Zungu: Dini zikijiingiza kwenye Siasa zinaweza kuwachanganya Waumini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,819
13,582
IMG_4153.JPG

Mussa Azzan Zungu
IMG_4133.JPG

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu ametoa wito kwa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya kuendelea kushirikiana na Jamii katika kudumisha amani Nchini na kutozingatia watu ambao wana chuki binafsi wana nia ya kuharibu amani.

Ametoa ujumbe huo wakati alipohudhuria Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 53 wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania katika eneo la Ahmadiyya Centre lililopo Kitonga, Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam, Septemba 28, 2024 ambapo kauli mbio ya Mwaka huu ni ‘Uislamu na Amani’.

Zungu ameisisitiza Jumuiya hiyo kuzingatia Haki za Binadamu kama nyenzo ya kustawisha amani nchini na kuongeza kuwa anatambua mchango wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya ikiwemo kujenga shule, kuchimba visima vya maji na huduma za hospitali.

Amesema amefika eneo hilo kumuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa afike katika mkutano huo lakini kutokana na kuwa na ziara Mkoani Ruvuma akamtuma Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amuwakilishe lakini naye akawa na ziara Nchini Marekani kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa.

“Serikali inatambua shughuli hii (Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 53 wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania), maelekezo na salamu za Rais ni kuwa wanatakiwa kuungana na Watanzania wengine kuhakikisha amani inadumishwa,” amesema Zungu.

Ameongeza anaomba tutimize wajibu wetu kwa kuungana naye katika kuleta maendeleo wakati tukielekea kwenye uchaguzi ujao wa Mwaka 2025.

Kuhusu Dini kujiingiza kwenye Siasa
Zungu anasema “Dini zikijiingiza kwenye Siasa zinaweza kuwachanganya Waumini, kuna muda wanaweza kuwa na taarifa zisizo sahihi na zinaweza kupotosha Umma na Waumini wanaweza kuingia katika jazba ya kuchukia Serikali bila kuwa na taarifa sahihi.”
IMG_4098.JPG

IMG_4131.JPG

Mkutano wa Ahmadiyya Tanzania
Naibu Spika amesema “Mikutano kama hii inakumbushana kufuata dini, inajenga umoja, amani, kumuogopa Mungu na kuacha dhambi.

IMG_4142.JPG

Screenshot 2024-09-30 100328.png

Khawaja Muzaffar Ahmak
Amir na Mbashiri Mkuu
Upande wa Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya, Khawaja Muzaffar Ahmak amesema “Tunafurahia kuwa na Naibu Spika ambaye ametoa mawaidha, tumefurahi kusikia Serikali yetu ipo pamoja nasi, tunasisitiza amani kwa Watu wote ili tupate maendeleo.
 
Back
Top Bottom