Zuberi Kaharibiwa Na Baba Mdogo Na Ibrahim Kaharibiwa Na Mwarabu!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zuberi Kaharibiwa Na Baba Mdogo Na Ibrahim Kaharibiwa Na Mwarabu!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Bikra, Jun 22, 2009.

 1. Bikra

  Bikra Senior Member

  #1
  Jun 22, 2009
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wanaume wawili Zuberi Juma, 22 na Ibrahim Ramadhani, 23, wamefikishwa kwenye Mahakama ya Mwanzo Magomeni wakiwa wamevaa kama mademu, kitendo kilichomchefua kabisa hakimu Mwanaidi Madeni wa mahakama hiyo na kuwafungia dhamana.
  Wanaume hao, Zuberi ambaye anajulikana kama Anti Zuberi na Ibrahim maarufu kama Anti Suzzy, wakiwa pamoja na wasichana saba, wamefikishwa kwenye mahakama hiyo wakikabiliwa na shtaka la kufanya umalaya.
  Kesi hiyo ilivuta umati wa watu ambao walijazana hadi madirishani kuisikiliza.
  Anti Suzzy na mwenzake Anti Zuberi walionekana kama wanawake halisi, kuanzia mavazi, kujiremba, kusuka nywele na hata sauti, jambo ambalo lilionekana kumkera mno hakimu huyo.
  Wasichana waliofikishwa kortini pamoja na akina Anti Suzzy ni Kibibi Athumani, 16, Sabina Ramadhani, 19, Tumaini Bushiri, 29, Hadija Ally, 27, Zuleikha Mohamed, 22, Mwajuma Otta, 22 na Mwajuma Ramadhani, 21.
  Hati ya mashtaka yao iliyosomwa kortini hapo ilidai kuwa Juni 11 mwaka huu, saa 2:00 usiku huko Magomei Mapipa, washtakiwa hao walikamatwa wakiwa hawafanyi shughuli yoyote ya maana.
  Hata hivyo imedaiwa kuwa kundi la askari waliwatia mbaroni likiongozwa na Konstebo Ayoub, lilibaini kuwa washtakiwa wote hao walikuwa wanauza miili yao, kitendo ambacho ni kosa kwa sheria za nchi.
  Sakata zima la kesi hiyo ya aina yake lilianza kama ifuatavyo baada ya hati ya mashtaka kumaliza kusomwa na hasa ilipofika zamu ya akina Anti Suzzy.
  Hakimu: Eti Zuberi ni kweli au si kweli?
  Zuberi: Si kweli.
  Hakimu: Wewe mwanaume au mwanamke?
  Zuberi: Mwanaume!
  Hakimu: Mwanaume anakuwa na sauti hiyo?

  Zuberi: (kimya)
  Hakimu: Na wewe Ibrahim, ni kweli shtaka lako?
  Ibrahim: Si kweli?
  Hakimu: Wewe nawe mwanaume?
  Ibrahim: Ndiyo!
  Hakimu: Mwanaume gani anakuwa hivyo?
  Ibrahim (kimya)
  Hakimu: Si unaona wanaume wenzako jinsi walivyo. Hebu waangalie (Anamuonyesha baadhi ya wanaume waliokuwepo kortini)
  Ibrahim: Ndiyo nimewaona.
  Hakimu: Wanafanana na wewe?
  Ibrahim: (kimya)
  Hakimu: Mwanaume gani anasuka nywele, ananyoa nyusi, anapaka wanja na hizo nguo kama za kike, jamani!
  Ibrahim: (kimya)
  Hakimu: Astaghafulullah!
  Afande: We Zuberi, hebu tueleze kwa nini uko hivyo?
  Zuberi: Mimi aliyeniharibu ni baba 'angu mdogo. Wazazi wangu wote walifariki ndiyo akanichukua nikae kwake.
  Afande: Hakuwa na mke?
  Zuberi: Hakuwa na mke. Akaanza kuniingilia na kuniambia nisiseme!
  Afande: Yuko wapi?
  Zuberi: Wakati huo tuko Tukuyu Mbeya, baadaye aliuza vitu vyake akaenda Sauzi na mimi nikaja Dar, nikawa nimeshazoea mchezo huo!
  Afande: Ulifikia kwa nani?
  Zuberi: Nilifikia kwa jamaa mmoja nikawa naishi naye kwa miaka minne, baadaye nikaachana naye, nikajiunga na kundi la mashoga wenzangu rasmi! Ndiyo mpaka leo tupo kwa Macheni!
  Afande: Na wewe Ibrahim ilikuwaje hadi ukawa hivyo?
  Ibrahim: Sikumbuki vizuri, lakini ninachojua ni kwamba kuna Mwarabu mmoja aliniingilia na ikawa ndiyo mchezo wake!
  Afande: Baadaye?
  Ibrahim: Baadaye nikaachana naye baada ya kuona anapenda sana watoto wadogo wakati mimi 'mkewe' nipo!
  Afande: Ehee?
  Ibrahim: Sasa jana nilipokuwa na wenzangu tunajiuza ndiyo tukakamatwa!.
  Hakimu: Jamani eee nendeni…mshanichefua hapa, hebu ondokeni.
  Afande: Haya wote nyanyukeni twendeni.
  Hakimu: Afande, unasikia, waambieni ndugu wote wa wasichana walioongozana na hawa 'maanti' hakuna dhamana hapa.
  Afande: (Anawaambia waliokuwa nje) Jamani hakimu anasema kesi nyingine dhamana ipo, lakini ya hawa 'maanti' pamoja na wasichana wao hakimu amefunga!
  Hakimu: Ndiyo nimefunga dhamana, sitaki mtu yeyote anifuate kwenye kesi hii ya 'maanti' na wasichana wao, waache kwanza waende rumande tarehe 26 Juni ndiyo nitatoa dhamana, wamenichefua sana . . . .

  To be Continued . . . . .
   
 2. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #2
  Jun 22, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Masikini ila hii ni changamoto kwa familia zenye watoto na kwa malezi ya kizazi hiki kwa ujumla. Ikiwezekana kwa wale wanaojenga nyumba sasa tafadhalini jengeni vyumba vya ziada

  1. Cha watoto wa kike (Peke yao)
  2. Watoto wa kiume peke yao
  3. Wageni wa kike peke yao
  4. Wageni wa kiume peke yao
  5. Baba na mama
  6. Housegirl-kama mkwanza unaruhusu
  7. Houseboy/Shamba boy- kama mkwanja unaruhusu.

  Angalau inawezakusaidia kuzuia kuharibiwa watoto.
   
 3. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  hii hali inatisha sio siri!

  Naona hakimu kakasirika kweli kweli,

  nisingetofautiana naye katika hili! daaaamn
   
 4. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Hao Maanti watapelekwa rumande ya jinsia gani sasa?
   
 5. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #5
  Jun 22, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hapo sasa bora wapelekwe kwa wanawake maana wakipelekwa kwa wanaume wanawezatolewa utumbo!
   
 6. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #6
  Jun 22, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  mungu anusuru.....
   
 7. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #7
  Jun 22, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Aaaaghhbrrrh!
  Nimejisikia kichefuchefu kabisa! Masikini u-Tanzania wetu!
   
 8. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #8
  Jun 22, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Duh, hapo kazi ipo!
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Jun 22, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,336
  Likes Received: 1,803
  Trophy Points: 280
  Eeh! Kuna wafanya plastic surgery huko nini?
   
 10. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #10
  Jun 22, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Tuangalie kwa kina yafuatayo:

  "lilibaini kuwa washtakiwa wote hao walikuwa wanauza miili yao, kitendo ambacho ni kosa kwa sheria za nchi".

  Sidhani kama kuna kosa la kuuza miili katika sheria zetu

  "wamefikishwa kwenye mahakama hiyo wakikabiliwa na shtaka la kufanya umalaya".

  Hakuna kosa la kufanya umalaya katika sheria zetu za nchi.

  "Hati ya mashtaka yao iliyosomwa kortini hapo ilidai kuwa Juni 11 mwaka huu, saa 2:00 usiku huko Magomei Mapipa, washtakiwa hao walikamatwa wakiwa hawafanyi shughuli yoyote ya maana".

  Ndio maana hati ya mashtaka inapishana kabisa na maelezo ya kosa.

  Kwa hali hii sidhani kama upande wa mashtaka (prosecution ) wataachieve kitu chochote kwani washitakiwa wote wanawake na wanaume wataachiwa tu.
   
 11. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #11
  Jun 22, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Huyu hakimu vp hata kama wapo vp, dhamana ni HAKI ya mshitakiwa on presumption of innosence until proven guilty.
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  Jun 22, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hao maanti wakiwekwa sello moja na wanaume watajuuuuuta kuuza miili yao.
  Duh maana kule kuna mijitu inaukame balaaaa hahahaha mtu kapigwa mvua 20 anakutana na anti kha! atahudumiwa ugali na maharage shuhuri night atajuuta.
   
 13. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #13
  Jun 22, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  waandishi wa udaku visa kweli kweli,...

  ...huyu ni underage, ...ana haki ya kulindwa kwa kutotajwa jina hadharani.  ...kwa maana hiyo kosa ni uzururaji (?), (siku hizi kuna curfew saa mbili usiku?)

  kudhaniwa ndio neno sahihi, kubaini maana yake nini? ...wana uhakika?
   
 14. Kobe

  Kobe JF-Expert Member

  #14
  Jun 22, 2009
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 1,756
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  hakimu kachukulia hasira,angewapa dhamani tu kwani huko rumande walipo hao maanti wa kiume ni BALAAA tupu,,jela jeraha.!
   
 15. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #15
  Jun 22, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nani alaumiwe?? Huyo mwarabu na huyo baba mdogo walitakiwa waadhibiwe kwanza.

  JIULIZE:
  Ni watoto wangapi mayatima wanafanyiwa vitendo hivyo??

  Umeisaidiaje jamii athirika??

  Tushirikiane kupiga vita vitendo hivyo, tuanze na kuimarisha familia zetu, epuka ajali za kujitakia
  kama UKIMWI zinazokusababishia kifo na kuacha watoto wetu wakitendewa vibaya.

  Kila mmoja wetu anawajibu, na atawajibishwa kulingana na matendo yake.
   
 16. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #16
  Jun 22, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kwa sababu gani wamenyimwa dhamana? Kwa sababu mashog, malaya au vipi? Hakimu ametumia mwongozo gani? Au chuki yake tu?
   
 17. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #17
  Jun 23, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Eti wamemchefua utafkiri mahakama ya mumewe!
   
 18. M

  Mtu wa Kawaida JF-Expert Member

  #18
  Jun 23, 2009
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Huyu hakimu anatia jasira. Je kwa tuhuma kama hizi ndio wanyimwe dhamana?? Mbona kina wazee wa vijisenti hawanyimwi dhamana??
   
 19. M

  Mtu wa Kawaida JF-Expert Member

  #19
  Jun 23, 2009
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hii hali inatia huruma sana. Kwani hawa wote hawakuta kuwa katika hali hii ni mazingira ndio yamewapelekea kifikia hali hii.

  Ni jukumu lete kwa kila mmoja kushirikiana kupiga vita kuondokana na hali hii.

  Vile vile watumiaji wa bidhaa hii watafutwe na wakamatwe. NAdhani watumiaji wakikamatwa wauzaji watakosa soko na wataacha hii tabia.

  Haya kina baba tuachane na tabia za kununua hii huduma kama kweli tumenuia kupunguza hii tabia kuendelea.
   
Loading...