Carlssin
Member
- Oct 22, 2017
- 44
- 70
Mnamo mwaka 1998 Jan Koum [Kulia kwenye picha ] alikutana kwa mara ya kwanza kabisa na Brian Acton [ Kushoto ] wote wakiwa wafanyakazi katika shirika la Yahoo. Walifanya kazi hapo kwa miaka 9, hadi September 2007 ambapo walishauriana kuacha kazi pale Yahoo Inc na kuchukua mwaka mmoja wa kupumzika wakiwa wanatafakari ni kitu gani kingine tofauti wafanye.
Baada ya hapo waliamua kwenda Twitter na Facebook Inc kuomba kazi kwa Bwana Mark Zuckerberg , lakini wote wawili walitolewa nje maombi yao. Hapo ilipita miaka 2 bila kufanya lolote la maana hadi ilipofika January 2009 ambapo Jan Koum aliponunua iPhone, kipindi hicho App Store ilikuwa ina miezi 7 tu tangu ilipoanzishwa.
Kama alijua vile, aliishtukia kuwa itakuja kuteka sana soko la Apps za simu. Basi hapo ndio akamshirikishawa Brian Acton wazo lake kuhusu kutengeneza App halafu haraka sana waitupie kwenye App Store kabla haijashika kasi sokoni. Kouma aliipa jina hiyo App kuwa iitwe WHATSAPP, alichagua hivyo kwa sababu alikuwa anapenda sana kusalimia watu kwa kusema "What's Up". Basi, week moja baadae Feb 24, 2009 siku ya birthday yake, Koum aliitambulisha rasmi Whatsapp Inc, California.
Mwaka 2014, Koum na Acton walikubaliana kuiuza Whatsapp kwenye shirika la Facebook ambalo miaka 7 iliyopita waliombaga kazi hapo na wakakataliwa. Walikubaliana kuiuza kwa USD 19 Billions, lakini mwisho walipanda hadi USD 22 Billions.
Natumaini umejifunza kitu.