Zoezi la uhakiki limeisha serikali yaanza kuajiri watumishi wapya.

nkanga chief

JF-Expert Member
May 31, 2016
2,084
1,620
hayo aliyasema waziri mkuu jana jijini dar es salaam akiwa anahutubia watumishi wa umma pamoja na madiwani ilala ikiwa ni moja ya ziara anazozifanya humo mh.kasimu majaliwa kuwa zoezi la kuhakiki watumishi hewa limeisha na kuwa watumishi ambao wapo ni halali hivyo serikali imeanza kuajiri kama kawaida
 
SERIKALI KUANZA KUAJIRI, KUTOA VIBALI VYA UHAMISHO,KUPANDISHA MADARAJA, SOURCE TANZANIA DAIMA.

serikali inatarajia kuanza kutoa ajira mpya na kupandisha vyeo watumishi wa umma baada ya agizo la rais john pombe magufuli la kusitisha utaratibu huo kupisha uhakiki wa watumishi hewa kukamilika. jana waziri mkuu kasim majaliwa akiendelea na ziara yake jijini dsm na kuzungumza na watumishi,wabunge na madiwani alisema UHAKIKI UMEKAMILIKA. tumekamilisha uhakiki na watumishi waliopo ni HALALI, Aliendelea kusema mtumishi yeyote atakayepandishwa cheo mwezi huo huo anaanza kupata stahiki zake maramoja. hivi sasa tumebadili mfumo, mtumishi atapandishwa cheo wakati huhuo tayari utaratibu utakuwa umeandaliwa kurekebisha mishahara na stahiki zake na ninaomba maofisa utumishi hili liwe linafanyika kabla ya tarehe10 ili wahasibu wa halmashauri wawe hawajafunga na hili ni watumishi wote hadi walimu. chanzo tanzania daima ijumaa agost 19, 2016.
 
1471619530501.jpg
 
nasikia waziri jafo kasema leo watumishi waliomasomoni wahakikiwe
 
Mbona wanasema watumushi wote hadi walimu!? Kwani ukisema watumishi wote! Na walimu si miongoni mwao.

Amenikumbusha zamani kidogo! Huko Bukoba ilikuwa ukiingia hotelini; ukiulizia chakula unaambiwa: "Chakula kimeisha! Umebaki UGALI tu"
Kwa sababu walimu ni watu "very special "
 
ni jambo zuri sana kwa serikali yetu kuanza kuajili tena na nijambo la kushukulu sana Mungu vijana tuchangamkie tenda kwani maisha ni pesa na pesa ni kazi kwa bidiiiii
 
Mbona wanasema watumushi wote hadi walimu!? Kwani ukisema watumishi wote! Na walimu si miongoni mwao.

Amenikumbusha zamani kidogo! Huko Bukoba ilikuwa ukiingia hotelini; ukiulizia chakula unaambiwa: "Chakula kimeisha! Umebaki UGALI tu"
Umewaza kama mm
 
Uzi umedoda huu baada ya Jafo kusema wanahakiki wafanyakazi walioenda kujiendeleza elimu zao mavyuoni..usimuamini mwanasiasa hata kama Baba/Mama ako
 
Huwa sipendi upotoshaji....Jaffo nilimsikia vizuri...alisema ameagiza waanze kuhakikiwa watumishi waliopo masomoni....Lakini pia aliongeza kusema.."watumishi hewa tayari tumewabaini lakini kuna watumishi wanasema wapo masomoni kumbe sio kweli"...

It is very clear kwamba miongoni mwa watumishi halali wanaendelea kupitia mambo mbalimbali kama hilo na kuondoa wenye vyeti vya Buguruni...Na hili halifuti kauli ya PM na kikatiba kauli ya waziri mkuu ni kauli ya serikali
 
Back
Top Bottom