Zungu :MBUNGE WA /ilala/mwenyekiti wa kamati ulinzi bungen /JUMUIA YA MADOLA..AKUNA WENGINE???

BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
9,735
5,003
KWANZA NAKUPONGEZA KAMANDA WANGU KWA KUCHAGULIWA KUTUWAKILISHA JUMUIA YA MADOLA NATUMAINI UNGENGE WEKO UMESAIIDIA KUFIKA HAPO ULIPO...
ANYWAY HILI NI KWA UPANDE WA CCM
HIVI MBONA VYEO VYOTE WANAPEWA WALIO NA VYEO NIKIMAANISHA YAANI INAFIKA WAKATI NAJIULIZA HIVI VYEO NI HAKUNA MWINGINE WA KUMPA AMA..MTU MMOJA ANAHODHI VYEO LUKUKI..ATAFANYAJE UENYEKITI WA USALAMA BUNGEN,ATATUMIKIA SAA NGAPI WANA ILALA,,NA JUMUIA YA MADOLA ATAENDA SAA NGAPI......

KILA LA KHERI KAKA MUNGU AKUWEZESHE YOTEE








Zungu aula mabunge ya madola Send to a friend Wednesday, 20 April 2011 08:20 0diggsdigg

Patricia Kimelemeta
WABUNGE wamemchagua Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu, kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Mabunge ya Nchi za Madola (CPA) Tawi la Tanzania.
Katika uchaguzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma, wabunge hao pia walimchagua Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo, kuwa Makamu Mwenyekiti wa CPA.
Zungu ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti ya Kamati ya Bunge ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje, alisema hatua hiyo inaonyesha imani waliyonayo wabunge wenzake.
“Imani huzaa imani, sitawaangusha nitawawakilisha vizuri na matumaini yangu ni kuhakikisha Tanzania inatetea maslahi yake. Hilo nitalifanya kwa nguvu zangu zote,” alisema.
Waliochaguliwa kuunda kamati ya utendaji ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Zainab Vullu, Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), Magdalena Sakaya na Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Lucy Owenya.
Wengine ni Mbunge wa Maswa Magharibi (Chadema), John Shibuda, Mbunge wa Mafia (CCM), Abdulkarim Shah, Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Mhonya Luhwanya, Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Raya Ibrahim Hamis na Mbunge wa Namtumbo (CCM), Vita Kawawa.
Rais wa CPA Tawi la Tanzania ni Spika wa Bunge, Anne Makinda na mlezi wake ni Waziri Mkuu, Mizengo
 
Back
Top Bottom