Zuchu: Diamond Platnumz alinipata nikiwa masikini na kunitunza kama mtoto wake

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
413
1,000
Msanii Zuchu ni miongoni mwa wasanii ambao wamesajili katika lebo ya WCB inayomilikiwa na staa wa bongo Diamond Platnumz.

Baada ya kujiunga na lebo hiyo Zuchu ameonekana akiinuka kutoka kiwango kimoja hadi kingine kutokana na biii yake.

Ni msanii ambaye ana uhusiano mwema na wa karibu na Diamond, kama inavyoonekana mitandaoni.

Licha ya kejeli zote ambazo Zuchu amepokea kutoka kwa wanamitandao, amezidi kutia bidii kila kuchao.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo alipakia video huku akionyesha nyumba yake na kusema kwamba alikuwa ameithamini.

Pia aliweka wazi kwamba yuko tayari kusherehekea sikukuu ya krismasi, na hata kumshukuru Diamond kwa umbali amemtoa.

" Mimi Dai akinipata sikuwa na chochote . Alinikuta maskini akanitunza kama Mtoto wake. Alinipa mkataba katika Lebo yake, akanipa nyumba , akanipa gari na kunitafutia umaarufu unaonilisha Leo hii. Dai ni zaidi ya babangu Allah azidi kumueka poa Kwa ajili ya wengine wengi," Alisema Zuchu.

images (7).jpeg

 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
6,266
2,000
Maisha ya mama yake sio ya kwake yeye kazungumzia maisha ya kwake
Bado ni fikra za ajabu na kuvipa value vitu ambavyo havina thamani..., sauti yake na kipaji chake ni priceless (yaani hata mtu uwe na pesa kiasi gani kuna vitu huwezi kununua) mojawapo ikiwa ni kipaji..., kwahio sioni tatumia equation gani.., iwe quadratic au simultaneous ili nipate Jawabu la huyu kiumbe kuwa masikini...., labda umasikini wa fikra na fadhila....
 

John henry

JF-Expert Member
Feb 22, 2014
412
1,000
Hakuna kitu kibaya kama kufilisika kifkra,ivi kama daimondi n bora Zaid ya baba yake basi ni nani angemzaaa,Zuchu amekufuru aende kutubu kabla cku ya kiama haina fika
Mtu akisema mtu flan ni zaid ya baba haimaanishi ni bora zaidi ya baba yake ila ni neno tu la kuonesha umuhimu au mchango wake mkubwa! Mfano mdogo, kuna marafiki wanakuwa na msaada mkubwa mwisho wa siku unasema huyu ni zaid ya rafiki! Kwahyo mtu akisema ni zaidi ya rafiki we unafikiri nini??
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom