Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,193
- 299
Nimesoma tetesi kuwa Marehemu Ballal atachomwa moto na sio kuwa atazikwa. Kwa nini watanzania walioko US wasiwasiliane na mwanasheria mkuu au kuomba mahakama izuie kuchomwa kwa Ballal mpaka mwili wake ufanyiwe uchunguzi kuhakikisha au kukanusha kuwa alipewa sumu? Kama aliuawa basi uchunguzi uweze kufanyika. Je kuna wakereketwa wenye ubavu wa kulisimamia hili??
Prof Baregu ataka Interpol wachunguze kifo cha Ballali
Na Jackson Odoyo
SIKU moja baada ya serikali kusema kuwa hakuna sababu ya kuchunguza kifo cha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu nchini (BoT), Daudi Ballali, Mhadhiri Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwasiga Baregu amesema kuna haja ya tukio hilo kuchunguzwa.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili jana, Profesa Baregu alisema serikali inatakiwa ku kubali kufanya uchunguzi juu ya suala hilo na kama wao hawawezi watumie wataalamu wa Polisi wa Polisi wa Kimataifa (Iterpol).
Alisema suala la uchunguzi wa kifo cha Ballali bado lina umuhimu kwasababu yawezekana serikali haikuhusika, lakini watuhumiwa wengine katika suala lake wakahusika ili kupoteza ushahidi, kwa sababu walifahamu kuwa Balali alikuwa shahidi muhimu katika suala la Akaunti ya ya Madeni ya Nje (EPA).
Alisema suala hilo likipuuziwa litasababisha watuhumiwa hao wazidi kujificha kwani baadhi ya wananchi wanaamini kuwa Balali hakuchuwa fedha peke yake katika sakata hilo na amekufa kabla hajajibu tuhuma zilizo kuwa zikimkabili.
"Serikali haiko makini katika suala hili, kwa sababu kama kweli wanadai kuwa hawakuhusika, kwanini wasitoe hata historia ya ugonjwa kuanzia alipokuwa BoT hadi alipoondoka kwenda kutibiwa," alisema Profesa Baregu
Alisema kitendo cha serikali kuendelea kuzuia uchunguzi wa kifo chake, inazidi kupoteza ushahidi juu ya suala la EPA na kwamba ikiendelea na ukimya huo itadhahirisha kuwa wanaohusika katika sakata hilo wataendelea kuneemeka na fedha hizo na hazitapatikana na kabisa .
Profesa alisema kutokana na uzito na unyeti wa suala hilo wananchi hawataacha kuhoji na kuendelea kupoteza imani na serikali yao, jambo ambalo ni hatari kwa mfumo wa utawala.
Juzi serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora) na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ilitoa kauli zilizozidisha utata juu ya suala la kifo cha Balali kwamba, haina sababu ya kufanyia uchunguzi wa kifo cahe kwa kuwa alikuwa mgonjwa siku nyingi.