Zote hizi ni hasira kutokanana na CDM kukipokonya CCM viti na kupunguza idadi za kura zao

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Kuna uwezekano mkubwa kwamba hasira zote hizi za polisi dhidi ya wananchi wa Arusha hasa zile za kurusha mabomu siku ile ya maombolezo zinatokana na CDM kunyang’nywa CCM viti vya udiwani na kuporomoka kwa kura za CCM katika kata hizo 22 ukilinganisha na ilivyokuwa katika uchaguzi wa 2010.
Gazeti la Mawio leo limetowa takwimu katika uchaguzi wa jumapili iliyopita kwamba pamoja na CCm kushinda kata nyingi, lakini chama hicho kikongwe kimeporomoka kwa kasi kulinganisha na 2010.



Katika uchaguzi wa jumapili CCM ilizoa 6 na CCM viti 16. Katika viti hivyo 6 vya CDM vitatu vimenyang’anywa kutoka CCM – yaani CCM imepoteza viti. Wengi wanasema iwapo ungefanyika uchaguzi katika kata 4 za Arusha, uwiano ungekuwa CDM 10 na CCM 16 kitu ambacho kinakiweka pabaya CCM kwani kwa vyovyote vile kinaonyesha mporomoko – yaani freefall ingawa wa pole pole.



Gazeti limeongeza kusema katika uchaguzi wa 2010 katika kata hizo 22 zilizofanya uchaguzi jumapili iliyopita, CDM ilishinda kata 2 tu – sawa sawa na asilimia 9 ya kura zote, huku CCM ikibeba kata 19 sawasawa na asilimia 86.36.
Lakini katika uchaguzi wa jumapili iliyopita CDM ilipata asilimia 27.27 na CCM kupata asilimia 72.73. Hivyo CDM imepanda kwa asilimia 18 wakati CCM CCM imeshuka kwa asilimia 14.


Hata katika jumkla ya idadi za kura zilizopigwa katika kata hizo CDM imezoa kura 18,431 huku CCM ilipata kura 17,968. Na iwapo kata zile nne za Arusha wangefanya uchaguzi kupanda kwa CDM kungezidi na kuporomoka kwa CCM nako pia kungezidi.


Kwa kuongezea tu hata katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata 28 mwaka jana, CDM ilifanikiwa kuinyang’anya CCM viti 3.

CC Nape Nauye
Mwigulu Nchemba
 
Umeiona hiyo like? Umesema cha kweli kabisa -- CCM inaporomoka pole pole na siyo siri tena -- na akina Chagonja ndiyo wamepewa kazi ya kujaribu kuiokoa kwa kulazimisha kuwa CDM wana vurugu. CCM ni kaput!
 
Back
Top Bottom