Zoezi la Utoaji wa Vitambulisho vya Taifa: Waziri Simbachawene asema NIDA wanafanya kazi, tatizo lipo kwenye mtambo unaozalisha Vitambulisho vichache

JMP Mchungu

Member
Jun 30, 2015
49
125
Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini, George Simbachaweme amesema Mamlaka inaendelea kugawa vitambulisho katika baadhi ya maeneo licha ya kuwa vinatengenezwa kwa uchache.

Amesema kwa mujibu wa taarifa, ndani ya mwezi wa Mwezi wa Novemba na Desemba mwaka 2020, vitambulisho 20,000 vimepelekwa Kongwa, na vingine 20,000 Wilaya ya Iramba, Kilindi napo 20,000 na Temeke imepelekewa vitambulisho zaidi ya 20,000.

Amesema NIDA bado wanaendelea kufanya kazi na tatizo lililopo ni kwamba mtambo unazalisha vitambulisho vichache.

Hata hivyo, ameeleza kuwa, hadi kufikia mwisho wa mwaka hakuna Mtanzania ambaye hatokuwa na vitambulisho, na wanakusudia kuanza kuchapisha vitambulisho vingi kwa wakati mmoja kuanzia mwisho wa mwezi huu wa Januari.


---
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema Januari hii ndiyo mwisho wa tatizo la uhaba wa vitambulisho vya Taifa (Nida), litakapopatiwa ufumbuzi na kuanza kutolewa kwa wingi.

Kiongozi huyo amesema kilichochelewesha kufikia hatua hiyo mapema ni mchakato wa manunuzi ndani ya Serikali ambao ulikuwa na vipengele vingi.

Alisema mashine hiyo hainunuliwi ikiwa imefungwa pamoja, bali kila sehemu ya utendaji kazi ndani yake inakuwa na mkataba wake na itafungwa kati ya Januari 20 hadi 25, 2021.

Waziri Simbachawene alitoa kauli hiyo jana alipoulizwa na Mwananchi kuhusu lini tatizo la uhaba wa vitambulisho litakwisha na nini chanzo chake.

Msingi wa swali hilo ulitokana na ukweli watu waliojiandikisha wamekuwa hawapati vitambulisho kwa muda badala yake wanapewa tu namba, huku maeneo mengine hata namba zenyewe hawajazipata.

Simbachawene alikiri kuwepo kwa tatizo hilo akisema hata yeye linamkwaza kuona Watanzania wanakosa vitambulisho ambavyo ni muhimu, lakini akataja changamoto ambazo zimekwamisha.

“Mashine tuliyo nayo inafanya kazi kizamani sana, kumbuka tunazalisha vitambulisho 2000 kwa siku kiasi ambacho ni kidogo ukilinganisha na idadi ya Watanzania waliotambuliwa, lazima tubadilike,” alisema Simbachawene.

Waziri alisema idadi ya Watanzania waliokuwa wametambuliwa hadi mwishoni mwa mwaka 2020 walikuwa 18.5 milioni, lakini waliopewa vitambulisho walikuwa 6.3 milioni tu na kwamba watu 12.2 milioni walikuwa hawajavipata.

Suluhu ya tatizo hilo alisema ni mashine mpya itakayofungwa ambayo itakuwa na uwezo wa kuzalisha vitambulisho vingi kwa wakati mmoja.

Alisema mkataba walioingia wakati wa kununua mashine mpya, ulionyesha ingezalisha vitambulisho 50 kwa dakika, lakini matokeo katika majaribio iliweza kuzalisha vitambulisho 45 kwa dakika, hivyo ilibidi kurudi upya katika mkataba jambo lililochukua muda.

Kutokana na malengo hayo mashine hiyo itazalisha vitambulisho 43,200 kwa siku, ikiwa ainaafanya kazi kwa saa 16 kila siku. .

Na ikiwa watafunga mashine yenye uwezo wa kuzalisha vitambulisho 45 kwa dakika na ikafanya kazi saa 16 yaani nane mchana na nane usiku kama alivyoeleza, itachukua siku 283 ambayo ni sawa na miezi 10 kumaliza vitambulisho kwa Watanzania waliosalia.

Hata hivyo, ikiachwa mashine ya zamani kuendelea na uzalishaji wa vitambulisho 2,000 kwa siku, itachukua siku 6,250 ambazo ni sawa na miaka 17 au miezi 204 ili Watanzania 12.2 milioni waweze kupata vitambulisho vyao.

Waziri alisema licha ya kuwa hawajafunga mashine mpya, uzalishaji wa vitambulisho haujawahi kusimama na hivi karibuni wametoka kupeleka vitambulisho 20,000 katika Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga na maeneo mengine wanaendelea kupeleka kadri wanavyochapisha.

Akijibu kuhusu malalamiko yanayotolewa ikiwemo taarifa kwenye mitandao kuhusu wananchi wa Karagwe kupata shida ya kupewa namba, alisema taarifa hizo anazo na kwamba anafuatilia kwa wahusika ili aweze kulifanyia kazi.

Mapema mwaka jana akiwa na siku chache tangu alipoteuliwa kwa wadhifa huo, Simbachawene alitangaza kuwaondoa baadhi ya watumishi katika mamlaka ya vitambulisho aliosema hawaendani na kasi inayotakiwa na mara kadhaa walitajwa kuwa na lugha chafu.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Simbachawene alisema jumla ya Watanzania 21,823,026 walikuwa wamejitokeza na kujisajili hadi Machi 27, 2020 kati ya watu 27,796,983 waliotarajia kusajiliwa.
 
Wakuu hii ni big shame dor this government yani mm nimejiandisha 2017 mpaka leo naambiwa kitambulisho hakijatoka, Hii inamaanisha kuwa serikali yetu ilikuwa haikujipanga kwa zoezi.

Wakaingiza siasa ambayo sasa inaigarimu taifa. Ni kwa nini wqsingetuambia tuchangie hela walau hata percentage kuliko kusema ni bure wqkati, hatukuwa na uwezo huwo.

Duuuh the drama country.
 
Huyu jamaa last year si alituambia wamenunua mashine kubwa tatizo wataalamu wa kuifunga walishindwa kuja sababu ya corona?
Sasa kesha sahau ana leta new story.

Tuna miaka minne hatuna vitambulisho. Itawezekanaje kuvipata Watanzania wote kwa kipindi cha mwaka mmoja?? kweli ni mitano tena
 
Wakuu hii ni aibu kubwa kwa hii serikal ya wanyonge.

Yaani nimejiandikisha 2017 mpaka leo naambiwa kitambulisho hakijatoka,

Hii inamaanisha kuwa serikali yetu ilikuwa haikujipanga kwa zoezi hii la kutoa vitambulisho bila malipo wakuu,

Wakaingiza siasa ambayo sasa inaigarimu taifa. Ni kwa nini wasingetuambia tuchangie hela walau hata percentage kidgo ili kuraisisha shughuli hii ifanyike kwa ufasahaa kuliko hii uhuuni inayoendeleya kufanyika.

Duuuh the drama country.
 
Lazima kuna tatizo,,mtambo kama mtambo hauwezi kushindwa kuzalisha vitambulisho milion 50 kwa miaka 5.

Either hivyo vitambulisho ni unique sana kiasi kila kutambulisho kinatengezwa na wahandisi 10,

Au wanatumia typewriter..
 
Ni kwanini mtambo uzalishe vitambulisho vichache wakati mnunuzi alikua anajua idadi ya Watanzania?
Je ni nani ameshachukuliwa hatua za kimahakama kwa kosa la kununa mtambo usio na sifa?

Kwanini vitambulisho vya kura vilitoka papo kwa papo ila hivi vya nida imekua ni story??

Naamini vitambulisho vya Nida vingetumika kupiga kura mwanasiasa angehakikisha anaweka bajeti kubwa ya kupata mtambo wenye sifa ya kuzalisha vitambulisho vingi na kila mtu angekua nacho mkononi.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini, George Simbachaweme amesema Mamlaka inaendelea kugawa vitambulisho katika baadhi ya maeneo licha ya kuwa vinatengenezwa kwa uchache. Amesema kwa mujibu wa taarifa, ndani ya mwezi wa Mwezi wa Novemba na Desemba mwaka 2020, vitambulisho 20,000 vimepelekwa Kongwa, na vingine 20,000 Wilaya ya Iramba, Kilindi napo 20,000 na Temeke imepelekewa vitambulisho zaidi ya 20,000...
Katika utaratibu ambao serikali ya awamu hii inachemsha kuhusu hili la NIDA ambalo ni zoezi lililojaa ubaguzi na uzembe wa kila namna mfano sisi tulisajiliwa Novemba 2017 mpaka sasa hivi tunatumia namba tu za NIDA vitambulisho hakuna je hapo kuna utendaji yakinifu au ni ubabaishaji?
 
Lazima kuna tatizo,,mtambo kama mtambo hauwezi kushindwa kuzalisha vitambulisho milion 50 kwa miaka 5..
Either hivyo vitambulisho ni unique sana kiasi kila kutambulisho kinatengezwa na wahandisi 10,,
Au wanatumia typewriter..
Kwani watanzania wote Wana miaka zaidi ya 17 Hadi useme vitambulisho 50 milion?
 
Wakuu hii ni big shame dor this government yani mm nimejiandisha 2017 mpaka leo naambiwa kitambulisho hakijatoka,
Hii inamaanisha kuwa serikali yetu ilikuwa haikujipanga kwa zoezi...
Sasa si bora hata wew umepata hyo namba ya nida wenzio hata namba hatujapata mpaka leo tunasubiria tu ufike mda tuambiwe ni wanyarwanda au wakimbiz wakokote tuondoke
 
Mtambo unazalisha vitambulisho vichache halafu mwisho wa mwezi huu eti vitazalishwa kwa wingi ...,. INAWEZEKANAJE?
 
Novemba na Desemba mwaka 2020, vitambulisho 20,000 vimepelekwa Kongwa, na vingine 20,000 Wilaya ya Iramba, Kilindi napo 20,000 na Temeke imepelekewa vitambulisho zaidi ya 20,000
Huu utani sasa, vitambulisho 20,000 kwa wilaya ni tone kwa bahari.. kwa spidi hiyo itapita miaka bila kukamilika
 
Binafsi nimeshaacha kufuatilia suala la kitambulisho cha NIDA. Natumia namba ya JKT na sura yangu ndio kitambulisho tosha
 
sasa si bora hata wew umepata hyo namba ya nida wenzio hata namba hatujapata mpaka leo tunasubiria tu ufike mda tuambiwe ni wanyarwanda au wakimbiz wakokote tuondoke
Ucjali kwasasa niraia Safi tu utapo anza kutukosao tu hapo Sasa ndio tutakuomba kitambulisho chako na babaako babuyko sijui nanani mwingine
 
Mengine ni ya aibu, wakaprint kule walikochapia makaratasi ya kupigia kura.
 
Watu watakuja kupata vitambulisho vikiwa vimeexpire.
Awamu ya Tano hakuna linalokamilika kwa wakati na smoothly kwa sababu ya kukurupuka kabla ya kujiandaa na mbaya zaidi Vitambulisho vinatolewa kuanzia tarehe mwananchi alipojisajiri na vinatumika kwa miaka 10 tu ikiwa na maana kuna watu watatumia Vitambulisho vyao kwa miaka 5 tu ya mwisho, mitano mingine ya kwanza ikiishia NIDA. Hii ndo "Hapa Kazi Tu" inayoimbwa kila siku!
 
Huyu jamaa last year si alituambia wamenunua mashine kubwa tatizo wataalamu wa kuifunga walishindwa kuja sababu ya corona?
Sasa kesha sahau ana leta new story.

Tuna miaka minne hatuna vitambulisho. Itawezekanaje kuvipata Watanzania wote kwa kipindi cha mwaka mmoja?? kweli ni mitano tena
Mimi nimewahi kuambiwa na NIDA wenyewe kuwa vitambulisho vinatengenezwa NJE ( something kama Malaysia ) ndio maana vya kusubiri.

Wewe hujiulizi, kama vitambulisho vya "KULA" ni papo hapo, why NIDA iwe mlolongo ??

Hapo ndio utashangaa, hata kijijini kuwe na umbali kiasi gani, barabara mbovu na changamoto lukuki lazima Masanduku ya kupigia "KULA" yatafikishwa ila Maendeleo ya huduma za jamii utasubiri saaana.
 
Back
Top Bottom