Zuchu hafanyi matangazo ya vileo. Vipi kuhusu kazi zinazodhaminiwa na makampuni ya vileo?

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,799
Hivi majuzi nilisikiliza interview ya Sallam SK kupitia kipindi cha The Switch cha Wasafi FM nikajifunza jambo -- kuwa kumbe si kila msanii yupo tayari kunyakua kila dili linalowekwa mezani, no matter how much mulla it brings.

Kumbe si ughaibuni tu ambapo watu wana uthubutu wa kukataa michongo ya pesa ndefu. Bongo tumefika pazuri. Inapendeza kuona sasa wasanii wetu wanaweza kuchagua pesa gani ya kuokota na ipi ya kuachia wengine.

Nimemsikia Mendez akisema bibiye Zuchu, kutokana na msimamo wake, hayupo tayari kukubali kazi za kutangaza vileo. Kwa mujibu wa meneja huyo, ambaye ninathubutu kumwita mwenye mafanikio zaidi kwenye soko la muziki wa Bongo, Zuchu coulda been pocketing megabucks from such endorsements.

Baada ya kufurahishwa na hayo, nimepata kujiuliza: msimamo huu unamaanisha pia kutofanya au kushiriki -- kwa namna yoyote ile -- kazi ambazo zinadhaminiwa na makampuni ya vileo? Vipi kuhusu matamasha yanayowezeshwa na vileo? Au hii ni yeye tu binafsi ndiye hataki kushika chupa na kutushawishi ni namna gani koo linasawijika linapokumbana na bia bariiiiiiid?

Natamani kufahamu msimamo wa Zuchu ni mpana kiasi gani. Ila kwakweli kuwa na misimamo ya namna hii mbele ya pesa ni jambo la kustahili pongezi.


Sehemu ya mahojiano ya Sallam SK
 
Hakuna aliye msafi isipokuwa kuna dhambi flani flani unakuta mtu unasema piga ua siifanyi. Mfano unakuta mtu anazini lakini hathubutu kuruka ukuta ukimuuliza anasema ni dhambi kubwa sana, ila kuzini ni dhambi pia hata kama hujaruka ukuta.
 
Zuchu Fala tu, kwenye mziki hakuna dini tusidanganyane, anatakiwa apige mpunga maana ndo njia aliyochagua over.

Kubagua cha kuchukua huku ukiwa kwenye entire state Ileile hamna lolote unafanya, just upo kwenye industry Ile Ile so piga kila aina ya mpunga unaotokeza
 
”Hawaogopi hata kusema "hukumu imekaribia"…!

Na waimbaji wa dini hata wao pia, wanatuzwa na wanaotengeneza bia..!!

Wanachanganywa na wanaofagilia, maovu na starehe za kupita hii dunia..!!”


~HAO.
 
Back
Top Bottom