi ya Pato Ghafi la Taifa (GDP). Ili iweze kuinua viwango vyake vya ukusanyaji wa mapato, Serikali inapaswa kuweka mkazo katika kuboresha viwango vya makusanyo katika sekta hii, kuweka vikwazo dhidi ya wakwepa kodi pale ambapo ni lazima. Motisha za kodi zenye nafuu kwa wawekezaji pia zipunguzwe, ukichukulia kwamba matokeo yake ni ya kutia shaka sana. Serikali iandae mkakati utakaolenga katika kurahisisha mfumo uliopo, kwani ni utata wa mfumo uliopo ndio lalamiko kuu la waendesha biashara ya utalii na vyama vyao. Aidha, Serikali ichukue hatua ya kupanua wigo wa kodi. Serikali ilenge kufanya haya kupitia ushirikiano kuliko mapambano na sekta binafsi.

Ili kuhakikisha utawala bora, ni muhimu kuhakikisha kwamba sekta ya utalii inatumika katika njia yenye ufanisi na uwazi. Kwa mazingira ya sasa, kufuatilia mgawo wa mapato haya ni kama haiwezekani kwa sababu ya sheria ngumu zinazotumika kutofautisha mapato haya. Kwa mfano, mapato kutoka kwenye uwindaji kinadharia hutumwa Hazina, Wizara ya Maliasili na Utalii, na serikali za mitaa, ripoti ya hivi karibuni ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali haikuweza kuhakiki iwapo fedha hizo zilipelekwa kwa taasisi lengwa. Huu si mkasa wa kipekee, wakati masuala yanayofanana mara kwa mara hutokea sehemu nyingine kutokana na idadi kubwa ya mawakala wanaojihusisha na ukusanyaji wa kodi na ada.

Nadharia ya uchumi inapendekeza uwezekano wa njia mbili zinazoshamirishana: (i) inaweza kuwa na taratibu ya sehemu moja kuu ya kufanya makusanyo na kutumia vigezo vya wazi vya mgawo kupitia taratibu za bajeti pale ambapo walengwa ni wengi na anuwai; na/au (ii) inaweza kugatua taratibu za makusanyo kwa serikali za mitaa pale ambapo walengwa wanatoka eneo hilo (kanuni ya kisaidizi).

Kuzingatia kanuni tatu za upanuzi katika maeneo anuwai, muunganisho na utawala bora kutawezesha Tanzania kupata manufaa mengi zaidi kutoka kwenye rasilimali na vivutio vyake vya utalii. Iwapo Tanzania inataka kupata manufaa makubwa kutokana na sekta hii, lazima iweke msisitizo sio tu katika hatua za kuongeza idadi ya watalii, lakini pia katika kuhakikisha kwamba sekta inaleta manufaa kwa sehemu kubwa ya wananchi na kwamba wanyamapori, utamaduni na maliasili vinalindwa ili faida hizi ziwe endelevu.
 
Binafsi napinga Ripoti kwa kiasi kikubwa sana, na nasema Tanzania hahiitaji kutoa Kipaumbele cha kwanza kwenye utalii, bali KIPAUMBELE CHA KWANZA kiwe kwenye Rasilimali zetu!

Tuwekeze kwenye Madini kama Nickel yetu, Uranium, Dhahabu, Shaba, Bauxite, Chuma, Makaa ya Mawe na kwenye Gesi yetu hapo ndipo pa kuhakikisha piga uwa tunatoboa, haya mambo ya Utalii ni ya ziada tu lkn UCHUMI hasa uko kwenye Rasilimali zetu!
 
This is good news. That said, we still should aim higher. When China grows at 7% we say it is underperforming, so why should we praise African countries, including Tanzania, for growing at that rate?

Tanzania should focus on infrastructure (roads, rails, ports, electricity and water). With proper infrastructure, all other sectors will grow exponentially, tourism included. It is a shame that we rely on Kenyan airports to source our tourist to this date, 53 years on!
 
The momentum from tourism is about right. There aren't that many unexplored places with such great eco-system as Tanzania.

Ministry of Torurism should get on with technology and make sure the Twitter Generation keeps Tanzania in their bucket list as they grow up.

Currently every American wants to Visit Europe, Every Asia wants to visit the US,and Every European want to visit Asia. we should get into that loop and make sure we have mind-share potential tourist before they even visit.

One of the way that we have completely under utilized is placement in popular Hollywood Sitcoms and Movies. Zanzibar should be That honeymoon place, Serengeti should be that virgin land the hero explorer visits. These things have more mileage than a generic ad in a poster no one cares to take a look at.

I applaud the Premier league advertisements as in something is better than nothing, but stadium advertisements are not as effective me thinks as fewer eyeballs, care about them as when its part of the narrative.

I just remember once I saw in Scandal where the main character (Olivia Pope) went to Zanzibar as a place to completely relax and not be found. This was a good steed, i wonder if TTB ever saw that episode, or even care that millions of Americans and people around the world watch these shows.

We should be part of the narrative, part of the lifestyle, that will give us a better milestone.
 
Nitoe pongezi kwa Benki ya Dunia kwa kuaandaa taarifa hii. Pamoja na yote yaliyosemwa, nafikiri ili sekta ya utalii iweze kukua kwa kiwango kinachotarajiwa, mambo yafuatayo pia yanapaswa kuzingatiwa:

1. Wizara ya Maliasili na Utalii na taasisi zake [Idara ya Utalii, Idara ya Wanyamapori, TTB, TANAPA] ndio wahusika wakuu wa kuweka sera nzuri, mipango na mikakati ya kuendeleza utalii hapa nchini kwa kushirikiana na wadau wengine. Lakini niseme kuwa uwezo wa taasisi hizi kwa maana ya uwezo wa watu tulionao kwenye hizi taasisi ni wa wastani na hauwezi kuleta mapinduzi yanayotakiwa kwenye sekta ya utalii. Kuna umuhimu mkubwa sana wa kuhakikisha kuwa tunakuwa na watu wenye uwezo thabiti katika taasisi zinazosimamia sekta ya utalii ili kuhakikisha kuwa tuna sera, mikakati na mipango mizuri ya kuendeleza utalii. Ukitizama uwindaji wa kitalii, kwa mfano, ni ubabaishaji mtupu. Hakuna innovations na shughuli nzima imegubikwa na vested interests.

Umezungumzia matangazo kwenye mechi za mpira wa miguu katika ligi ya Uingereza. Je matangazo hayo yamekuwa na impact gani? Can anyone clearly show the impact of those adverts on number of arrivals? In other words, what will happen if we do not advertise on premier league matches? Au tunafanya kwa mazoea tu? Au ni miradi ya watu ya kula pesa?

2. Decentralize as much as possible the ownership and management of tourist attractions, including wildlife. Kufanya hivyo kutapelekea wananchi kunufaika moja kwa moja na kuona thamani ya kulinda na kuhifadhi raslimali zetu. The idea I have in mind is community-based tourism, which has been successful in other places like Namibia.

3. The quality of tour guides and other service providers is essential. Kwa sasa, ubora wa waongoza watalii ni mdogo. Hali hii inaathiri sana experience ya mtalii na inawafanya baadhi kukata tamaa ya kutembelea tena Tanzania. Baadhi ya makampuni yanayotoa huduma kwa watalii si waaminifu. Nimeshuhudia matukio ambayo mtalii anafika airport hapa Tanzania na hakuna wa kumpokea kama alivyoahidiwa wakati malipo ya ziara nzima au sehemu kubwa ya malipo alishayafanya. Kuwe na utaratibu mathubuti wa ku certify tour guides pamoja na watoa huduma wengine kwenye Sekta ya Utalii.
 
World Bank nao ni wa ajabu wanachagua hiyo sekta wakijua kabisa kuwa hatuna cha kufanya zaidi ya kutegemea watu wa nje na vyombo vya nje kuijenga. Pindi "wakikasirika" tunaanguka na tusiweze kuinuka.

Basi tuanze wenyewe siyo kwa kujenga viwanja vya ndege bali kuunda shirika letu la ndege litakalowaleta hao watalii. Ebu jaribu kuwaambia WB watoe msaada au hata tu mkopo wa kuimarisha shirika letu la ndege usikie majibu yao. Watasema hiki siyo kipaumbele...

Bahati mbaya pia watalii tunaowalenga ni wale wale ambao "wakikasirika"wanatengeneza tishio la usalama na kulitangaza na wala haichukui muda unaanguka! Waulize Kenya watakuambia.
 
World Bank nao ni wa ajabu wanachagua hiyo sekta walijua kabisa kuwa hatuna cha kufanya zaidi ya kutegemea watu wa nje n vyombo vya nje kujenga. Pindi "wakikasirika" tunaanguka na Tusiwe kuinuka.

Basi tuanze wenyewe siyo kwa kujenga viwanja vya ndege bali kuunda shirika letu la ndege litakalowaleta hao watalii. Ebu waambIe WB watoe msaada au hata tu mkopo wa kuimarisha shirika letu la ndege us ikielekezwa majibu yao. Watasema hiki siyo kipaumbele...

Bahati mbaya pia watalii tunaowalenga ni wale wale ambao "wakikasirika"wanatengeneza tishio la usalama na kulitangaza na wala haichukui muda unaanguka! Waulize Kenya wanakuambia.


Too much negativity here.

Nitakuwekea picha moja itaniepusha kuandika maneno mengi.

TTB should think outside the box.

CK6aONG.jpg
 
Binafsi napinga Ripoti kwa kiasi kikubwa sana, na nasema Tanzania hahiitaji kutoa Kipaumbele cha kwanza kwenye utalii, bali KIPAUMBELE CHA KWANZA kiwe kwenye Rasilimali zetu!

Tuwekeze kwenye Madini kama Nickel yetu, Uranium, Dhahabu, Shaba, Bauxite, Chuma, Makaa ya Mawe na kwenye Gesi yetu hapo ndipo pa kuhakikisha piga uwa tunatoboa, haya mambo ya Utalii ni ya ziada tu lkn UCHUMI hasa uko kwenye Rasilimali zetu!
Ndugu hayo mambo uliyoyataja hapo yanaitwa 'primary exports'......ni vibaya economically kwa nchi kutegemea primary exports kwa maendeleo yake.....sababu zake ni nyingi ikiwemo price flactuations n.k.
 
Ndugu hayo mambo uliyoyataja hapo yanaitwa 'primary exports'......ni vibaya economically kwa nchi kutegemea primary exports kwa maendeleo yake.....sababu zake ni nyingi ikiwemo price flactuations n.k.

HAPANA! Lazima ujue ya kwamba Utalii ni uwekazaji wenye Gharama sana na nchi kama ni masikini na haina miundombinu Imara ni ngumu sana kuweza kufaidika na Utalii!

Nitakupa mfano mdogo sana chukulia Ml.Kili Mtalii anapanda at his/her own risk kama akizimia huko juu atashushwa na machela mpaka chini na hapo utampeleka Hospitali gani? KCMC au mpaka Muhimbili km 500?

Sasa nchi zenye Watalii wengi sana zina mpaka Ambulance za Helikopta ambapo Mtalii anafwatwa juu na kukimbizwa Hospitali moja kwa moja sasa huu ni mfano tu na Watu matajiri wanajali sana mambo kama haya!

Ndio maana nasema kwanza ni lazima kujenga na kuwekeza nguvu zote kwenye hizi primary Industiries kwa maana hapa ndiko kwenye kazi zinazolipa vizuri na hivyo kuongeza mapato ya Watu wetu na hizi primary Industries zitahitaji Miundombinu kama Br. Hospitali za kutibu watu watakaoumia kwenye migodi, n.k sasa hii tukiiweza ndio tunaweza kwenda kwenye Utalii ambao kwangu mimi ni secondary Industries na watu wanaofanya kazi kwenye hii sekta ni low paying jobs hivyo michango kwenye uchumi siyo mikubwa sana ukilinganisha na watu walioajiriwa kwenye Migodi, Gesi n.k halafu isitoshe tukifanikiwa hapa hata tunaweza pia tukategemea utalii wetu wa ndani kwani Wananchi wetu watakuwa fedha za spend!
 
Too much negativity here.

Nitakuwekea picha moja itaniepusha kuandika maneno mengi.

TTB should think outside the box.

CK6aONG.jpg
Tatizo siyo kufikiria nje ya kisanduku tu bali hao watalii watakujaje hapa. Huwezi kutarajia mashirika ya ndege ya nje yawe msingi wa kukuletea watalii hao. Hayo yanatakiwa yawe nyongeza tu kwa shirika lako. Tunavyokwenda si muda mrefu hata Rwanda watatupita kwa idadi ya utalii. siyo too much negative bali am disappointed by our priorities in all areas of our economy.
 
Nimeangalia documentary moja inayohusu East Africa tourism, nadhani ni muda wa kuwaweka wazee wapumzike, kazi ifanywe na vijana wadogo.

Honestly jamaa bado wana mipango ya kizamani sana, the world is changing, we have to change with it, kila mtu anataka kwenda Dubai coz wamejaribu kuonyesha youth culture, wanajaribu kwenda na trend, attraction zetu ilifaa tutumie kama huyo jamaa alivotoa mfao hapo juu wa hollywood actors, athletes etc kama advertisements.

Mtu anaweza akaona kama a crazy idea but it works zaidi ya mtu anavofikiri, am positive kati ya watalii wengi wanaokuja nchini wengi wao ni vijana sio wazee, we must give them reasons to come here.. kwenda kuweka mabango kwenye soccer matches was a stupid move, watu wameenda kuangalia mpira sio mabango, asilimia kubwa they don't even notice kama kuna mabango pale..
 
HAPANA! Lazima ujue ya kwamba Utalii ni uwekazaji wenye Gharama sana na nchi kama ni masikini na haina miundombinu Imara ni ngumu sana kuweza kufaidika na Utalii!

Nitakupa mfano mdogo sana chukulia Ml.Kili Mtalii anapanda at his/her own risk kama akizimia huko juu atashushwa na machela mpaka chini na hapo utampeleka Hospitali gani? KCMC au mpaka Muhimbili km 500?

Sasa nchi zenye Watalii wengi sana zina mpaka Ambulance za Helikopta ambapo Mtalii anafwatwa juu na kukimbizwa Hospitali moja kwa moja sasa huu ni mfano tu na Watu matajiri wanajali sana mambo kama haya!

Ndio maana nasema kwanza ni lazima kujenga na kuwekeza nguvu zote kwenye hizi primary Industiries kwa maana hapa ndiko kwenye kazi zinazolipa vizuri na hivyo kuongeza mapato ya Watu wetu na hizi primary Industries zitahitaji Miundombinu kama Br. Hospitali za kutibu watu watakaoumia kwenye migodi, n.k sasa hii tukiiweza ndio tunaweza kwenda kwenye Utalii ambao kwangu mimi ni secondary Industries na watu wanaofanya kazi kwenye hii sekta ni low paying jobs hivyo michango kwenye uchumi siyo mikubwa sana ukilinganisha na watu walioajiriwa kwenye Migodi, Gesi n.k halafu isitoshe tukifanikiwa hapa hata tunaweza pia tukategemea utalii wetu wa ndani kwani Wananchi wetu watakuwa fedha za spend!
HASWA!

Which is why nikasema it all comes down to infrstucture.

Miundombinu ndio uti wa mgongo wa uchumi wa nchi yoyote ile duniani... WB ingeipa issue ya miundombinu kipaumbele na siyo utalii. Mi mwenyewe naona kwa hilo wamekosea!
 
Sijaisoma hii habari, ila nikukumbushe tu hata utalii ni sehemu ya rasilimali zetu pia.

Kuna nchi nyingi tu duniani ambazo sehemu kubwa ya uchumi wao hutegemea utalii, mfano Misri.

La muhimu ni kuangalia jinsi ya kuboresha tu sehemu zote kwa uwiano.
Binafsi napinga Ripoti kwa kiasi kikubwa sana, na nasema Tanzania hahiitaji kutoa Kipaumbele cha kwanza kwenye utalii, bali KIPAUMBELE CHA KWANZA kiwe kwenye Rasilimali zetu!

Tuwekeze kwenye Madini kama Nickel yetu, Uranium, Dhahabu, Shaba, Bauxite, Chuma, Makaa ya Mawe na kwenye Gesi yetu hapo ndipo pa kuhakikisha piga uwa tunatoboa, haya mambo ya Utalii ni ya ziada tu lkn UCHUMI hasa uko kwenye Rasilimali zetu!
 
​Nina wasiwasi hapa kuna muvi nyingine tunataka kuchezewa, kwanini hawashawishi kwenye madini na gas?? Au wanataka watushawishi tukiwa tumeshaliwa ndo tutoe tongotongo?
 
Sijaisoma hii habari, ila nikukumbushe tu hata utalii ni sehemu ya rasilimali zetu pia.

Kuna nchi nyingi tu duniani ambazo sehemu kubwa ya uchumi wao hutegemea utalii, mfano Misri.

La muhimu ni kuangalia jinsi ya kuboresha tu sehemu zote kwa uwiano.
Mkuu hapa hakuna kitu kama wanamaanisha kwa serikali hii iliyopo madarakani.

Nimesoma ripoti ile ya PAC kuhusiana na ATCL nimeondoa imani kabisa na utawala huu uliopo. Hapa tunao viongozi wanaofikiria fursa za kujineemesha wao tuu, na kila wazo la kuleta maendeleo wao wanawaza yao kwanza. Mpaka waondoke ndio Utalii au lolote lile litaleta manufaa kwa nchi yetu.

Hawa wa sasa hata ukiwaambia biashara ya Senene inaweza kubadili maisha ya watanzania watahakikisha wao kwanza.
 
  • Thanks
Reactions: 999
Tatizo siyo kufikiria nje ya kisanduku tu bali hao watalii watakujaje hapa. Huwezi kutarajia mashirika ya ndege ya nje yawe msingi wa kukuletea watalii hao. Hayo yanatakiwa yawe nyongeza tu kwa shirika lako. Tunavyokwenda si muda mrefu hata Rwanda watatupita kwa idadi ya utalii. siyo too much negative bali am disappointed by our priorities in all areas of our economy.


Shirika la ndege la Tanzania ni muhimu lakini sio subject to requirements. Kuna nchi zinafanya vizuri sana kwenye utalii lakini mashirika yao ya ndege ni average.

Hata Air Tanzania ikiwa na Airbus A380 kwenye fleet yake yote. Usidhani Mtu anayeenda kulipa $2000 kwa siku Bilila lodge atapanda Air Tanzania Asilani.

i would prefer we have better airports than waste money on national carrier that will not be likely to compete effectively in global scale.

Pesa za kuifufua Air Tanzania ili iwe globaal Airline zitumike kujenga kiwanja chenye hadhi inayokubalika KIA. Air Tanzania can do just fine kwa kupanua wigo wake ndani ya Tanzania.

Rwanda ni nchi ndogo kwa Tanzania kujilinganisha nayo. We have to think bigger, and focus on tourism heavyweights kama Egypt.

Habari ya kujifanya jack of all trades unaishia kuji-stretch too thin halafu mwisho wa siku kila kitu kinakwenda shaghala baghala.Kama KIA ni world class, Kila Shirika la maana duniani litaleta ndege zake, na kufungua ofisi zake Tanzania. Kwa nchi za Asia,kuhakikisha kuwa TTB inafanya localised promotions kwenye nchi zenye population kubwa ya potential tourists ni muhimu sana.biahsara ya kutanagza vinyago kutwa kucha inachosha.TTB has to be creative.
 
Shirika la ndege la Tanzania ni muhimu lakini sio subject to requirements. Kuna nchi zinafanya vizuri sana kwenye utalii lakini mashirika yao ya ndege ni average.

Hata Air Tanzania ikiwa na Airbus A380 kwenye fleet yake yote. Usidhani Mtu anayeenda kulipa $2000 kwa siku Bilila lodge atapanda Air Tanzania Asilani.

i would prefer we have better airports than waste money on national carrier that will not be likely to compete effectively in global scale.

Pesa za kuifufua Air Tanzania ili iwe globaal Airline zitumike kujenga kiwanja chenye hadhi inayokubalika KIA. Air Tanzania can do just fine kwa kupanua wigo wake ndani ya Tanzania.

Rwanda ni nchi ndogo kwa Tanzania kujilinganisha nayo. We have to think bigger, and focus on tourism heavyweights kama Egypt.

Habari ya kujifanya jack of all trades unaishia kuji-stretch too thin halafu mwisho wa siku kila kitu kinakwenda shaghala baghala.Kama KIA ni world class, Kila Shirika la maana duniani litaleta ndege zake, na kufungua ofisi zake Tanzania. Kwa nchi za Asia,kuhakikisha kuwa TTB inafanya localised promotions kwenye nchi zenye population kubwa ya potential tourists ni muhimu sana.biahsara ya kutanagza vinyago kutwa kucha inachosha.TTB has to be creative.

Kama unafikiri tatizo ni Uwanja ni kwanini Uwanja wa Zanzibar unapata ndege na wageni wengi kuliko KIA? Wakati KIA ni mzuri kuanzia Miundombinu mpaka huduma mara 50 ya wa Zanzibar? Au kwanini Uwanja wa Mombasa ambao ni kama Songwe (Mbeya) tu lkn unapata wageni wengi kuliko wa KIA?
 
Kama unafikiri tatizo ni Uwanja ni kwanini Uwanja wa Zanzibar unapata ndege na wageni wengi kuliko KIA? Wakati KIA ni mzuri kuanzia Miundombinu mpaka huduma mara 50 ya wa Zanzibar? Au kwanini Uwanja wa Mombasa ambao ni kama Songwe (Mbeya) tu lkn unapata wageni wengi kuliko wa KIA?


kwa sababu Mtalii akilinganisha KIA na JKIA anapata unafuu JKIA, Zanzibar iko karibu sana na Dar, hivyo ni 20 minutes detour kwa mashirika mengi ya ndege.huwezi fananisha na 2 hour marathon ya kutoka Dar kwenda KIA.

Mombasa hakuna option nyengine ya visitor wa Kenya kwenda coast, hivyo ile ni force.

Songwe, southern circuit is the most underdeveloped tourism circuit Tanzania.
 
kwa sababu Mtalii akilinganisha KIA na JKIA anapata unafuu JKIA, Zanzibar iko karibu sana na Dar, hivyo ni 20 minutes detour kwa mashirika mengi ya ndege.huwezi fananisha na 2 hour marathon ya kutoka Dar kwenda KIA.

Mombasa hakuna option nyengine ya visitor wa Kenya kwenda coast, hivyo ile ni force.

Songwe, southern circuit is the most underdeveloped tourism circuit Tanzania.


Nafikiri haujanielewa Swali langu, embu rudia kusoma polepole kama ukiweza! Nilichomaanisha ni kwamba wewe umesema ya kwamba tukiwekeza kwenye Uwanja mpya wa KIA na kuwa kisasa au sijui world class kama ulivyoita mwenyewe basi kila Shirika la ndege litakimbilia kuja KIA!
Na mimi ndio nikakuuliza kama tatizo ni Uzuri wa Kiwanja ni kwanini basi Uwanja mbaya wa Zanzibar unapata ndege na wageni wengi kuliko Uwanja mzuri wa KIA?
 
Nafikiri haujanielewa Swali langu, embu rudia kusoma polepole kama ukiweza! Nilichomaanisha ni kwamba wewe umesema ya kwamba tukiwekeza kwenye Uwanja mpya wa KIA na kuwa kisasa au sijui world class kama ulivyoita mwenyewe basi kila Shirika la ndege litakimbilia kuja KIA!
Na mimi ndio nikakuuliza kama tatizo ni Uzuri wa Kiwanja ni kwanini basi Uwanja mbaya wa Zanzibar unapata ndege na wageni wengi kuliko Uwanja mzuri wa KIA?


tatizo lako wewe huna tofauti na fundi mchundo anayefikiri kila tatizo ni msuari unatatuliwa kwa nyundo.

Sikiza, Downside ya KIA ni below standard Airport,compare to the closest airport, which competes with KIA. that is not the case with Zanzibar. Umeelewa?

Ukiwa kiongozi hautatui tatizo kw akutumia formula moja tu, unatazama kila tatizo kwa u-unique wake.Zanzibar haina competition na JKNIA actually zina-complment each other. That is not the case between JKIA na KIA. Mtalii akishatua JKIA haji tena KIA kwa ndege, atapanda tour bus. Mtalii anayeenda Zanzibar hahitaji kutua dar, sicho alichokifuata TZ.

Nani amekuambia KIA ni uwanja Mzuri?kwa kiwango kipi?unalinganisha na Musoma Airport au?
 
Back
Top Bottom