Zombi wa Zanzibar, genge linalolindwa na Watawala

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Mwanzoni wakiitwa janjaweed miaka ile ya 1990 na 2000. Serikali za wakati huo zilikuwa zikikana kufahamu watu hao lakini cha ajabu uhalifu na hujuma zao zilizidi kila kukicha hasa wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu.

Miaka hii ya 2010 na 2015 wamepachikwa jina jipya la Zombi. Sasa WANAVAA SOKSI USONI na kujichora sura zao na huvaa vinyago na hufafana na zombie.

Vikundi hivi ni maarufu kwa kupiga, kupora na kuhujumu wapinzani tena mchana kweupe. Licha ya kuripotiwa polisi na taarifa kutolewa ,hakuna chengine kinachoonekana kufanywa na dola kwa upande wa pili.

Kwa mwaka 2015 kule Zanzibar kuliripotiwa matukio kadhaa ya kujeruhi na kuharibu mali ikiwemo kituo cha redio moja kuhujumiwa na mwandishi wake kupigwa. Wafuasi na wapenzi wa upinzani kuvamiwa misafara yao ya kampeni na kuvamiwa vijiwe vyao vya siasa maarufu kama Barza.

Licha ya matukio haya yote kuripotiwa na kufunguliwa majalada si Polisi wala mamlaka za kiutawala hazitowi mwendelezo wa kinachoendelea na hatima yake matukio hujirudia bila ya kufanyika hatua yoyote.

Tumezoweya matukio ya kihalifu ya aina hii, serikali huchukua hatua mahsusi za kidharura mfano ni kule Amboni Tanga na mkuranga. Serikali yote na jeshi la Polisi lilishughulishwa, lakini Zombi wa Zanzibar kimya.

Ni majuzi tu, Zombi walivamia baraza moja ya CUF huko jimbo la Pangawe Unguja na kujeruhi watu bila sababu. Taarifa zilienea na mpaka sasa kimya.

Katika hali hio ni wazi Zombi hawa wanapata baraka za watawala au wanalindwa na watawala. Haiwezekani iwe imeshindikana kufuatiliwa na kukamatwa kwa zaidi ya miaka miwili sasa.Na kinachoogofya basi wenye jukumu la usalama hawashughulishwi nalo.

Suala linakuja ikiwa mamlaka za Zanzibar zimeshindwa kuliondowa tatizo hili basi hata Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ndiyo dhamana wa usalama na ulinzi wa raia wote nao wameshindwa? tena kwa miaka miwili sasa?

Kwa mtiririko huu wa matukio, ni maoni yangu na ni dhahiri, Zombi wanalindwa na watawala.

Kishada.
 
unayonena ni kweli, halafu wanajulikana maeneo wanayopatikana muda wote wapo, mfano nyuma ya kituo cha polisi cha mwanakwelekwe
 
unayonena ni kweli, halafu wanajulikana maeneo wanayopatikana muda wote wapo, mfano nyuma ya kituo cha polisi cha mwanakwelekwe

Kwa kadiri siku zinavyosonga na hujuma za hawa jamaa kuzidi na bila kuchukuliwa hatua mahususi jamii inazidi kuamini kuwa wametengenezwa na kulindwa. Ndio nikaleta hii mada wanaohusika waelewe.
 
Kuna taarifa kuwa wakati mwengine zombi hulindwa na kusindikizwa na vyombo vya dola wanapokwenda kufanya hujuma.
 
No kweli malalamiko haya ya RAIA wa unguja yapo na niya muda mrefu kama alivosema mleta mada, hivi hakuna kauli yeyote ya serekali kuhusu hili suala?
Siwezi amino kama kweli serekali imeamua kupuuzia malalamiko ya (uzushi) ya RAIA wake!
Vilevile siwezi amni kuwa serkali na vyombo vyake vya ulinzi na usalama kwa kipindi chote hicho, eti wameshindwa kuwazibiti hao wahalifu!
Huu uwepo wa vikundi vya kihalifu vinavyoshika silaha za moto, na kuhujumu RAIA pasipo haki, na bila serekali kuchukua hatua zinazofaa kukomesha Mara moja matukio haya itatukosti! Vikundi vingi vinavyoshika silaha na hata magaidi, huanzia ktk vikundi kama hivi"
Watu wanaoajiriwa kwenye vikundi hivi hawawezi kulipwa sawa na polisi, wanalipwa kidogo mno na hawana madili, inawezekana hayo neo madili yao ksbb hawana kitu" Sikh wakisalitiana utasikia...wanatafutwa watu 200 waliotoroka na silaha nyingi vikiwemo vifururu vya jeshi!
Sio dalili njema kwa jamii yetu.
 
sasa kama watawala na police wameuchuna,umma ujuchukue jukumu la police,akishkwa mmoja akashughulikiwa na kumkatakata mikono sidhan kama wataendelea lkn kama wanacuf ndo wanaolengwa nanyi mkakaa kimya basi mmekubaliana na matokeo! iweje mvamiwe na vyombo vya dola vinakaa kimya na cuf mko kimya? siamin kama hao mazombi wao wanahat milik na kuwanyanyasa raia kias hch,cuf chukua sheria mkononi make hakuna namna! mateso huvumilika kwa muda na sio muda wote!
 
Mpunguze maneno maneno mjenge nchi yenu. ...siasa zinawatia umaskini ....anayeshiba mpigapo siasa mnamjua
 
sasa kama watawala na police wameuchuna,umma ujuchukue jukumu la police,akishkwa mmoja akashughulikiwa na kumkatakata mikono sidhan kama wataendelea lkn kama wanacuf ndo wanaolengwa nanyi mkakaa kimya basi mmekubaliana na matokeo! iweje mvamiwe na vyombo vya dola vinakaa kimya na cuf mko kimya? siamin kama hao mazombi wao wanahat milik na kuwanyanyasa raia kias hch,cuf chukua sheria mkononi make hakuna namna! mateso huvumilika kwa muda na sio muda wote!

Hapana ni bora kutii sheria bila shuruti.

CUF wamejitahidi sana kujizuiya kuchukuwa sheria mikononi kwa hili. Wamekuwa wakuilalamika mno lakini wanapuuzwa.

La msingi Watawala watende haki
 
Inshaalwa Mwenye enzi mungu atatuvua hasadi hizi za Zombie na inshaalwa atawalpa hapahapa duniani akhera itenda hesabu. Wako wapi wale waliokuwa wanajiita Unanijua Mimi?Leo kama wapo basi wako Ndembendembe kwa maneno ya msaliti.
 
kwanza ninyi wanafiki sana. huku wasiingilie mambo yenu mnajuana wenyewe hamchelewi,kutusema, na hivyo vikundi vyenu vya upande mwingine mnafundishna sana za mapigano na kuuwa,je.! au unafikiri watu hawajui. mnajuana wote mnayofanya na mambo yenu yatamalizwa na ninyi wenyewe
 
Back
Top Bottom