Zombe kuachiwa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zombe kuachiwa...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sheikh, Feb 5, 2009.

 1. S

  Sheikh Member

  #1
  Feb 5, 2009
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HABARI za kuaminika ni kwamba mtuhhumiwa mkuu katika kesi ya mauaji ya vijana wasiokuwa na hatia jijini huenda akaachiwa huru baada ya rushwa kugawanywa kama pipi kwa mahakimu, waendesha mashtaka na mawakili.

  Inaaminika fedha hizo zinatokana na mauzo haramu ya almsai na vito walivyoporwa marehemu.
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Unazungumzia mtuhumiwa gani? na ni kesi ipi?. Manake sasa kuna kesi ya Zombe na wenzake inayoendelea.
   
 3. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mkuu sheikh hii yako imekaa juu juu sana imekosa substance.hebu weka nondo za kutosha! kesi inaendelea kusikilizwa mwisho wa siku mahakama itaamua kama inawaona na hatia au la hayo ndiyo matokeo ya kesi yoyote inayokuwa mahakamani.Kwahiyo Zombe ni Innocent until proven guilty au hii huijui mkuu. lazima tukubaliane na maamuzi ya mahakama wakati mwingine kunakuwa hakuna hata rushwa iliyotembea ila tu kunakosekana ushahidi wa kutosha kuweza kumtia hatiani mshitakiwa.
   
 4. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Hapa katikati sikufuatilia sana, lakini jana nilisikiliza defense yake and I have to say hata mimi ningekuwa jury ningelazimika kumwachia kwa sababu there is reasonable doubt, na hakuna substantial proof kwamba alihusika na mauaji. Ushahidi wa mtu kusema eti Zombe alimwagiza is hearsay, there is nothing else tying Zombe to the crime. Prosecution ilichemka I think, na DPP alitaka sifa na aliharakisha hii kesi bila evidence ya kutosha. Ngoja mtaona kesi ya akina Mramba pia, they will walk.
   
 5. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Muhimu ni sheria ifuatwe, iwapo kama kuna watu kwenye ofisi ya DPP walichemka hao wanaweza kuchukuliwa hatua vilevile.
   
 6. M

  Middle JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2009
  Joined: Feb 7, 2007
  Messages: 243
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  yote sawa tu kwa Bongo,anaweza kuhachiwa,hata akina Yona vile vile
   
 7. Sober

  Sober JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2009
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 289
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Typical UDAKU... mtoa mada anaonekana ameshamhukumu mtuhumumiwa...na anaifuatilia kesi na hukumu yake kichwani. Sasa baada ya kuona upande wa utetezi wameanza kuibomoa kesi, anaanza ku pre empt verdict na udaku. Tuache mahakama
  ifanye kazi yake,na tuheshimu utawala wa sheria.
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Feb 5, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  hata mimi, pamoja na ujuzi wangu finyu wa sheria, lakini sijaona chochote kinachomtia Zombve hatiani. nadhani kuna namna ilifanywa na wmendesha mashitaka (aidha kwa maelekezo mahsusi au after he was compromised) na aka-frame mashitaka (in fact shitaka) kwa namna ambayo halitamtia hatiani hata mtu mmoja kati ya walioshitakiwa. katika kesi kama hii, haitarajiwi kuwe na charge moja tu-murder. Hilo ndilo alilolifanya mwendesha mashitaka na kwa kweli Zombe na wenzake wataachiwa kiulaini kwa sababu anayehusika na shitaka lililopo mahakamani wala hajakamatwa, na ninaamini kuwa alitoroshwa makusudi.
  lakini, mwisho wa siku, mchezo wa kuigiza utaisha kwa akina Zombe kuachiwa na jamii itaambiwa -"si mnaona, tuliwaburuza mahakamani lakini wameonekana hawana hatia." mwisho wa mchezo
   
 9. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Je waliofiwa walipewa fidia au mpaka kesi iishe?
   
 10. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Nimepokea sms mchana huu kuwa baadhi ya Watuhumiwa katika kesi ya mauaji inayomkabili kamanda Zombe na wenzake wamekutwa hawana mashitaka ya kijujibu. Nimpokea sms hiyo kutoka kwa ndugu yangu akniarifu kuwa ndugu yetu mmoja ambaye ni miongoni mwa Polisi waliotuhumiwa kufanya mauaji ya wafanyaboashara wa Madini kutoka Morogoro ameachiwa.

  Mliopo huko Dar mtujuze- walioachiwa ni wangapi, Zombe yumo kati ya hao?
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kwa mujibu wa habari za TBC1 (saa 7 mchana), Zombe na baadhi ya wenzake wana kesi ya kujibu. Hata hivyo watuhumiwa watatu wameachiwa huru baada ya ushahidi uliotolewa mahakamani kushindwa kuonesha walishiriki vipi katika kosa walilokuwa wanatuhumiwa kulitenda.

  NB:Mod unaweza kuiunganisha thread hii na ile nyingine iliyokuwa inaongelea kesi ya Zombe.
   
  Last edited: Feb 9, 2009
 12. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mkuu wakati tunasubiri nani wana kesi ya kujibu, tunaomba ututajie huyo aliyeachiwa. Lakini kama hutumii jina lako humu, usitaje manake ukimtaja ndugu yawezekana ikawa sababu ya kukujua. Manake humu JF kuna wanaoingia kwa majina yao, na kuna wana majina ya mtandaoni.
   
 13. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kwa habari nilizozipata mahakamani muda si mrefu washtakiwa watatu wameonekana hawana kesi ya kujibi na mmojawapo alikuwa dreva siku ya tukio... zombe yeye ameonekana ana kesi ya kujibu. ni hayo tu kwa sasa
   
 14. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #14
  Feb 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kesi ya Zombe: Watatu waachiwa huru

  Washtakiwa watatu katika kesi ya mauaji inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Abdalah Zombe na wenzake 12 wameachiwa huru mchana huu baaada ya kuonekana hawana kesi ya kujibu.

  Washtakiwa hao ambao waliondoka mahakama kuu wakiwa watu huru ni mshtakiwa namba 4, namba 6 na namba 8.

  Kesi imeahirishwa hadi kesho ambapo washtakiwa wataanza utetezi baada ya kula kiapo kilichoshindikana kuliwa leo. Akitoka mahakamani na kupanda karandinga, Zombe alisikika akisema mambo yote kesho na kwamba nchi inaendeshwa kwa utawala wa sheria.

  Wiki iliyopita, mawakili wa pande zote walijenga hoja kuishawishi mahakama kukubaliana na maoni yao, baada ya upande wa mashitaka kumaliza kutoa ushahidi wao.

  Wakati upande wa mashitaka unasisitiza kuwa Zombe na wenzake wana kesi ya kujibu, upande wa utetezi unadai hakuna ushahidi mzito unaowafanya washitakiwa hao wasimame kizimbani kujitetea.

  Zombe na wenzake wanashitakiwa kwa mauaji ya Wafanyabiashara wanne ambao ni Ephrahim Chigumbi, Sabinus Chigumbi ‘Jongo’, Mathias Lunkombe na Juma Ndugu, ambaye alikuwa dereva wa teksi iliyokuwa ikitumiwa na wafanyabiashara hao katika shughuli zao.

  Washitakiwa wengine katika kesi hiyo namba 26/2006 ni Mrakibu wa Polisi Christopher Bageni, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Ahmed Makele, F. 5912 Konstebo Noel Leonard, WP. 4593 Konstebo Jane Andrew, D. 6440 Koplo Nyangelera Moris na D. 1406 Koplo Emmanuel Mabula.

  Wengine ni E. 6712 Koplo Felic Sandsy Cedrick, D. 8289 Konstebo Michael Shonza, D. 2300 Koplo Abeneth Saro, D 9321 D/C. Rashid Lema, D. 4656 D/Koplo Rajab Bakari na D. 1367 D/Koplo Festus Gwabisabi.


  Source:MICHUZI
   
 15. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Jaji wa mahakama ya rufaa Mh.Salum Masati alikuwa anatoa ruling leo kama washitakiwa wana kesi ya kujibu au la sasa nilifikiri kama hawana kesi ya kujibu basi wote watakuwa wameachiwa huru.To the delight of Mr.Zombe's family lakini uchungu kwa wanafamilia ya marehemu wale waliouawa kikatili bila hatia. sheria jamani!
   
 16. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #16
  Feb 9, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Tupeni details zaidi re. Maelezo ya upande wa mashtaka na pia nani wameachiwa huru, na je hao hawakwenda kwenye msitu wa pande etc?
   
 17. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #17
  Feb 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Washtakiwa hao ambao waliondoka mahakama kuu wakiwa watu huru ni mshtakiwa namba 4 Konstebo Noel Leonard, mshtakiwa namba 6 Koplo Nyengelera Morris na mshtakiwa namba 8 Koplo Felix Cedrick.

  Source: MICHUZI
   
 18. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #18
  Feb 9, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mkuu sina haja ya kusema huyo ndugu yangu aliyeachiwa ni nani maana identity yangu yote itakuwa hadharani. Si wajua jinsi ambavyo JF inawindwa?
   
 19. share

  share JF-Expert Member

  #19
  Feb 9, 2009
  Joined: Nov 22, 2008
  Messages: 2,295
  Likes Received: 2,294
  Trophy Points: 280
   
 20. Mr Kiroboto

  Mr Kiroboto JF-Expert Member

  #20
  Feb 9, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
   
Loading...