Zombe ashikwa pabaya, rufaa yatinga leo

Kamanda

Senior Member
Dec 5, 2007
150
176
Mchezo wa siasa waanza.
Baada ya Zombe kutamba jana nyumbani kwake kuwa serikali itapoteza muda na fedha kwa kumkatia rufaa, kwani atashinda, leo serikali imeibuka na kukata rufaa.

Leo jioni, ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) imewasilisha makabrasha kupinga hukumu hiyo katika Mahakama ya Rufani, Dar es Salaam.

Zombe na maofisa wenzake wanane wa Jeshi la Polisi walikabiliwa na kesi ya kuua wafanyabiashara watatu wa madini wa Mahenge, Moro na dereva taksi mmoja wa Dar.

Rufaa hiyo ambayo iliwasilishwa ilielezea sababu za Serikali kukata rufani hiyo dhidi ya maofisa hao wa zamani ambao ni Zombe, Christopher Bageni, Ahamed Makelle, Rajabu Bakari, Philipo Wabisabi, Jane Andrew, Emmanuel Mabula, Michael Shonza na Abeneth Saro.

Serikali imepinga uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kupitia Jaji wa Mahakama ya Rufani, Salum Massati baada ya kumwona aliyekuwa mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Zombe kuwa hana hatia pamoja na kuwa ushahidi wa kimazingira uliotolewa mahakamani hapo ulikuwa ukimgusa moja kwa moja.
 
wasije wakatia aibu, sio wanakata rufaa afu wanashindwa ku prove the case beyond reasonable doubt.
 
wasije wakatia aibu, sio wanakata rufaa afu wanashindwa ku prove the case beyond reasonable doubt.

Wanatafuta kura tu! Bila kukata rufaa wataenda kusema nini huko Mahenge? Lakini sasa wataingia na gia kuwa serikali imekata rufaa na kwamba lazima Zombe atanyongwa. Wakishapata kura zao basi, wanajua hadi 2015 wadanganyika wa Mahenge watakuwa wamesahau tayari!!
 
in short hata wakate rufaa mahakama ya dunia kwa ushahidi ule zombe hafungwi wala hatatiwa hatiani.toka lini ushahidi wa kimazingiza katika kesi ya mauaji unamtia mtu hatiani?Zombe ana haki ya kujigamba kuwa serikali inapoteza muda maana anajua ni upuuzi mtupu
 
Serikali yamfanyia kweli Afande Zombe Tuesday, 06 October 2009 16:43 Rufaa dhidi yake yatinga mahakamani
Ni siku moja baada ya kusema hatishiki
Wamo pia askari polisi wenzake wanane

Na Grace Michael

HATIMAYE Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) amekata rufani dhidi ya Askari Polisi tisa akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Abdalah Zombe ambao waliachiwa huru na Mahakama Kuu kwa kesi ya mauaji hivi karibuni.

Rufani hiyo yenye namba 254 ya mwaka huu ina sababu 11 zinazopinga kuachiwa huru kwa washitakiwa hao ambao wanadaiwa kuwaua kwa makusudi wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge, Morogoro pamoja na dereva texi.

Waliouawa katika tukio hilo ni Ephraim Chigumbi, Sabinus Chigumbi (Jongo), Mathias Lung'ombe na dereva teksi Juma Ndugu wa Manzese. Tukio hilo lilitokea Januari 14, 2006 katika msitu wa Pande, Mbezi Luis, Dar es Salaam.

Sababu zilizowasilishwa na DPP ni kwamba Jaji Salum Massati ambaye ndiye aliyesikiliza kesi hiyo alikosea kisheria katika kujenga na kutoa tafsiri juu ya ushiriki wa wahusika katika kosa la mauaji.

Pia rufani hiyo ilidai kuwa katika mazingira ya kesi hiyo, Jaji alijielekeza vibaya katika kutumia kanuni zinazolinda nia ya pamoja lakini pia alifanya makosa ya kisheria na ukweli katika kujenga na kutafsiri kanuni ya ungamo, hatua iliyosababisha kufikia uamuzi usio sahihi.

Rufani hiyo inadai kuwa Jaji Massati alifanya makosa katika kumwachia huru mshitakiwa wa kwanza ambaye ni Bw. Zombe licha ya kuwepo ushahidi wa kutosha wa kimazingira ambao ungeweza kumtia hatiani.

Tayari Zombe alikaririwa na gazeti moja jana akisema hatishiki kwa rufaa inayokatwa na serikali kwa kuwa inataka kujikosha kwa wananchi kuwa inafanya kazi nzuri, wakati ikijua kuwa wapelelezi wake walikiuka taratibu na kuwa huo ni mwendelezo wa ufujaji wa fedha za walipa kodi.

Kwa upande wa mshitakiwa wa pili ambaye alikuwa ni SP Chrisptopher Bageni, DPP anadai kuwa Jaji alikosea kisheria kumwachia mshitakiwa huyo kwa kuwa kulikuwa na ushahidi wa kutosha ambao uliwasilishwa na upande wa mashitaka.

Sababu za rufani kwa mshitakiwa wa tatu, Bw. ASP Ahmed Makelle, zilidai kuwa yalifanyika makosa na kushindwa kutoa tafsiri na kutumia vizuri kanuni ya kukutwa na mali ambapo kwa mujibu wa ushahidi, mshitakiwa huyo ndiye aliyehusika katika ukamataji wa marehemu hao.

Rufani hiyo pia inadai kuwa Jaji alishindwa kutoa sababu za washitakiwa wa WP Jane na D.2300 D/CPL Sarro ni waathirika wa kimazingira bila kueleza ni jinsi gani waliathirika kimazingira.

Washitakiwa wengine ni D.1406, CPL Mabula na D8289 PC Shonza ambao sababu zilizomo kwenye rufani hiyo zinadai kuwa yalifanyika makosa ya kisheria katika kuwaachia kwa kuegemea katika utetezi wa kutokuwepo kwenye tukio.

Kuhusiana na mshitakiwa D.4656 D/CPL Rajab ambaye katika utetezi wake alielezea namna marehemu hao walivyouawa, rufani hiyo inasema yalifanyika makosa makubwa katika kumwachia kwa kuwa kulikuwa na ushahidi mzito dhidi yake.

Aidha, ilielezwa kuwa Jaji alishindwa kuwatia hatiani Bw. Zombe na mshitakiwa wa tisa D.1367 D/CPL Gwabisabi kwa kuzingatia kifungu cha 300(2) cha CPA lakini pia yalifanyika makosa katika kufanya uchambuzi wa ushahidi uliotolewa mbele yake hali iliyosababisha kuwepo mkanganyiko katika hukumu hiyo.

Washitakiwa hao waliachiwa huru na Mahakama Kuu ya Tanzania ambayo ilisema upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha bila kuacha shaka yoyote katika mashitaka yaliyokuwa yakiwakabili.

Kuachiwa kwao huru kulizua mtafaruku mbele ya jamii ambayo ililalamikia kitendo cha kuachiwa kwa washitakiwa hao.

Source: Majira
 
hawa nao wanatupotezea muda wetu na kupumbaza akili zetu tu ,wameshindwa kufanya vitu vya maana sasa wanaanza kutuletea longolongo --boring
 
Daylight cheating.

Ni ushahidi gani ulioshindikana wakati wa kesi ya msingi, na ambavyo kwa sasa vimepatikana?

Hili suala ni 100% la kisiasa!

Mgombea wa upinzani aende haraka sana Mahenge...wanaJF wapenda siasa mko wapi...nafasi ya bure hiyo!
 
Wanatafuta kura tu! Bila kukata rufaa wataenda kusema nini huko Mahenge? Lakini sasa wataingia na gia kuwa serikali imekata rufaa na kwamba lazima Zombe atanyongwa. Wakishapata kura zao basi, wanajua hadi 2015 wadanganyika wa Mahenge watakuwa wamesahau tayari!!

Hii ni kweli Kabisa nakukubali. Siunakumbuka kuwa hata jK mwenyewe alisema ili kuwadanganya wapiga kura kuwa wanapigana na hiyo hali. lakini ni uhuni mtupu kwani ukweli wanaujua na kile ni kitu ambacho walipewa mapema. na wameamua kutuzingua tu. lakini Unajua Target yao ni nzuri maaana wanajua kwa watu wao ni wakudanganyika hivyo lazima iwe hivyo. Tuombe Mungu wadanganyika waamuke ili tujenge Tanzania Mpa kama itawezekana
 
Mambo ya kukurupuka tena haya
hawajakurupuka, wanajua wanachokifanya. Mi nadhani nchi hii kna watu wengi wajanja wanaoibua mambo ilimradi tu wajipatie kitu fulani. Hivi hawa mawakili wanaosimamia hizi kesi, kama kesi zenyewe zitakwisha unafikiri watakula wapi. nina wasiwasi nao pia. lkini ni kwamba Nchi inaendeshwa kihuni na watu kibao wasikaji zetu.
 
Mchezo wa siasa waanza.
Baada ya Zombe kutamba jana nyumbani kwake kuwa serikali itapoteza muda na fedha kwa kumkatia rufaa, kwani atashinda, leo serikali imeibuka na kukata rufaa.

Leo jioni, ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) imewasilisha makabrasha kupinga hukumu hiyo katika Mahakama ya Rufani, Dar es Salaam.

Hongera sana Jaji Massati. Hakika Zombe na wenzake hawana hatia. Inawezekana Zombe na wenzake wanamjua aliyefyatua risasi na kuwaua wale wafanyabiashara wa Mahenge. Lakini pale Mahakama Kuu muuaji hakuwepo kutoka na usanii wa Police investigators. Wanalindana hawa. Sasa DPP anakata rufaa ambayo aimleti mtu aliyefyatua risasi? (I'm doubtful if the DPP is serious on this case). Definately the appeal will be dismissed by the Court of Appeal.
 
Maneno ya Zombe hayo alipohijiwa na Tz Daima!

"Nasikitika sana serikali imenipotezea muda mwingi gerezani, ila hivi sasa namuachia Mungu, naamini kwa wakati wake atashughulika na wale wote walioshiriki kuniangamiza, kwa sababu fitna hizo za kunibambikia kesi ya mauaji zilikuwa kubwa mno"

"Serikali iache mchezo wa kubambika watu kesi kwa visasi na kutaka umaarufu wa kijinga, kwani mwisho wa ubaya ni aibu," alisema Zombe kwa hisia, huku akilionyesha nyaraka mbalimbali gazeti hili."

"Ifikapo Septemba 21, mwaka huu, nitakuwa natimiza umri wa miaka 55 ambapo kwa hiari yangu mwenyewe pasipo kushawishiwa na mtu yeyote, nimeamua nistaafu kwa hiari, hasa nikizingatia matatizo ambayo nimeyapata kwa kubambikiziwa kesi ya mauaji na huku taratibu za kisheria zikikiukwa wazi wazi kwa hila na kunikomoa"
 
Maneno ya Zombe hayo alipohijiwa na Tz Daima!

“Nasikitika sana serikali imenipotezea muda mwingi gerezani, ila hivi sasa namuachia Mungu, naamini kwa wakati wake atashughulika na wale wote walioshiriki kuniangamiza, kwa sababu fitna hizo za kunibambikia kesi ya mauaji zilikuwa kubwa mno"

“Serikali iache mchezo wa kubambika watu kesi kwa visasi na kutaka umaarufu wa kijinga, kwani mwisho wa ubaya ni aibu,” alisema Zombe kwa hisia, huku akilionyesha nyaraka mbalimbali gazeti hili."

"Ifikapo Septemba 21, mwaka huu, nitakuwa natimiza umri wa miaka 55 ambapo kwa hiari yangu mwenyewe pasipo kushawishiwa na mtu yeyote, nimeamua nistaafu kwa hiari, hasa nikizingatia matatizo ambayo nimeyapata kwa kubambikiziwa kesi ya mauaji na huku taratibu za kisheria zikikiukwa wazi wazi kwa hila na kunikomoa"

Ifikapo September 21??????? leo lini na hayo maneno ameyasema lini?

Waandishi wa kibongo bwana!
 
Hakuna jipya ni kujikanyaga tu. Serikali haiwezi shinda hata ikifanya nini.

Zombe ndugu yangu usitie shaka huna kesi jipumzikie tu. Serikali ilichemsha katika kufile case yako.
 
Sasa sie tusifanye hukumu kwa kutumia hukumu ya kwanza, wamesema wamekata rufana, si tuwaachie wajieleze mahakamani kwanza? Tusiwe mahakimu wenye jazba. Shida ya sheria ni namna unavyoiwasilishia hoja na wala sio inavyondikwa kwenye vitabu. Sie ndio twaanza longolongo. Kama wangekaa kimya bado tungewazodoa. Si heri wajianike nyuchi zao tuone akili zao zilivyo?

Hata kwenye kampeni usijefanya makosa kusherehekea ushindi ati kwa kuwa mkutano uliohutubia watu walikuwa wengi na walikushangilia sana hata kukubeba mzobemzobe. Ngojea kura zihesabiwe ndipo upate sababu ya kushereheka kwa hakika.


Leka
 
[
Kama wangekaa kimya bado tungewazodoa. Si heri wajianike nyuchi zao tuone akili zao zilivyo?

Leka[/QUOTE]
Kazi kwelikweli hapa!
 
Zombe anajiamini nini???? Anaweza asiwe na hatia ya mauaji lakini ana makosa mengi ambayo kama mashitaka yangeandikwa vizuri yangemtia hatiani na kufungwa lao miaka kadhaa. Mfano uzembe kazini kutojua watu wake wanamdanganya, kushiriki kusaidia uhalifu, wizi - fedha walizonyang'anywa marehemu zilienda wapi kama sio mwizi.

Sio kawaida DPP na wanasheria walio chini yake kufungua shitaka moja tu la mauaji kwa kesi iliyokua na mlolongo wa matukio mengi vile na iliyo husisha watu wengi vile kila mmoja na sehemu yake. Huu ulikua usanii toka mwanzoni na DPP na Zombe mwenyewe wanajua.

Hatudanganyike. Ni kweli wanapoteza hela za umma bure kama alivyosema Zombe.
 
Serikali inatafuta kura za mwakani kwa kutumia mgongo wa Zombe. Tangia mauaji yalipofanyika, serikali ilikaa kimya na kulala bila kufuatilia kiundani yaliyo tokea, hadi vyobo vya habari vilipo waamsha kwenye usingizi huo na kuunda tume.
Zombe anajiamini kwani kwa sehemu fulani anaifahamu serikali ya ccm na maovu walio nayo, hivyo ni vigumu kwake kutiwa hatiani kwani mchezo ulisha chezwa tayari.
La msingi ni pesa walizochukua wazirudishe kwa jamaa za wafiwa, kwani wasipozirudisha, basi serikali itaonekana kuwa iliwatuma wauaji hao. Pia wana maenge wasiwape kura chama cha ccm.
 
Back
Top Bottom