Zungu ataka huduma njia za intaneti zitumike kuongeza pato la Taifa

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Naibu Spika, Mussa Hazzan Zungu ameishauri Serikali kuona umuhimu wa kuzifanya huduma za njia za ‘internet’ (internet gateway) zichangie pato la Taifa (GDP).

Zungu amesema hayo kwenye mahojiano maalumu na Mwananchi kuhusiana na hoja zake alizozitoa bungeni wiki hii.

Miongoni mwa hoja hizo ni mapato yaliyoko kwenye umiliki wa njia za kutoa huduma ya internet (internet gateway), lakini siyo kwa kutoza bando.

“La pili, Tanzania hatuna GDP kwenye internet, ‘sovereignty’ ya internet gateway iko nje ya nchi kwa maana hiyo pesa zinakwenda nje ya nchi tunapowasiliana kwa kutumia internet. Sisi tunao ‘service providers’ (watoa huduma), lakini na wao vile vile wanalipa hizi pesa nje ya nchi.

“Nikuombe mheshimiwa Nape (Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye), wewe ni mtaalamu na wewe ndio mwokozi wa nchi hii tunakutegema wewe hufanye haya mabadiliko nchini mwetu tupate pesa nyingi kwenye intarnet.

“Sasa hivi mapato mengi ya simu siyo kwenye kupiga simu ni kwenye data, huko ndiko fedha zilipo. Kwa hiyo nakuomba wewe na wizara yako wa kushirikiana na Wizara ya Fedha, muweke mkakati maalumu wa kuhakikisha ‘gateway internet’ (njia ya internet inabaki nchini na mapato haya yabaki nchini tusilipe nje ya nchi.

“Internet inaweza ikawa sehemu moja ya maeneo mengi nchini hata vijana hawa wakawa ‘service providers’ (watoa huduma, najua siyo jambo dogo litapigwa vita sababu ni suala la pesa, hapa tunazungumzia masilahi ya Taifa, kumsaidia Rais (Rais Samia Suluhu Hassan) apate mapato, kusaidia vijana wapate ajira kuwa watoa huduma kwenye internet,” alisema.

Fuatilia mahojiano kamili kwenye gazeti la Mwananchi kesho Jumamosi ya Septemba 24, 2022.
 
Akafie mbali huko, yeye ndiyo chanzo cha misukosuko nchini na agenda zake za tozo za kijinga, kiukweli Rev. Mtikila hakukosea kuwaita gabachori
 
Si ndio hivi hivi aliropoka mambo ya tozo wazee wa Trat na Trab wakalichukua kichwakichwa na kututwisha zigo? Matokeo yake akasema hawakufanya alichomaanisha.

Sasa naona anakomaa ionekane Bado hoja yake ya tozo inamashiko.
 
“La pili, Tanzania hatuna GDP kwenye internet, ‘sovereignty’ ya internet gateway iko nje ya nchi kwa maana hiyo pesa zinakwenda nje ya nchi tunapowasiliana kwa kutumia internet. Sisi tunao ‘service providers’ (watoa huduma), lakini na wao vile vile wanalipa hizi pesa nje ya nchi.

“Nikuombe mheshimiwa Nape (Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye), wewe ni mtaalamu na wewe ndio mwokozi wa nchi hii tunakutegema wewe hufanye haya mabadiliko nchini mwetu tupate pesa nyingi kwenye intarnet.
Huyu ameamua kuzima moto kwa petrol, hivi huwa anapitia mitazamo ya watu wengine na kujifunza?
 
Sasa si muanzishe vya kwenu ili muweze kupata izo pesa, wezenu wanawekeza kwenye technolojia nyinyi mnawekeza kwenye matumbo
Nimecheka, nikawaza mbali Sana. Hayo magari ya kupasua lami yatapita saa ngapi? Badala ya kubuni ajira za vijana na wait wapate mapato wao wanashupalia kupunguza ajira za watanzania I'll wapate mapato.
 
Naibu Spika, Mussa Hazzan Zungu ameishauri Serikali kuona umuhimu wa kuzifanya huduma za njia za ‘internet’ (internet gateway) zichangie pato la Taifa (GDP).

Zungu amesema hayo kwenye mahojiano maalumu na Mwananchi kuhusiana na hoja zake alizozitoa bungeni wiki hii.

Miongoni mwa hoja hizo ni mapato yaliyoko kwenye umiliki wa njia za kutoa huduma ya internet (internet gateway), lakini siyo kwa kutoza bando.

“La pili, Tanzania hatuna GDP kwenye internet, ‘sovereignty’ ya internet gateway iko nje ya nchi kwa maana hiyo pesa zinakwenda nje ya nchi tunapowasiliana kwa kutumia internet. Sisi tunao ‘service providers’ (watoa huduma), lakini na wao vile vile wanalipa hizi pesa nje ya nchi.

“Nikuombe mheshimiwa Nape (Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye), wewe ni mtaalamu na wewe ndio mwokozi wa nchi hii tunakutegema wewe hufanye haya mabadiliko nchini mwetu tupate pesa nyingi kwenye intarnet.

“Sasa hivi mapato mengi ya simu siyo kwenye kupiga simu ni kwenye data, huko ndiko fedha zilipo. Kwa hiyo nakuomba wewe na wizara yako wa kushirikiana na Wizara ya Fedha, muweke mkakati maalumu wa kuhakikisha ‘gateway internet’ (njia ya internet inabaki nchini na mapato haya yabaki nchini tusilipe nje ya nchi.

“Internet inaweza ikawa sehemu moja ya maeneo mengi nchini hata vijana hawa wakawa ‘service providers’ (watoa huduma, najua siyo jambo dogo litapigwa vita sababu ni suala la pesa, hapa tunazungumzia masilahi ya Taifa, kumsaidia Rais (Rais Samia Suluhu Hassan) apate mapato, kusaidia vijana wapate ajira kuwa watoa huduma kwenye internet,” alisema.

Fuatilia mahojiano kamili kwenye gazeti la Mwananchi kesho Jumamosi ya Septemba 24, 2022.
Huyu jamaa mchimvi sana. Hata boko la "tozo" lilianzia kwake akawalisha wabunge matango pori.
 
Kang'ang'ania kwenye mambo ya simu tu. Angesema tuanzishe na viwanda vya magari kila Mkoa, tujitegmee kwa kutengeneza saloon hadi graders, mabasi na cranes. Ajira nazo zitaongezeka maradufu! Ukiagiza gari utatozwa kodi sawa na bei ya uliyonunulia sababu MaCCM yanaona fursa ya kuwapiga watu makodi ya ajabu sababu yanajua magari lazima yataagizwa kwa vile kumiliki gari siyo anasa. Serikali iingiilie masuala ya sekta binafsi, hadi miamala ya akaunti za Wananchi wake, hizo ni dalili za kufilisika.
 
Si ndio hivi hivi aliropoka mambo ya tozo wazee wa Trat na Trab wakalichukua kichwakichwa na kututwisha zigo? Matokeo yake akasema hawakufanya alichomaanisha.

Sasa naona anakomaa ionekane Bado hoja yake ya tozo inamashiko.
Nape nae atalichukua. Maana wanachowazia ni posho tu.
 
Hoja zake zina mawili, moja udanganyifu na pia ukosefu wa uelewa.

Wakati ule tunasambaza mkongo wa taifa tulikuwa tunaambiwa gharama zitashuka. TTCL ikafufuliwa na kwa ninavyojua mimi, makampuni mengine yanachukua internet zao kupitia TTCL.

Pia yeye anaangalia tu faida zitakazopatikana kwa hao vijana kuwa internet service providers. Kwanza sina uhakika anamaananisha huduma gani hasa anapoongelea service providers? Anaongelea kampuni za kushindana na Vodacom, Tigo? Kwa nini TTCL inashindwa huko pamoja na kuwa ina support yote ya serikali?

Na pesa kwenda nje ya nchi inamkera nini kama wanawatoza kodi stahiki? Haya mawazo ya 'kiMagufuli' ndiyo yametuletea ATCL na huduma zake ambazo sihitaji kuzielezea. Hawa viongozi wanahitaji uthibitisho gani watambue serikali haiwezi kutoa huduma kwa ufanisi? Kwa nini wanakuwa na wivu na mafanikio ya watu na makampuni binafsi wakati mafanikio hayo ndiyo yanatakiwa kuwa uthibitisho wa mafanikio ya serikali? Ni vijana wapi hao wenye mitaji ya kushindana na Vodacom na Tigo au anataka tu kuwatumia kama chambo ili tu kuwafukuza wawekezaji ili TTCL ibaki peke yake?
 
Back
Top Bottom