Zuieni muziki wa nje,tukuze muziki wa ndani

N'gwanantugwa

JF-Expert Member
Apr 25, 2015
347
343
KAMA SUKARI;FUNGIENI MZIKI WA NJE PIA ILI TUKUZE MZIKI WA NDANI.

Ilikuwa katika mjadala wa bajeti ya habari,utamaduni,michezo na sanaa,Mbunge wa kigoma mjini Zitto Z Kabwe alichangia kwa masikitiko makubwa kuhusu ulimbukeni wa vyombo vyetu vya habari kupiga sana mziki wa nje huku wasanii wengi wenye weredi wakibaki hawajulikani kiwilaya,kimkoa wala kitaifa.

Kusema kweli katika bunge hili na lililopita, mbunge Zitto amekuwa mtetezi mkubwa wa maslahi ya wasanii kuliko hata wasanii waliopo bungeni. Nachukua fursa hii kumpongeza mbunge huyu kijana kwa kuona umuhim wa serikali kupitia Waziri wa wizara husika Ndugu Nape Nnauye kutengeza sheria itakayovibana vyombo vya habari kupiga mziki wa nje kwa kiwango maalum.

Inasikitisha na inashangaza vyombo vyetu vya habari vikubwa na vidogo vimekuwa vinatabia ya kunyima wasanii wa nchi hii muda wa kucheza hewan kazi(vibao) vya wasanii wanyumbani kisa hawana hela ya kulipia bila stakabadhi malipo yenye harufu ya rushwa wenyewe wakiita promo.

Vyombo vingi vya habari vinawatoza wasanii wandani kiasi kikubwa cha pesa huku muda mwingi wakipiga mziki toka Nigeria,South Afrika,Congo n.k bila malipo.Hii ni aina ya utumwa wa fikra uliopo kwenye ubongo wa operater wa mitambo ya vituo hivyo.Utumwa huu umetengeneza kansa kwa watangazaji na madj wa media ndogo.

Leo hii kunawasanii wanatoka katika maeneo ya radio ndogo zilizopo mikoani na wilayani hawasikiki kwenye media hizo.Media zinashindwa kucheza nyimbo za wasanii wa maeneo hayo bila hela ya maji au hela ya vocha ihali nyimbo za nje zinapigwa bila gharama yoyote.

Hii imepelekea wasanii wa ndani mziki wao kuzidi kukosa matumaini ya kusikika kwa watu wengi.Leo hii Tanzania inavituo zaidi ya 200 vya radio lakini hakuna vilivyoamua kupiga asilimia kubwa ya mziki wa ndani.

Baada ya kauli ya Zitto bungeni,kuna wasanii wameanzisha kampeni kushinikiza serikali nawadau wengine kuokoa mziki wa nyumbani kwa kucheza asilimia 90 mziki wa ndani na asilimia kumi zibaki kwenye muziki kutoka nje ya nchi.Kampeni hii nilitarajia wasanii walioko bungeni wataikazia mkazo ila ajabu mpaka sasa naandika hapa sijaona hotuba yoyote inayoonyesha wasanii hawa wakiongelea kadhia hii.

Naomba wabunge kama Sugu na Prof.Jay waunge mkono hoja ya Zitto bila kuangalia itikadi za vyama kwani hoja hii ni nzuri kwa maslahi ya wasanii wa nyumbani.

Sheria hii ikiundwa itasaidia kuinua sana wasanii wa ndani wasiofahamika kwa watu wengi.Tunaona serikali ikichukua hatua ya kuzuia vibali vya sukari nje ili kuokoa viwanda vya ndani,tunaomba pia ichukue hatua hii ya kuzuia upigaji holela wa muziki wa nje ili kulinda muziki wa ndani.Haina maana serikali ikizuia kiwango cha upigaji wa muziki wa nje katika media zetu ni ubaguzi.

Mataifa mengi duniani yamewalinda wasanii wa ndani kwa sheria kama hii.Kama serikali imeamua kuchukua jukum la kuagiza sukari nje yenyewe pia inaweza kupanga kiwango cha asilimia za mziki wa nje utakaosikika kwenye vyombo vya habari vya ndani.


#Tunaomba serikali na wadau wote wa muziki tuunge mkono kampeni hii, tumshinikize Nape aone umuhim wa kulinda sanaa ya ndani
Plate ya maarifa
 
KAMA SUKARI;FUNGIENI MZIKI WA NJE PIA ILI TUKUZE MZIKI WA NDANI.
Ilikuwa katika mjadara wa bajeti ya habari,utamaduni,michezo na sanaa,Mbunge wa kigoma mjini Zitto Z Kabwe alichangia kwa masikitiko makubwa kuhusu ulimbukeni wa vyombo vyetu vya habari kupiga sana mziki wa nje huku wasanii wengi wenye weredi wakibaki hawajulikani kiwilaya,kimkoa wala kitaifa.Kusema kweli katika bunge hili na lililopita,mbunge Zitto amekuwa mtetezi mkubwa wa maslahi ya wasanii kuliko hata wasanii waliopo bungeni.Nachukua fursa hii kumpongeza mbunge huyu kijana kwa kuona umuhim wa serikali kupitia Waziri wa wizara husika Ndugu Nape Nnauye kutengeza sheria itakayovibana vyombo vya habari kupiga mziki wa nje kwa kiwango maalum.
Inasikitisha na inashangaza vyombo vyetu vya habari vikubwa na vidogo vimekuwa vinatabia ya kunyima wasanii wa nchi hii muda wa kucheza hewan kazi(vibao) vya wasanii wanyumbani kisa hawana hela ya kulipia bila stakabadhi malipo yenye harufu ya rushwa wenyewe wakiita promo.Vyombo vingi vya habari vinawatoza wasanii wandani kiasi kikubwa cha pesa huku muda mwingi wakipiga mziki toka Nigeria,South Afrika,Congo n.k bila malipo.Hii ni aina ya utumwa wa fikra uliopo kwenye ubongo wa operater wa mitambo ya vituo hivyo.Utumwa huu umetengeneza kansa kwa watangazaji na madj wa media ndogo.Leo hii kunawasanii wanatoka katika maeneo ya radio ndogo zilizopo mikoani na wilayani hawasikiki kwenye media hizo.Media zinashindwa kucheza nyimbo za wasanii wa maeneo hayo bila hela ya maji au hela ya vocha ihali nyimbo za nje zinapigwa bila gharama yoyote.
Hii imepelekea wasanii wa ndani mziki wao kuzidi kukosa matumaini ya kusikika kwa watu wengi.Leo hii Tanzania inavituo zaidi ya 200 vya radio lakini hakuna vilivyoamua kupiga asilimia kubwa ya mziki wa ndani.
Baada ya kauli ya Zitto bungeni,kuna wasanii wameanzisha kampeni kushinikiza serikali nawadau wengine kuokoa mziki wa nyumbani kwa kucheza asilimia 90 mziki wa ndani na asilimia kumi zibaki kwenye muziki kutoka nje ya nchi.Kampeni hii nilitarajia wasanii walioko bungeni wataikazia mkazo ila ajabu mpaka sasa naandika hapa sijaona hotuba yoyote inayoonyesha wasanii hawa wakiongelea kadhia hii.Naomba wabunge kama Sugu na Prof.Jay waunge mkono hoja ya Zitto bila kuangalia itikadi za vyama kwani hoja hii ni nzuri kwa maslahi ya wasanii wa nyumbani.
Sheria hii ikiundwa itasaidia kuinua sana wasanii wa ndani wasiofahamika kwa watu wengi.Tunaona serikali ikichukua hatua ya kuzuia vibali vya sukari nje ili kuokoa viwanda vya ndani,tunaomba pia ichukue hatua hii ya kuzuia upigaji holela wa muziki wa nje ili kulinda muziki wa ndani.Haina maana serikali ikizuia kiwango cha upigaji wa muziki wa nje katika media zetu ni ubaguzi.Mataifa mengi duniani yamewalinda wasanii wa ndani kwa sheria kama hii.Kama serikali imeamua kuchukua jukum la kuagiza sukari nje yenyewe pia inaweza kupanga kiwango cha asilimia za mziki wa nje utakaosikika kwenye vyombo vya habari vya ndani.
#TUNAOMBA SERIKALI NA WADAU WOTE WA MUZIKI TUUNGE MKONO KAMPENI HII, TUMSHINIKIZE NAPE AONE UMUHIM WA KULINDA SANAA YA NDANI
Plate ya maarifa
Sheria itakuja tu just wait, nchi inaweza tungwa sheria yoyote hata ile kuwa oxygen italipiwa!
 
Back
Top Bottom