Uchaguzi wa Marudio wa Ubunge majimbo ya Kinondoni na Siha, Udiwani Kata 8: CCM yanyakua majimbo yote!

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,801
11,961
Uchaguzi wa Marudio katika majimbo ya Kinondoni Jijini Dar na Siha mkoani Kilimanjaro pamoja na kata 10 za unafanyika leo hii.

UPDATES: CCM imeshinda majimbo ya Siha na Kinondoni







Kata hizo ni kama ifuatavyo, wilaya zinakopatikana katika mabano

Mkoa wa Mwanza - Isamilo (Nyamagana), Kanyelele (Misungwi)

Mkoa wa Dodoma- Manzese (Chawino) Kimagai (Mpwapwa)

Mkoa wa Tanga- Madanga (Pangani)

Mkoa wa Kagera - Buhangaza (Muleba) - Bi. Jenitha Tibihenda wa CCM ameshinda kwa kura 883 huku CHADEMA ikipata kura 825 na NCCR 16

Mkoa wa Singida- Mitunduruni (Singida)

Mkoa wa Kilimanjaro- Kashishi, Gararagua, Donyomuruak (Siha)


Fuatilia hapa kujua kinachojiri...

UPDATES;

>> 0800HRS
Mawakala wamezuiwa kuingia vituoni Mpaka Muda huu kwa kukosa barua za msimamizi na ni kutoka vyama vyote

>> 0900HRS
Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Maulid Mtulia, amepiga kura asubuhi hii katika kituo cha Friends Corner huko Kata ya Ndugumbi
mtulia.jpg


>> 0945HRS
Mawakala 67 kati ya 70 wa Usimamizi wa uchaguzi mdogo wa Chama cha Wananchi (CUF ), Jimbo la Siha watolewa vituoni kwa madai kuwa barua zao za kiapo zimesainiwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo pekee badala ya Hakimu

>>1000HRS
Mawakala mablimabli katika vituo mbalimbali vya kupigia kura wametolewa au kuzuiwa kuingia vituoni humo kwa sababu mbalimbali. Moja ya sababu hizo ni inasemekana ni fomu zao kutokidhi vigezo

>>1100HRS
SIHA: Zoezi la upigaji kura linaendelea, baadhi ya wananchi wamelalamikia kutoyaona majina yao katika orodha ya wapiga kura, ili waweze kupata haki yao ya msingi ya kupiga kura.

===
Wasimamizi wa uchaguzi katika Kituo cha Shule ya Msingi Ndugumbi wakisubiri wapiga kura katika kituo hicho. Kumekuwa na muitikio mdogo wa wapiga kura katika vituo vingi jimbo la Kinondoni.
DWOOLyzWkAAwzG1.jpg

===

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi, Jaji Semistocles Kaijage ametembelea Kituo cha kupigia kura cha Leaders Club asubuhi hii Amesema vituo vimefunguliwa kwa wakati Hajapokea malalamiko yoyote hadi sasa
DWOFdDaW4AEdmys.jpg


===

Salum Mwalimu alalamika mawakala wa Chadema kucheleweshwa


Mgombea wa ubunge jimbo la Kinondoni kupitia Chadema, Salum Mwalimu amelalamikia uchaguzi huo kuwa mawakala wa chama hicho wamezuiwa kuingia katika vituo vya kupigia kura kwa wakati.

Mwalimu alitolea mfano Kata ya Hananasifu kuwa mawakala hao wameingia saa 2 asubuhi wakati vituo vyote 613 vya kupigia kura vimefunguliwa saa 1 asubuhi.

Mwalimu ambaye alitembelea kituo cha Hananasifu B, amesema mawakala hawa wamezuiwa baada ya kuelezwa kwamba hawana fomu za halmashauri na wengine zile za kiapo

"Cha ajabu nimeingia kituo kimojawapo halafu wakala wa chama cha UMD anazo barua zote tangu saa 12 asubuhi wakati huohuo wakala wa Chadema hana barua na nilipohoji wananiambia mbona wakala wa CCM pia hana barua na hajaingia,” amesema Mwalimu

"Sasa mtu anapoanza kukuuliza mbona na wa CCM hana unaanza kujiuliza maswali mengi kwanini? Mle ndani walivyokaa wamejipanga kufanya wanachokifanya na wao wanajua wanafanya kazi kwa maelekezo ya nani.”



====

Baadhi ya mawakala katika eneo la kata ya Tandale Dar es Salaam.wamelalamikia kitendo cha kutolewa nje ya vituo kwa kile walichoambiwa kuwa hawatambuliki, Huku wao wakidai kuwa wanavigezo vyote.

DWOLZ4wW0AEM1AR.jpg

====

Baadhi ya mawakala katika eneo la Makumbusho Dar es Salaam wamezuiwa kuingia katika vituo vya kupigia kura huku wengine wakiingia kwa kuchelewa, Ambapo Msimamizi wa Uchaguzi wa eneo hilo amesema mawakala hao walizuiliwa kwasababu walikuwa hawana barua za utambulisho.

DWOQ_YQWAAI-dkc.jpg

===

Licha ya zoezi la upigaji kura katika uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Siha Kilimanjaro kwenda vizuri, baadhi wananchi wamelalamikia kutoyaona majina yao katika orodha ya wapiga kura,ili kupata haki ya msingi ya kupiga kura.

siha.jpg

====
Mgombea ubunge Jimbo la Siha (Kilimanjaro) kwa tiketi ya CUF, Tumsifueli Mwanry amepiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Moniko

UCHAGUZI 4.jpg


-------------------------------------------------
Mawakala wazidi kukwama, ufafanuzi watolewa


Baadhi ya mawakala hao katika kituo cha Lasko kilichopo kata ya Tandale wamezuiwa kwa madai kuwa hati zao za uthibitisho walizopewa zimekosewa.

Msimamizi wa mawakala wa CUF kata ya Tandale, Abdul Zain amesema wamefika vituoni tangu saa 12 asubuhi lakini mawakala wao wamezuiwa kuingia ndani ya vituo hadi hati zao zitakapobadilishwa.

Amesema kuwa wamefuatilia suala hilo ofisi za Kagurumjuli na kupewa fomu nyingine ambazo pia zimekataliwa.

Ufafanuzi watolewa
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kinondoni , Aron Kagurumjuli amesema uchaguzi huo unakwenda vizuri.

Kagurumjuli amesema mawakala wengi hawakuwa na barua kutoka NEC zinazowatambulisha kuwa ni mawakala ambazo walitakiwa kupewa na viongozi wa vyama vyao na badala yake wanatumia barua za viapo alizodai kisheria haziwezi kuwa utambulisho pekee wa kuwa mawakala.

Amefafanua kuwa barua hizo za viapo hazitumiki kuwahalalisha, kwamba vituo vyote katika kata tano wameshatatua tatizo hilo.

“Wakala anapaswa kuapa kwanza na barua ya kiapo napaswa kuwa nayo mimi ili wakifanya kosa niwachukulie hatua. Kiapo si mali yao ndiyo maana tuliwapa nakala, hakuna sheria ya kupewa barua ya kiapo kuna sheria inayosema wakala ataapa siku saba kabla ya uchaguzi na ndivyo ilivyofanyika,” amesema.

“Barua ya utambulisho ndiyo kitu muhimu wanapaswa kuwa nazo ambazo zimetolewa na ofisi ya Mkurugenzi. Barua ya kiapo siyo suluhisho la kuingia nayo kwenye kituo ila barua ya utambulisho ndiyo inahusika.”

Kuhusu matokeo kutangazwa amesema, “Tunatarajia hadi saa sita usiku matokeo yatakuwa yameshajulikana iwapo kura zitapigwa vizuri na kuhesabiwa bila vurugu.”



====================


Salum Mwalimu asema wasiamizi wa uchaguzi wanataka kuwaondoa mawakala wotewa CHADEMA vituoni

Mgombea wa Ubunge wa CHADEMA, Salum Mwalimu amelaumu wasimamizui wa uchaguzi kuwaondoa vituoni mawakala wa CHADEMA kwa madai kuwa viapo vyao ni feki na kuhoji, wanataka wakavithibitishe viapo vyao wapi wakati wao ndio wangepaswa kumpigia mkurugenzi simu na kuhakiki?

Ameendelea kusema asubuhi walipofanya hivyo walitegemea wangefanikiwa kwa kiasi kikubwa lakini wameona mafanikio sio makubwa na wamepanga kuwaondoa vituoni mawakala wa CHADEMA

Sanduku la kura ladaiwa kuondolewa na polisi kituoni kisha kurudishwa

Salumu Mwalimu pia ameeleza pia kuna kituokimoja Idrissa polisi wameondoka na sanduku la kupigia kura na kisha kulirudisha kituoni, ila bado hawajathibitisha taarifa hizo

Pia amesema Polisi wamepanga kufanya vurugu wakati wa majumuisho ili kuwaondoa mawakala wa CHADEMA waliopo vituoni



=========================

Wananchi wadai wameshuhudia Sanduku la kura likitolewa kituoni na kisha kurudishwa

Hali ya sintofahamu imeibuka muda huu katika kituo cha Idrisa kata ya Magomeni baada ya wananchi kudai kuwa kuna mtu ametoroka na sanduku lenye kura.

Wakazi hao ambao hawakutaka kutaja majina yao kwa kuhofia kukamatwa wameieleza MCL Digital kuwa wana uhakika sanduku hilo limechukuliwa na kurejeshwa.

"Kuna gari ilikuja ikaegeshwa pale jirani kabisa na walipo askari halafu ghafla jamaa
mmoja akashuka kuzuga zuga hatimaye akanyakua sanduku na kutokomea nalo," amesema mmoja wa wananchi hao.

Hata hivyo msimamizi wa uchaguzi wa kituo hicho, Zuhura Mohamed amekanusha kutokea kwa tukio hilo.

"Hakuna kitu kama hicho , mambo yamekwenda vizuri, vituo vilifunguliwa kwa wakati na watu wameonyesha kujitokeza ingawa kasi yao si kubwa sana. Tunaamini wataongezeka,” amesema.

Salum Mwalim akamatwa na Polisi

Mgombea ubunge Kinondoni (Chadema), Salum Mwalimu amekamatwa na polisi kituo cha kupigia kura cha Idrisa kata ya Magomeni baada kugoma kuondoka kituoni

Salum Mwalimu akaizozana na Polisi kituo cha kupigia kura



Salum Mwalimu akiwa amepakiwa katika gari la polisi



===============

Wasimamizi wa uchaguzi mdogo Jimbo la Kinondoni wakisubiri wapiga kura katika kituo cha Mabatini Kijitonyama jijini Dar es Salaam, bado muitikio wa wapiga kura katika uchaguzi huo ni mdogo

wala kuku.jpg


=====================
Salum Mwalimu ameachiwa na jeshi la polisi baada kukamatwa muda mfupi uliopita
=========

Updates: Matokeo ya Ubunge Kinondoni, Mtulia anaongoza
Katika matokeo hayo, Mtulia anafuatiwa na mgombea wa Chadema, Salum Mwalimu huku wa CUF, Salum Rajab Juma akishika nafasi ya tatu lakini kwa tofauti kubwa ya kura.

Baadhi ya matokeo hayo ni kama ifuatavyo; Kituo cha Mbuyuni 3 Kata ya Tandale, Mtulia amepata kura 53, Juma 3 na Mwalimu 18.

Kituo cha Mashuka 2 Kata ya Tandale, Mwalimu amepata kura 16, Juma 7 na Mtulia 53.

Kituo cha Mashuka 1 Kata ya Tandale, Mtulia amepata kura 59, Mwalimu 14 na Juma 3.

Kituo cha Ofisi ya Mpakani -7 Kata ya Ndugumbi, Mtulia amepata kura 33, Mwalimu 20, Juma 6 na mgombea wa Tadea 1.

Kituo cha Mpakani -3 Kata ya Ndugumbi, Mtulia amepata kura 49, Mwalimu 14, Juma 16 na mgombea wa Tadea 1.

Kituo cha Serikali ya Mtaa Bwawani 4 Kata ya Kijitomyama, Mtulia amepata kura 237, Mwalimu 21 na Juma 1.

Kituo cha Bwawani 01 Kata ya Kijitonyama, Mwalimu amepata kura 23 na Mtulia 100.

Kituo cha Bwawani 2 Kata ya Kijitonyama, Mtulia amepata kura 37, Mwalimu 24 na Juma 1.

Kituo cha Weo 1 Kata ya Makumbusho, Mtulia amepata kura 35, Mwalimu 20 na Juma 3.

Kata ya Sokoni Makumbusho A-1 Kata ya Kijitonyama, Mtulia amepata kura 30, Mwalimu 12 na Ashiri Saidi 1.

Kituo cha Shule ya Msingi Mwananyamala Kisiwani B Kata ya Makumbusho, Mwalimu amepata kura 13, Mtulia kura 39 na mgombea wa UMD 1.

Kituo cha Shule ya Msingi Mwananyamala Kisiwani C 1 Kata ya Makumbusho, Mtulia amepata kura 41, Mwalimu 15 na Juma 9.

Kituo cha Shule ya Msingi Mwananyamala C 2 Kata ya Makumbusho, Mtulia amepata kura 42, Mwalimu kura 21 na Juma 15.

Kituo cha Kijitonyama 2 Kata ya Kijitonyama, Mwalimu amepata kura 20, Mtulia 29 na Juma 1.

Kituo cha Shule ya Msingi Kijitonyama B2 Kata ya Kijitonyama, Mtulia amepata kura 78, Mwalimu kura 24 na Ally Abdallah wa Tadea 1.

Kituo cha Shule ya Msingi Kijitonyama A-2 Kata ya Kijitonyama, Mwalimu amepata kura 24, Mtulia 68 na Ally Abdallah wa Tadea 1.

Kituo cha Shule ya Msingi Kisiwani D 2 Kata ya Makumbusho, Mtulia amepata kura 37, Mwalimu 21 na mgombea wa NRA 1.

Kituo cha Shule ya Msingi Minazini C 1 Kata ya Makumbusho, Mtulia amepata kura 46, Mwalimu 20 na Juma 12.

Kituo cha Ofisi ya Serikali ya Mtaa Kijitonyama 2 Kata ya Kijitonyama, Mtulia amepata kura 25, Mwalimu kura 36.

Kituo cha Ofisi ya Weo-3 Kata ya Kijitonyama, Mtulia amepata 22, Mwalimu 20.

Kituo cha Mwenge Zahanati Kata ya Kijitonyama, Mtulia amepata 19 na Mwalimu 12.

Kata ya Mwenge Zahanati 2 Kata ya Kijitonyama, Mtulia amepata kura 56 na Mwalimu 13

Updates: Matokeo Siha, mgombea wa CCM, Dk Godwin Mollel akiongoza kwa mbali katika baadhi ya vituo
Kituo cha Kirua–Kawate Kata ya Siha, Wilaya ya Siha mgombea wa CCM alipata kura 208, huku Alvis wa Chadema akipata kura 42 na Mwanri wa CUF akipata kura 10

Katika kituo cha Lawate namba 2 Kata ya Siha, CCM ilipata kura 300 na Chadema 21 huku CUF ikiambulia 0.

Kituo cha Lomakaa, CCM ilipata kura 190, Chadema 10 na CUF haikupata chochote.

Pia kituo cha Ofisi ya Kijiji Sanya Juu, CCM ilipata kura 284,Chadema 54 na CUF 1.

Kwa upande wa kituo cha Sanya Juu, CCM ilipata kura 93,Chadema 50, CUF 0, huku kituo cha Kaboko Kusini 2, CCM 403, Chadema 68 ,CUF na Sau zikiwa hazijapata kitu.

Pia Kituo kingine cha Kaboko B; CCM 106,CUF 76, Sau 0 na kituo cha Ofisi ya VEO Merali Juu1; Chadema 33, CCM 64 huku CUF na Sau vikiwa havijapata kitu. Ofisi ya VEO Merali Juu2: Chadema 22 na CCM 87.

Baadhi ya matokeo hayo ni kama ifuatavyo. Kituo cha Pyarita kata ya Nasai Mgombea wa CCM alipata kura 194 huku Alvis wa Chadema akipata kura 44 na Mwanri akipata Cuf akipata kura 5.
=====

CHADEMA kimesema kitatoa taarifa kuhusu uchaguzi uliofanyika leo, ambapo wataweka wazi hatua zilizochukuliwa kutokana na hali halisi iliyojitokeza, yakiwemo matendo yanayolitia taifa aibu

ef64fd1c582913cc8d43fd016c4a07fe.jpg

04e0db37a327ffce436ee7206cab3089.jpg
 
Leo Jumamosi, wananchi katika majimbo mawili ya uchaguzi – Siha mkoani Kilimanjaro na Kinondoni jijini Dar es Salaam watafanya uchaguzi mdogo wa wabunge kuziba nafasi zilizo wazi.

Mbali na majimbo hayo, pia utafanyika uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata tisa za Isamilo wilaya ya Nyamagana, Manzase (Chamwino), Madanga (Pangani), Mitunduruni (Singida), Kanyelele (Misungwi), Buhangaza (Muleba) na Donyomurwak, Gararagua na Kashashi wilayani Siha.

Uchaguzi huo unatokana na majimbo na kata hizo kuwa wazi kwa sababu mbalimbali, kubwa ikiwa ni kujiuzulu kwa waliokuwa wabunge na madiwani na kuhamia katika vyama vingine.

Kutokana na uchaguzi huo, tayari vyama 12 vya siasa vilivyosimamisha wagombea vimefanya kampeni kwa zaidi ya wiki tatu, shughuli ambayo inakamilika leo.

Katika kipindi hicho, kwa wastani shughuli za kampeni zimefanyika kwa utulivu na amani, ingawa katika siku za mwisho yameripotiwa matukio ya machache likiwamo la kada mmoja wa Chadema kuuawa na mwingine kujeruhiwa, huku pia kukiwa na matukio ya polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa baadhi ya vyama.

Pia, yamekuwapo madai ya baadhi ya vyama kuwa mawakala wao wanawekewa vizingiti katika kupewa barua za utambulisho, mambo ambayo tunaamini Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) itayamaliza kabla ya shughuli hiyo kufanyika.

Pamoja na kuwa uchaguzi huu unachukua sehemu ndogo tu ya nchi yetu, tunaamini kuwa unatoa picha pana kitaifa, inayoeleza kiwango cha ukuaji wa demokrasia ya nchi yetu kwa miaka 26 ya mfumo wa vyama vingi tangu mwaka 1992.

Ni uchaguzi mdogo wa kwanza kufanyika baada ya ule wa majimbo matatu ya Longido, Singida Kaskazini na Songea Mjini wa Januari ambao baadhi ya vyama vya upinzani vilisusa kutokana na madai ya kuwapo kwa kasoro katika uchaguzi mdogo wa kata 43 wa Novemba mwaka jana.

Pia ni uchaguzi ambao unafanyika katika mazingira ya ushindani mkali huku baadhi ya wagombea wakiwa wale waliovihama vyama vyao na kupoteza nyadhifa zao na kisha kuteuliwa na vyama shindani walikohamia kuwania tena nafasi hizohizo.

Ni kutokana na mazingira hayo, tunaamini kuwa vyombo vinavyohusika na usimamizi wa uchaguzi na vile vya dola, hasa Jeshi la Polisi, vinavyoangalia suala la usalama na amani, vitahakikisha haki, amani na usalama vinaimarishwa kwa kiwango kinachostahili katika maeneo yote unakofanyika uchaguzi.

Hatutarajii kuona mazingira yaliyokuwa yanalalamikiwa katika uchaguzi mdogo wa Novemba au chaguzi nyingine zilizopita yakijirudia na kuendelea kuiweka demokrasia ya nchi yetu katika majaribu.

Miaka 26 ambayo nchi yetu imepita tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe, tukiwa tumepita katika uchaguzi mkuu ulioshirikisha vyama vingi vya siasa mara tano, inatosha kujifunza, kujirudi, kusahihisha makosa na kuboresha mifumo na jinsi tunavyoendesha chaguzi zetu ili kuweka mazingira ya haki na usawa.

Ni imani yetu kuwa kila mtu kuanzia NEC, wasimamizi wa uchaguzi na vyombo vya usalama, anatambua kuwa jukumu lake ni kukaa katikati kuhakikisha mchezo unachezwa kwa haki, wananchi wapiga kura, zinahesabiwa kwa usahihi na mshindi anatangazwa bila upendeleo wowote.

Tukumbuke jambo la msingi ni utendaji wa haki kwa kuwa amani ni tunda la haki na pale inapokosekana vurugu huibuka na kuhatarisha amani.

Tunasihi wananchi wa maeneo hayo kujitokeza kwa wingi kutimiza wajibu wao huo wa kidemokrasia wa kuchagua viongozi wawatakao.

Chanzo: Mwananchi
 
Wadau tayari tupo kwenye foleni ya kupiga kura hapa Kinondoni ili tukamchague Mbunge muwakilishi wa wananchi ...nitawaletea matokeo ya mwanzo pia wenye matokeo ya awali msisite kurusha hapa....by saa 12 jioni hata kama DED watakuwa hawajatangaza mshindi sisi tutakuwa tumeshajua nani kashinda kama mkionyesha ushirikiano .R.I.P Acquiline.....
 
Niwatakieni uchaguzi mwema wa kaki na huru bila kusahau kulinda kwa mwenye kuweza
 
Police ni wengi mno, wangepungua kwenye vituo,maana inaweza ogopesha wapiga kura
 
Hali iko shwari kabisa,

ulinzi wa kutosha.

Mpaka sasa zoezi la upigwaji kura linaendelea
 
Back
Top Bottom