Zuio la Uchaguzi Meya wa Dar Lageuka Kaa la Moto, Aliyelisoma asema Hakujua kama ni halali au feki

Yaani ni ajabu sana. Mwanasheria mzima anajibu majibu mepesi hivyo?!
Hilo siyo ajabu kabisa. Ajabu ni pale wananchi wamekamata mwizi na kumtaka aziache mali alizoiba lakini badala yake Polisi wanaingilia kati na kuanza kuwakamata wananchi kwa sababu eti wamefanya vurugu.
 
Hizi sarakasi za Kipuuzi sana. Kwa mujibu wa clip ya tukio la Karimjee, huyo RAS wakati akisoma hilo zuio alisema AMEJADILIANA NA WANASHERIA WA JIJI NA WAKAMWELEZA ZUIO HILO NI LA MIEZI MITATU.Leo huyo Mwanasheria anadai hakulipitia vizuri sababu ya muda, ikawaje akatoa Ushauri aliompa RAS?Unashauri kitu usichokijua? Huyu awe wa Kwanza kutumbuliwa na kizimbani tunamuhitaji. RAS naye inaelekea KILAZA,maelezo anayotoa hayamsaidii kukwepa kwamba yeye ndiye chanzo cha hizo fujo. Kuna njama, na wote waliokula njama na kutenda kosa wanapaswa kupelekwa Keko!
Halafu RAS mwenyewe alishachungulia paper mapema akaona waendako ni mtiti akasepa zake na kumuachia huyo kaimu RAS.
 
aliyet

aliyetengeneza zuio mahakamani masawe, aliyepeleka zuio ukumbini mosha, aliyenyakua zuio kutoka kwa mwenyekiti mdee nyie wachagga acheni kucheza na akili za watu.




Wahi hospitali,fistula ya ubongo inatibika na matibabu yake ni bure kabisa.
 
Zuio la Uchaguzi Meya wa Dar Lageuka Kaa la Moto..... Aliyelisoma asema Hakujua kama ni Halali au Feki

Thursday, March 3, 2016

Baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kulikana zuio llilotumika kuahirisha uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, suala hilo limekuwa sawa na kaa la moto na hakuna mtu anayetaka kulishika.

Jana Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando, ambaye alikuwa mwenyekiti wa uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Jumamosi iliyopita, jana alisema hajui lilikotoka zuio hilo kwa kuwa alipewa tu na wanasheria wa jiji ili alisome kama lilivyo.

“Baada ya kufika eneo la tukio (kwenye ukumbi wa Karimjee), nilikabidhiwa zuio hilo nilisome. Suala la kujua kama limeisha muda wake au la naomba uwasiliane na mwanasheria wa jiji au mwanasheria wa mkoa, wao ndio walikuwa nalo na hata nilivyopoteza vitu vyangu vingine, hilo (zuio) wao wanalo,” alisema Mmbando.

Baada ya kutimiza wajibu wake, kama alivyotakiwa na wanasheria hao, alisema ndipo zilipozuka vurugu na yeye kupoteza nyaraka zake ikiwa pamoja na ajenda na miongozo ya kikao hicho.

Kwa upande wake, Mwanasheria wa Jiji la Dar es Salaam, Jackline Mosha, alisema hakupitia tamko hilo kabla ya kumpa aliyekuwa mwenyekiti wa uchaguzi huo na kwamba alilikuta kwenye ukumbi huo bila kujua limetoka wapi.

Alisema walijua kuna zuio hilo baada ya kufika katika viwanja vya Karimjee siku hiyo ya uchaguzi.

“Zuio lilitoka Februari 5, sisi tulijua siku ya tukio, tulimkabidhi mwenyekiti Mmbando alisome, hatukufahamu kama limeisha muda wake.

“Hatukupata muda wa kulipitia na kujiridhisha kwa sababu haikuwa siku ya kazi kwa mahakama. Hata hivyo zuio hili hatukupewa mapema, wangetupa mapema tungejiridhisha na yote hayo tungeyajua kabla ya siku ile,” alisema.

Kuhusu madai kuwa walitumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufanya hivyo, alisema wao ni wanasheria na kwamba wanafanya kazi kitaalamu.

Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene, amesema kuwa tayari ameagiza apelekewe taarifa rasmi na Theresia Mmbando, ili kubaini ukweli kuhusu zuio hilo kama lilikuwa la kweli au la.

Waziri Simbachawene alitoa kauli hiyo juzi na kusisitiza kuwa kwa wakati huo hakuwa na taarifa zinazothibitisha zuio la kuahirishwa kwa uchaguzi huo lililosomwa na Mmbando kama ni la kweli au la.

“Kwa sasa kama wizara hatuna cha kusema kuhusiana na tukio zima lililitokea siku ile. Kama mnavyojua Katibu Tawala alipigwa anaumwa, yeye ndiye aliyesoma zuio hilo hivyo tunasubiri apone atuandalie taarifa kamili,” alisema na kuongeza:

“Kama Waziri sijapokea taarifa zozote zinazosema zuio hilo lilikuwa halali au la. Tusubiri kwanza atuandikie hiyo taarifa yake ili tufanye ulinganisho ndipo wizara itapata cha kusema,” alisema.

Uchaguzi huo ulipangwa kufanyika kwanza Desemba, mwaka jana, ukapangwa kufanyika Januari 23, mwaka huu lakini na baadaye kupangwa kuwa Februari 8.

Februari 8, mwaka huu, madiwani baada ya kufika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya uchaguzi, walikabidhiwa barua ambazo hazikueleza sababu za kuahirishwa kwake bali utafanyika utakapopangwa tena na ndipo ulipopangwa kufanyika Jumamosi iliyopita.

Jumatatu wiki hii, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Warialwande Lema, alikanusha taarifa kwamba mahakama hiyo imetoa zuio la uchaguzi huo.

“Mahakama ilitoa amri ya zuio la muda Februari 5, mwaka huu la kuzuia uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari 8 na ilipanga kusikiliza maombi hayo Februari 15 lakini walalamikaji hawakufika mahakamani,” alisema na kuongeza:

“Mahakama ilipanga tena maombi hayo kusikilizwa Februari 23, mwaka huu, lakini pia walalamikaji hawakutokea mahakamani.”

Walalamikaji katika shauri hilo walikuwa Susan Massawe na Saad Khimji, dhidi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam.

Akiendelea kufafanua, Hakimu Lema alisema baada ya walalamikaji kushindwa kufika, mahakama iliondoa maombi ya zuio yaliyokuwa yamewasilishwa mbele yake na walalamikaji pamoja na zuio lililokuwa limetolewa awali.

“Aliyesema mahakama imetoa zuio ni uongo kwa kuwa walitumia amri ambayo ilipitwa na wakati. Sijui chochote kuhusu zuio la Februari 27, mwaka huu,” alisema Hakimu Lema.

Kwa upande wake, Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi Cyprian Mkeha, alisema baada ya maombi hayo kuondolewa mahakamani, hajapokea maombi mengine kuhusu kuzuia uchaguzi huo.
Chanzo Mpekuzi blog
waliokua wanasema serikali ya mwaka huu imeletwa na Mungu ilifaa waende kutubu
 
Wahuni hapa mtu akifukuzwa wa hawa washitakiwa na wafungwe jela. Hii ndiyo njia pekee ya kukomesha haya mambo.
Namsubiri
kwenye kona Magu na team yake ya kutifua majibu. kama watabaransi hapa. KUNA ATAKAYEFUKUZWA KWA UZEMBE AU ATATETEWA KWA SABABU ...........
 
Kuna watu wanasema wana hofu ya Mungu na wanamcha Mungu.Huko dio kumcha Mungu? Mheshiwa JPM uamuzi wa watu ni uamuzi wa Mungu.Sheria ya watu ni sharia ya Mungu.Uko kwenye majaribu m,akubwa juu ya hofu yako kwa Mungu na uchaji wako kwa mungu.Ynayofanyika ni kinyume cha mapenzi ya Mungu.Mwenye macho haambiwi Tazama.Tenda haki Mungu atakubariki na atakujazi.
 
Hii ni sawa na kumpiga mwizi halafu ukafunguliwa mashitaka wewe! Yaani bora Mungu angeumba mashetani badala ya ma CCM!
 
Ni kwanini sisi CCM tunapenda kupata UMEYA wa DAR kwa njia ya PANYA. Kuna uozo gani tunataka kuficha? tusimwaibishe RAISI wetu tuache uchaguzi uwe HURU na HAKI.
 
narudia kauli yangu ya kila siku,ukiwa mwanaccm lazima uwe hayawani...!!hebu fikiria mwanasheria makini wa jiji naye anakili kuwa alitoa hilo zuio bila kujua kama limwkwisha muda,vipi kuhusu mikataba wanayotakiwa kutoa ushauri wakisheria kulinda maslahi ya taifa??yaani unakuwa kwenye nafasi nyeti lakini kumbe nimbumbumbu wa kutupwa,chochote kinachokuja mbele yako kisa kimetoka kwa boss unapitisha tu..!!Siku ikiondoka ccm madarakani itabidi magereza yaongezwe maana mapuuzi yakufungwa nimengi sana
Yaani nimesoma hiyo sehemu inayomuhusu huyo dada nikashangaa sana. Yaani unajinasibu kuwa unafanya kazi Kwa weledi na kitaalam alhali unaingizwa mkenge na matapeli!!! Huyu dada na wenzie wanapaswa kufikishwa mahakamani Kwa kosa la kughushi nyaraka za mahakama.

Wakati huo huo wanapaswa kuachishwa kazi kupisha uchunguzi ili ibainike endapo walighushi nyaraka na Kama kuna vitendo vyovyote vya kijinai na rushwa. Maana wale jamaa wapeleka mapingamizi hawajambo Kwa hila na rafu
 
narudia kauli yangu ya kila siku,ukiwa mwanaccm lazima uwe hayawani...!!hebu fikiria mwanasheria makini wa jiji naye anakili kuwa alitoa hilo zuio bila kujua kama limwkwisha muda,vipi kuhusu mikataba wanayotakiwa kutoa ushauri wakisheria kulinda maslahi ya taifa??yaani unakuwa kwenye nafasi nyeti lakini kumbe nimbumbumbu wa kutupwa,chochote kinachokuja mbele yako kisa kimetoka kwa boss unapitisha tu..!!Siku ikiondoka ccm madarakani itabidi magereza yaongezwe maana mapuuzi yakufungwa nimengi sana
Ueledi wa wanasheria unabakwa kwa hali hii ya zuio feki!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hapo si majaliwa wala magu wala huyo Simba atathubutu kuwagusa halafu mtu mnafiki bilan chembe ya aibu anasema niombeeni .hii mijitu inaitwa ccm imelaaniwa siku nyingi EE Mungu shusha moto angamiza haya majitu
 
Kwa upande wake, Mwanasheria wa Jiji la Dar es Salaam, Jackline Mosha, alisema hakupitia tamko hilo kabla ya kumpa aliyekuwa mwenyekiti wa uchaguzi huo na kwamba alilikuta kwenye ukumbi huo bila kujua limetoka wapi.Alisema walijua kuna zuio hilo baada ya kufika katika viwanja vya Karimjee siku hiyo ya uchaguzi.
“Zuio lilitoka Februari 5, sisi tulijua siku ya tukio, tulimkabidhi mwenyekiti Mmbando alisome, hatukufahamu kama limeisha muda wake.“Hatukupata muda wa kulipitia na kujiridhisha kwa sababu haikuwa siku ya kazi kwa mahakama. Hata hivyo zuio hili hatukupewa mapema, wangetupa mapema tungejiridhisha na yote hayo tungeyajua kabla ya siku ile,” alisema.
Mwanasheria huo ndio utetezi wake hivi huu utetezi una mantiki kweli?Unampa bosi wako apitie tamko hata bila ya kujiridhisha?Kama Tamko hawajui limetoka wapi walilisoma la nini?Daaah
Hao ndio wasomi wetu,yaaani ningekuwa magu ningemtumbua jipu faster,yaaani learned friend anajibu mambo ya kisheria kihuni hivi!alafu anampa boss wake asome.
Huyu atakuwa bush lawyer au mtumishi wa ccm.
 
[]Ukichukua CCM na Shetani ukalinganisha, shetani utamuona malaika.[/QUOTE]
Mcha Mungu Magufuli kazi unayo kwenye chama chako.
 
Kuna watu wanataka kumharibia Rais wetu mpendwa, huwezi kusoma zuio LA mahakama halafu usijue LA lini. Zuio lolote LA mahakama huwa na Tarehe lilipotoka na Tarehe ya utekelezaji wa zuio. Kwa maoni yangu Huyo Mrs. Mmbando na hao wanasheria hawatakiwi kuwepo kazini kwa kuidhalilisha serikali na kuiingizia hasara.
 
Ni hatari sana,kunya anye kuku,akinya bata ameharisha.Daah!!Waziri anasubiri Katibu Tawala (Theresia Mmbando) apone ndio atoe taarifa,Wanasheria wa Serikali wanasema hawakuhakiki na kujiridhisha na tarehe na uhalali wa zuio kabla ya kumkabidhi Theresia alisome.Theresia naye anasema hakujiridhisha na uhalali wa zuio kabla ya kulisoma..Hii ni zaidi ya Majipu.CCM OYEEE!
Hapa kazi tu
 
Back
Top Bottom