Tetesi: Zuhra Yunus ndiye Mkurugenzi mpya wa Azam TV

Mzee wa mbwebwe wa kubinya jicho moja hakula hii kitu kwel maana baada ya habar alipenda kusogelea
 
Aliyekuwa mtangazaji nguli wa BBC Swahili, Bi Zuhra Yunus ametundika daruga za utangazaji wa BBC tangu Ijumaa tarehe 14/01/2022 na kuhamia rasmi Azam TV kama Mkurugenzi mpya kuchukua nafasi ya Charles Hillary aliyeteuliwa na Rais Hussein Mwinyi wa Zanzibar kuwa Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano Ikulu. Zuhra ameondoka BBC baada ya kuitumikia idhaa hiyo kwa kipindi cha miaka 14. Tukumbuke kwamba Charles Hillary naye alitokea BBC kabla ya kuja Azam TV. Karibu nyumbani Bi Zuhra.

View attachment 2082904

Katika kazi zake za uandishi wa habari na utangazaji akiwa BBC, Zuhra amewahi kuwahoji watu mashuhuri wakiwemo marais, wasanii na wanasiasa mbalimbali. Mmojawapo wa wanasiasa waliowahi kuhojiwa naye ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Profesa Paramagamba Kabudi (a.k.a Profesa Majalala) kama unavyoweza kumsikia kwenye kipande cha mahojiano hapo chini.

View attachment 2082902

MAONI YANGU
Binafsi namkubali sana mtangazaji huyu nguli kutoka anga za Tanzania na ninamjivunia sio tu kwa kuwa ni mtanzania mwenzangu bali kwa sababu ya kazi yake ya utangazaji iliyotukuka. Kwa kweli ameipeperusha vema bendera ya Tanzania. Ni nadra sana kumpata mtangazaji mwenye karba ya Zuhra hapa nchini.

Nawasilisha.​
Mkurugenzi wa Azam media ni Thido Mhando.
 
Daah! Hongera dada zuhra yunus wa(BBC SWAHILI) naona ndo umeamua kula shavu kwa bwana bakhresa japo hata mimi sijapenda uamuzi aliouchukua but all in all kila mtu anaangalia maslahi yake huwezi mpangia huyu na salum kikeke hakika wanajua.
 
Nimesoma coment zote sijaona mtu wa kumuelewesha mtoa mada

Iv Chaz hilary alikuwa mkurugenz? Mm navyofaham Mkurugenz wa Azam ni Tido Mhando
Navyojua Chalz Hirary hakuwa mkurugenz
Ulitakiwa uandike ninavyojua chazi alikua ni ........
 
Back
Top Bottom