Mwanzoni wakiitwa janjaweed miaka ile ya 1990 na 2000. Serikali za wakati huo zilikuwa zikikana kufahamu watu hao lakini cha ajabu uhalifu na hujuma zao zilizidi kila kukicha hasa wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu.
Miaka hii ya 2010 na 2015 wamepachikwa jina jipya la Zombi. Sasa WANAVAA SOKSI USONI na kujichora sura zao na huvaa vinyago na hufafana na zombie.
Vikundi hivi ni maarufu kwa kupiga, kupora na kuhujumu wapinzani tena mchana kweupe. Licha ya kuripotiwa polisi na taarifa kutolewa ,hakuna chengine kinachoonekana kufanywa na dola kwa upande wa pili.
Kwa mwaka 2015 kule Zanzibar kuliripotiwa matukio kadhaa ya kujeruhi na kuharibu mali ikiwemo kituo cha redio moja kuhujumiwa na mwandishi wake kupigwa. Wafuasi na wapenzi wa upinzani kuvamiwa misafara yao ya kampeni na kuvamiwa vijiwe vyao vya siasa maarufu kama Barza.
Licha ya matukio haya yote kuripotiwa na kufunguliwa majalada si Polisi wala mamlaka za kiutawala hazitowi mwendelezo wa kinachoendelea na hatima yake matukio hujirudia bila ya kufanyika hatua yoyote.
Tumezoweya matukio ya kihalifu ya aina hii, serikali huchukua hatua mahsusi za kidharura mfano ni kule Amboni Tanga na mkuranga. Serikali yote na jeshi la Polisi lilishughulishwa, lakini Zombi wa Zanzibar kimya.
Ni majuzi tu, Zombi walivamia baraza moja ya CUF huko jimbo la Pangawe Unguja na kujeruhi watu bila sababu. Taarifa zilienea na mpaka sasa kimya.
Katika hali hio ni wazi Zombi hawa wanapata baraka za watawala au wanalindwa na watawala. Haiwezekani iwe imeshindikana kufuatiliwa na kukamatwa kwa zaidi ya miaka miwili sasa.Na kinachoogofya basi wenye jukumu la usalama hawashughulishwi nalo.
Suala linakuja ikiwa mamlaka za Zanzibar zimeshindwa kuliondowa tatizo hili basi hata Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ndiyo dhamana wa usalama na ulinzi wa raia wote nao wameshindwa? tena kwa miaka miwili sasa?
Kwa mtiririko huu wa matukio, ni maoni yangu na ni dhahiri, Zombi wanalindwa na watawala.
Kishada.