singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
Nianze kwa kuwauliza wapinzani, ni lini watapevuka na kufanya mambo kama watu wazima? Utu uzima ni dawa na pia utu uzima ni elimu tosha amabayo haiitaji kwenda chuoni kupata shahada ya kumwezesha kuitwa mtu mzima, kwa kuwa hakuna darasa la kufundisha masomo ili mtu apevuke kufikia utu uzima.
Sipendi kutumia mipasho ya Yule msanii muimbaji aliyemuita mizani wake ‘mtu mzima ovyo’ ingawa maneno hayo ni ya kweli. Inatuhuzunisha watanzania kwamba wapinzani sasa wanataka kujiumbia utamaduni wa kuzomea bila aibu, wanataka wananchi tuukubali utamaduni huu wa kihuni ndani ya bunge.
Mara ya kwanza walisusia kuapishwa kwa Rais John Magufuli pale uwanja, nasi tkasema labda matokeo ya kushindwa kwenye uchaguzi mkuu. Mara ya pili wapinzani wakaonyesha utovu wa nidhamu wa hali ya juu wakati Rais Magufuli alipokwenda kufungua (kuzindua) bunge la kumi na moja akimbatana na Rais wa Zanzibar Dk. Shein.
Hoja ya wapinzani ilikuwa Dk Shein urais wake umekwisha, wapinzani hawakujali kuwa wanajitukanisha kwa mbele ya watanzania waliomchagua Dk. Magufuli, na mbele ya mabalozi wanaoziwakilsha nchi zao na wageni waalikwa.
Wapinzani wajkaonyesha tabia za hovyo, kupiga kelele, kuzomea, kupiga miluzi kama kwamba watoto watukutu walioko darasani, tena darasa lisilo na mwalimu wala kiranja. Safari hii wamerudia tena tena kuzomea, kupiga mbinje, wanataka watanzania tuuzoee utamaduni wao wa hovyo kabisa.
Labda kidogo tuangalie jinsi zomea zomea ilivyoanza naamini waliotimamu wataungana name, ilianza hivi……Alipewa nafasi mbunge wa Iringa mjini Peter Msingwa, wakati anajenga hoja zake wabunge wa CCM walitulia tuli wakimsikiliza, na kumpa fursa ya kutosha kuwasilisha hoja yake, na huu ndio ukomavu na uungwana unaotakiwa kwa watu wanaoitwa waheshimiwa wabunge.
Lakini Mheshimiwa Naibu Spika Dk.Tulia Ackson alipompa nafasi waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nauye wabunge wa upinzani wakakosa vyote vitatu. Walikosa uvumilivu wa kutulia na kumsikiliza, wakakosa na ungwana kwamba naye ana haki ya kusikilizwa kama alivyosikilizwa Msigwa pia wakakosa na kujitambua kwamba wao ni waheshimiwa wanaotakiwa kujiheshimu, wakaanza zomeazomea, kupiga yowe, kupiga panda ambayo wapare wanaita ‘ukunga’ (hutolewa linapotokea janga).
Hayo ndio maana yananifanya niwaulize wapinzani hivi watakuwa lini? Watakapoanza kujiona ni watu wazima wanaopaswa kujiheshimu?.