Off GridElectric Company tunatafuta wakala wa mauzo

Jul 28, 2015
38
13
Mwenye uelewa na hii kampuni tuelekezane na hizi fursa

Wakala Mauzo(Sales)

Details:

Employer Name: Off.Grid:Electric- Zola

Organization Type: Company

Role: Entry Level

Position Type: Internship

Location: Arusha Mjini

Application Deadline: 06-11-2016

Listed on: 01-11-2016

Description:

Application Instructions

Je unataka kuendesha maisha yako mwenyewe? ZOLA inakupatia fursa hiyo. Mwezi uliopita, Wakala wetu wa Mauzo alifanikiwa kupata zaidi ya shilingi milioni 2, wewe pia unaweza kufanikiwa hivyo.Tutakupatia mafunzo, unachohitaji ni kua na tabia nzuri, uwezo wa kujifunza haraka na moyo wa kujituma.

Off Grid Electric ni kampuni inayokua kwa kasi, inatoa huduma za umeme kwa gharama nafuu na za kuaminika katika maeneo yanayokosa huduma hizo. Kampuni inatumia nishati mbadala kutoa huduma ya umeme wa muda mrefu kwa wateja ambao wameathirika kutokana na huduma ghali na isiyokua ya uhakika, au hawajafikiwa kabisa na huduma ya umeme.

Makaomakuu ya kampuni yako Arusha Tanzania. Mpaka sasa Zola imetoa huduma ya umeme wa jua kwa zaidi ya kaya laki moja nchini Tanzania. Kwa sasa, tunatafuta wajasiliamali wanaotaka fursa ya kuimarisha biashara na kubadilisha maisha yao. Tunatafuta watu wa kujiunga na timu yetu
ya mauzo kama mawakala kwenye maeneo yafuatayo;

•Morogoro:
Mvomero,Ifakara,Rural,Bagamoyo,Mkuranga, and Kilosa.

•Mbeya: Kyela and Chunya.

•MbeyaPwani: Mkuranga and Bagamoyo

Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kufanya maombi;

•Uwe unaishi au uwe tayari kuishi kwenye wilaya au kata uliyochaguliwa.

•Uwe na elimu ya kuanzia form four na kuendelea.

•Uwe na umri kati ya miaka 18-35.

•Ni lazima ujue Kusoma na Kuandika.

•Ukifanikiwa kupita kwenye usahili, utaajiriwa kama Wakala mauzo.

•Wakala ambaye atakua na idadi kubwa ya mauzo kwa miezi mitatu mfululizo,atapata nafasi ya kuajiliwa kama mfanyakazi wa kudumu,atalipwa mshahara wa awali pamoja na mafao mengine kama fao la matibabu na mfuko wa jamii.

•Ukishathibitishwa kua wakala wa mauzo,utaitajika kuwa na shillingi 200,000/- itakayo kuwezesha kununua simu pamoja na salio la Zola.

•Uwe na account ya m-pesa.

Hatua zifuatazo zitafanyika wakati wa usahili ili kupata wafanyakazi sahihi;

•Usahili kwa njia ya simu; hii itafanyika kwa watu wote watakaokua wamejisajili kwenye mtandao au kwa njia ya simu.

•Usahili wa ana kwa ana; hii itafanyika kwa wale watakaokua wamepita usahili kwa njia ya simu.

•Wiki moja na nusu ya mafunzo ya mauzo; hii itakua kwa wale wote waliopita usahili wa ana kwa ana.

Ili ufanikiwe kwenye mambo yaliyotajwa hapo juu, tafadhali fuatilia hatua zifuatazo;

•Kopi anuani hii Sales Representatives Application Form kwenye kisakuzi (browser) cha kompyuta yako na kisha ujaze form.

•Mwisho wa kujaza form hii ni tarehe 6/11/2016. Hatutapokea maombi yatakayochelewa.

•Iwapo utashindwa kujisajili mwenyewe, lakini bado unahitaji kazi hii, Tuma SMS kwenda 0769 046216 ikiwa na ujumbe ufuatao “Majina yako mawili,mkoa,wilaya na kata unayotokea, namba ya simu, pamoja na umri.”

Baada ya kumaliza usajili, mwakilishi kutoka idara ya rasilimali watu atakujulisha utaratibu utakaofatia.
 
Kwa mlio wafanyanyia vijana na mabinti zetu sitaman tena kuna vijana wanahangaika na hii kampuni uupuzi mtupu
 
Jamani ni kweli Zola ndo Mpower nimeingia kwenye web yao nikajiridhisha ni watu Hawa tuchangamkie kaz hii jaman
 
Jaman naomba kujua sisi wa MWANZA si tunaweza kuapply? Coz naona wametaja mikoa tele ila MWANZA sijaona nataman nipate huku huku MWANZA Mungu nisaidie
 
kazi za siku hizi jamani utoe pesa kwanza ndo upate kazi. kama mtu hana hiyo laki 2 atafanyaje
 
Hiyo laki mbili utatoa baada ya kufaulu usahil na kusain mkataba wa kaz na hiyo Pesa ni kwaajili UA cm na salio LA Zola so sio kama wanaichukua no ni kwaajili ya kufanyia kax
 
Back
Top Bottom