Zzk aliamini kauli ya wassira na mishiko ya ccm

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,334
1,464
kauli ya Waassira ilikuwa imebeba uzito pale walipojua kuwa kijana wao ZZK ndio njia pekee ya kuimaliza CDM. Alisaidiwa kuanzisha masalia, then MM, MM2 na mabadiliko 2013. Wote Wassira, ZZK, Nchimbi wameangukia pua. Jitahada za ZZK na Wassira zimesaidia kuitangaza CDM na kuvifanya vyombo vyote vya habari kuitangaza CDM kwa wiki mbili sasa. CDM ilikuwa inaminywa sana kwenye TV, Magezeti, redio nk lakini kwa muda wa wiki mbili habari zake zimekuwa lulu.

Ninawaomba makanda wote watumie muda huu kutangaza na kusambaza chama vijijini kwani bomba la habri liko upande wetu. Nifuraha kubwa sana kwani kwa sasa kila mtanzania akiamka anasoma habari za CDM. Kila tangazo ni jema. ZZK na Wassira ndoto yao imeshindwa, walifikiri tuko bado miaka ya 90. Hawakufanya studies zao vizuri.

Tanzania ya leo ina tatizo kubwa sana la ajira, vijana wengi wapo mitaani baada ya kumaliza IV, VI. na vyuo mbalimbali. Ugunduzi wa gesi asilia na madini haujaweza kutatua tatizo sugu la ajira, kwani serikali ilishindwa kuandaa vijana wetu vyuoni kwa kuanzisha mitaala ya oil and gas, na vyuo mchundo vya kusaidia kuzalisha mafundi mchundo hasa kwenye matumizi ya vifaa vya uchimaji, mechanicla, electronics nk hasa kwenye secta ya madini na, oil na gas. Wao walikuwa bizy kufikiria kuingamiza CDM.

Na hii hapa ni kauli ya Dr SLaa huko mitaa ya Kigoma.

"CHADEMA HAITAYUMBA
Awali akizungumza na wananchi wa Kata ya Muhande katika mkutano wa hadhara uolifanyika viwanja vya Shule ya Msingi Muhande, alisema Chadema haitayumba milele licha ya hujuma inazofanyiwa na wapinzani wake.

Alisema Chadema haiwezi kuyumba kwa sababu inajikita katika misingi yake na wala haingozwi kwa matakwa ya viongozi bali kwa kuzingatia katiba.

"Chadema haiongozwi kwa matakwa ya Dk. Slaa wala Mbowe, bali kwa matakwa ya katiba, kwa hiyo kamwe haitayumba milele kwani kila jambo tunalofanya tunamtanguliza Mungu na kumaliza na Mungu," alisema.

Dk. Slaa alisema zipo kampeni kubwa zinafanywa kuichafua Chadema na hata kabla ya ziara yake mkoani Kigoma yapo maneno mengi ambayo yalisemwa ikiwamo kwamba yeye (Dk. Slaa) amepigwa marufuku kufanya ziara.

Alisema hakuna mtu anayeweza kumzuia asifanye ziara katika mkoa wa Kigoma na mikoa mingine kwa sababu Tanzania bado hatujafikia hatua ya mtu kuzuwiliwa kufika katika mkoa wowote.

Akizungumza juzi mjinni Kahama, mkoani Shinyanga, Dk.Willbroard Slaa, alisema chama hicho kinafanya kazi na kutoa maamuzi kwa kuzingatia katiba na kama wapo watu wanaotaka kuwa na chama legelege yupo tayari kuachia ngazi nafasi ya ukatibu mkuu.

Aliuambia umati wa wananchi katika viwanja vya CDT kuwa: "Chadema tuliahidi tutairudisha nchi kwenye mstari, kurudisha reli, lakini yote huwezi ukayarudisha ukiwa legelege, hatuhitaji chama legelege na kama mnasema tuwe na chama legelege hata ukatibu huu nipo tayari kuuacha."

Alisema Chadema ni chama makini ambacho kinaunganisha na katiba, hivyo mtu yeyote asifikilie ni mkubwa kuliko katiba.

"Hata mimi na Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema Taifa) katiba inatuwekea mipaka, kuna vitu ambavyo mimi kama katibu siwezi kuvisema, ni lazina visemwe na mwenyekiti wangu tu," alisema.

Dk.Slaa alisema yanayoendelea ndani ya Chadema kwa sasa yamepangwa na chama tawala kama ambavyo walishawahi kusema baadhi ya mawaziri wa serikali ya CCM kwamba Chadema itakufa kabla ya 2013, lakini ni propaganda itavuka.

Aliongeza kuwa mambo mengine yanayoendelea hivi sasa ndani ya Chadema Watanzania waiachie Kamati Kuu ambayo ina watu makini wataweza kulipatia ufumbuzi tatizo lililopo. CHANZO: NIPASHE
 
Dogo alilewa sana bichwa likawa kubwa kishenzi sasa sijuhi hari yake ikoje sahivi na siku zenyewe ndo hizo zishakwisha
 
Back
Top Bottom